Inasikitisha kanisa katolilki nalo limeingia kwenye kundi la makanisa ya mchongo; ushahidi huuu hapa!

Unafikiri utapata wa kubishana naye waumini wenyewe wanajua nini wanaamini .
Wewe hapa umefanyaje mkuu? Waumini wanauziwa nini kanisani hadi wakamuliwe pesa nyingi kihivyo?
 
Ukiacha kizazi cha miaka 2000 iliyopita cha Yesu, hata kizazi cha akina Isaac Newton hakuna picha zao, isipokuwa zinatumika potrait.

A portrait is an artistic representation, such as a painting, photograph, or sculpture, that focuses on capturing the likeness and personality of a person. It often emphasizes the face and its expression, aiming to reveal the subject's character, mood, or even a specific moment in time.
Kwa hiyo hiyo picha uliyoiona hapo kwenye kitenge ni portrait ya Yesu mkuu?
 
Kabla ya kuandika uzi huu, naomba kutangaza maslahi kuwa mimi ni mmojawapo wa watu waliokuwa wakiliamini kanisa katoliki 100% hadi juzi nilipogundua kuwa hata kanisa katoliki nalo kumbe ni kanisa kanjanja kama yalivyo makanisa mengine ya ovyo hapa nchini Tanganyika.

Katika pitapita zangu za hapa na pale nilikutana na kipande hiki cha kitenge kikiwa kimevaliwa na mkatoliki mmoja hadharani bila wasiwasi. Tazama walivyochemeka picha ya "Yesu" katikati ya maandishi. Mwenye macho haambiwi tazama. Jamani eti huyu ndiye Yesu?

View attachment 3389578
Nimeshangaa sana kuona kanisa katoliki nalo limejaa matapeli kama walivyo akina Mwamposa, Kuhani Musa, GeoDavie, Mzee wa Upako, Kiboko ya Wachawi na matapeli wengine waliotapakaa hapa nchini Tanganyika.

MAONI YANGU
Nilidhani kanisa katoliki ndilo kanisa la kweli ambamo makanisa mengine ya mchongo kama Anglikana, KKKT, Assemblies, Maranatha, Orthodox n.k yamechipuka, lakini sasa naamini kanisa hili nalo ni wapigaji tu kama akina Mwamposa.

Pia nimeamini mafundisho mengi kutoka kwenye biblia yanatumiwa na wajanja wachache kwa manufaa yao binafsi, wakiwemo pia mapadri wa kanisa katolliki. Kwa mfano, siku zote tunasisitizwa kutoa sadaka na fungu la kumi kwa ajili ya kuinua kazi ya Mungu kumbe pesa hizo zinatumika kuinuua matumbo ya wajanja wachache wanaojiita viongozi wa makanisa.

Mfano halisi ni namna ambavo Mwamposa alipiga hela za sadaka akaenda kujengea hoteli ya nyota tano, ambayo ni mali yake binafsi na mapato yote yanayotokana na hoteli ile yanatumika kumnufaisha yeye na familia yake tu. Hii ndio kazi ya "Mungu" ambayo siku zote tunahimizwa kutoa sadaka kwa ajili hiyo ilhali mapato ya sadaka yanaenda kuinua uchumi wa watu binafsi.Kama sadaka zingetumika kujenga sunagogi hapo kweli zingekuwa zimefanya kazi ya Mungu. Kinyume na hapo, zimetumika kujenga uchumi wa MunguMtu.

Haya ndiyo mambo ambayo kanisa katoliki nalo linatufanyia. Kila mwaka tunachangishwa mamilioni ya michango na kukamuliwa sadaka na mafungu ya kumi lakini mwisho wa siku fedha zote hutumwa kwenda Roma, Italia kuwanufaisha wazungu huku watoaji sadaka wakiambulia patupu. Huu ni uhuni unaopaswa kukemewa na kila mtu anayewatakia mema sio tu watanganyika bali waafrika wote kwa ujumla. Utumwa huu wa kiimani ifike wakati ukomeshwe kwa nguvu zote.
Nauli ya kwenda Makka Sasa hivi milioni 16 mkuu.
Halafu bado ukifika kule utauziwa mawe saba ya kumrushia shetani
 
Huo nao pia ni utapeli mkuu. Tuuepuke
 
Sadaka inaanza nyumbani kwako then watu wa karibu yako then jirani zako then watu unajua huyu anashida sio kutoa katika kanisa wanajilia watu kimya kimya
 
Makanjanja ni wewe mwenyewe na siyo Kanisa Katoliki, wewe unamwamini Mungu au unaamini Kanisa?
 
Kwa hiyo hiyo picha uliyoiona hapo kwenye kitenge ni portrait ya Yesu mkuu?
Ndiyo, ni portrait. Na hata wewe unaweza ukaja na portrait yako ya Yesu au Muhamedi au Einstein. Ni jambo dhahiri kabisa kuwa hakukuwapo teknolojia ya kuhifadhi picha enzi zao, lakini wabongo wengi hujidai ujuaji kwa kuanzisha malumbano ambayo jibu lake ni dhahiri kabisa.

Yaani ukaona ile picha, ukaishangaa, ukaja kuanzishia kabisa uzi kuwa wanawadanganya watu kuwa ni picha ya Yesu? Wamekuambia yule ndiye Yesu kwa sura kabisa ile?
 
Kwa hiyo hiyo picha uliyoiona hapo kwenye kitenge ni portrait ya Yesu mkuu?
Portraits nyinine hizi hapa, siku nyingine hauna haja ya kushangaa mapichapicha:

1751435757669.png
 
Na kukusaidia ili uelewe logic ya kumpa mtu ID, ni kwamba Kanisa Katoliki huwa lina utaratibu huo pale ambapo haikutajwa katika maandiko yoyote, kama ambavyo picha ya Yesu haipo katika maandiko au kumbukumbu zozote. Mfano wa hili ni wale mamajusi watatu wa Mashariki walioenda kumtafuta Yesu baada ya kuiona nyota yake (kiuhalisia walikuwa wanatumia nguvu za giza kuangalia nyota, na walikuja kumrudia Mungu baada ya kutii maagizo yake ya kutompelekea Herode taarifa). Wale jamaa majina yao hayajatajwa katika Biblia au kumbukumbu, lakini ili kuwatambulisha katika mafundisho, walipewa ID kuwa ni Caspar (Gaspar), Balthazar na Melchior
 
Naomba unioneshe portrait ya YESU tufunge huu mjadala mkuu. Inawezekana hiyo picha iliyo kwenye kitenge ni portrait ya YESU.
Mojawapo ndio hiyo uliyoiona kwenye kanga. Mwingine anaweza akaja na version yake. Kumbuka lugha ni sauti za nasibu (hopefully ulipita shule japo kidogo ndio maana walau unaweza kusoma na kuandika)
 
Nalipenda sana Kanisa Takatifu Katoliki la Roma.

Mimi ni Mkatekumeni
 
Mojawapo ndio hiyo uliyoiona kwenye kanga. Mwingine anaweza akaja na version yake. Kumbuka lugha ni sauti za nasibu (hopefully ulipita shule japo kidogo ndio maana walau unaweza kusoma na kuandika)
Huyo mtu kwenye kitenge ni Brian Deacon. Aliigiza filamu ya Yesu kama portrait ya Yesu?
 
Lengo ni nini? Kanisa limefanya makubwa kama serikali tu, sababu za kitenge kuingiza hapa inaelekea nia ovu ilikuwepo, uzi wako hauna cha maana.
 
Huyo mtu kwenye kitenge ni Brian Deacon. Aliigiza filamu ya Yesu kama portrait ya Yesu?
Portrait ya Yesu ilifanyiwa usanifu mwaka 300 AD, yaani karne ya nne. Deacon alizaliwa mwaka 1947 na aliigiza filamu hiyo mwaka 1979, hiyo ilikuwa karne ya 20.

Ukiwa na akili walau za kuvukia barabara utaona kipi kilipotray kingine. Je, wasanifu walimportray Deacon wa karne ya 20 au Deacon aliportray portait ya Yesu iliyokuwapo tangu karne ya nne?

NB: muigizaji Eddie Murphy katika filamu ya Coming to America, ametokea kama watu wanne tofauti

Screenshot_2025-07-03-05-58-31-414_org.mozilla.firefox.jpg
 
Portrait ya Yesu ilifanyiwa usanifu mwaka 300 AD, yaani karne ya nne. Deacon alizaliwa mwaka 1947 na aliigiza filamu hiyo mwaka 1979, hiyo ilikuwa karne ya 20.

Ukiwa na akili walau za kuvukia barabara utaona kipi kilipotray kingine. Je, wasanifu walimportray Deacon wa karne ya 20 au Deacon aliportray portait ya Yesu iliyokuwapo tangu karne ya nne?

NB: muigizaji Eddie Murphy katika filamu ya Coming to America, ametokea kama watu wanne tofauti

View attachment 3392173
Afadhali umejijibu mwenyewe. Naona sasa tumeanza kuongea lugha moja mkuu. Kwa hiyo sasa tunakubaliana kuwa picha ya huyo mtu aliyepo kwenye kitenge sio portrait ya Yesu bali ni picha ya Brian Deacon aliyeigiza filamu ya Yesu. Je ni sahihi wakatoliki kumtumia kama mfano wa Yesu kwenye misalaba na katika maandiko yao?
 
Kabla ya kuandika uzi huu, naomba kutangaza maslahi kuwa mimi ni mmojawapo wa watu waliokuwa wakiliamini kanisa katoliki 100% hadi juzi nilipogundua kuwa hata kanisa katoliki nalo kumbe ni kanisa kanjanja kama yalivyo makanisa mengine ya ovyo hapa nchini Tanganyika.

Katika pitapita zangu za hapa na pale nilikutana na kipande hiki cha kitenge kikiwa kimevaliwa na mkatoliki mmoja hadharani bila wasiwasi. Tazama walivyochemeka picha ya "Yesu" katikati ya maandishi. Mwenye macho haambiwi tazama. Jamani eti huyu ndiye Yesu?

View attachment 3389578
Nimeshangaa sana kuona kanisa katoliki nalo limejaa matapeli kama walivyo akina Mwamposa, Kuhani Musa, GeoDavie, Mzee wa Upako, Kiboko ya Wachawi na matapeli wengine waliotapakaa hapa nchini Tanganyika.

MAONI YANGU
Nilidhani kanisa katoliki ndilo kanisa la kweli ambamo makanisa mengine ya mchongo kama Anglikana, KKKT, Assemblies, Maranatha, Orthodox n.k yamechipuka, lakini sasa naamini kanisa hili nalo ni wapigaji tu kama akina Mwamposa.

Pia nimeamini mafundisho mengi kutoka kwenye biblia yanatumiwa na wajanja wachache kwa manufaa yao binafsi, wakiwemo pia mapadri wa kanisa katolliki. Kwa mfano, siku zote tunasisitizwa kutoa sadaka na fungu la kumi kwa ajili ya kuinua kazi ya Mungu kumbe pesa hizo zinatumika kuinuua matumbo ya wajanja wachache wanaojiita viongozi wa makanisa.

Mfano halisi ni namna ambavo Mwamposa alipiga hela za sadaka akaenda kujengea hoteli ya nyota tano, ambayo ni mali yake binafsi na mapato yote yanayotokana na hoteli ile yanatumika kumnufaisha yeye na familia yake tu. Hii ndio kazi ya "Mungu" ambayo siku zote tunahimizwa kutoa sadaka kwa ajili hiyo ilhali mapato ya sadaka yanaenda kuinua uchumi wa watu binafsi.Kama sadaka zingetumika kujenga sunagogi hapo kweli zingekuwa zimefanya kazi ya Mungu. Kinyume na hapo, zimetumika kujenga uchumi wa MunguMtu.

Haya ndiyo mambo ambayo kanisa katoliki nalo linatufanyia. Kila mwaka tunachangishwa mamilioni ya michango na kukamuliwa sadaka na mafungu ya kumi lakini mwisho wa siku fedha zote hutumwa kwenda Roma, Italia kuwanufaisha wazungu huku watoaji sadaka wakiambulia patupu. Huu ni uhuni unaopaswa kukemewa na kila mtu anayewatakia mema sio tu watanganyika bali waafrika wote kwa ujumla. Utumwa huu wa kiimani ifike wakati ukomeshwe kwa nguvu zote.
What are you trying to say

Umeandika kama mtu aliyechanganyikiwa ,kichwa cha habari ukatoliki ndani ya mada mara Mwamposa mara KKKT,Hueleweki unaongelea kitu gani?

Rudi shule ukasome upya

Mambo ya ukatoliki yanakuhusu nini?Huo ukatoliki ulikuwepo kabla Babu yako na Mama yako hawajazaliwa

Acha vichekesho na vituko,Mama yako kabla hajazaliwa ukatoliki upo,Wewe umeukuta

Unafahamu maana ya Sanamu huko katoliki?
Unafahamu sheria za kanisa katoliki?

Hao katoliki wana taratibu zao wenyewe,wewe unawashwa nini?
 
Back
Top Bottom