Inasikitisha na kuumiza kweli: Hapa ndo tulipofika Tanzania, Taifa na Wajinga na Ujinga

Inasikitisha na kuumiza kweli: Hapa ndo tulipofika Tanzania, Taifa na Wajinga na Ujinga

Kama ni Rais ndo wavae t-shirt zenye sura yake? Ndo wavae t-shirt zenye jina lake?

Kwa hiyo ni Tanzania tu ndo tuna Rais au Kiongozi nchi zingine hawana? Mbona kwenye mataifa mengine ya watu wenye akili hawafanyi huo upuuzi wenu?
Tumefika nchi ngapi dada?!!! Ipi na ipi?!!!!!
 
Usilaumu watu!
Wakulaumiwa ni wale wenye kuifinyanga kesho ya Tanzania!

Walijisahau wakaanza kucheza beat za wanasiasa badala ya mstakabali wa kesho yetu!!

Chama tawala kimefanywa Cha maana kuliko jamuhuri iliyoanza mwaka 1964!!

The state watuombemsamaha wametukosea sana !wameifanya siasa kuwa ndio KAZI Bora na kuua elimu ionekanekituko hata kama wewe ni profesa unajiona ni wa jalalani!!
Hao wa kulaumiwa nao si wanawekwa na huyo huyo?
 
Ndio pesa za mikopo vinavyotumika hovyo ,tafrija ,misafara na anasa .

Ukitajiwa pesa iliyotumika kusafirisha wapambe na machawa , PR team kuprint hizo fulana, kofia na vitu vingine , malazi,posho na viburudisho vingine kila siku baada ya ziara hakika unaweza kuzimia, kwa kujiuliza ni nchi hiyo hiyo ndio inaongozwa kwa kutembeza bakuli la misaada kwa wahisani ilhali hata bajeti ya mwaka bado inafadhiliwa kwa 40% ya mikopo ya wahisani bado kuna utapanyaji mkubwa wa fedha kwa shughuli na mambo yasiyo na tija.

Inashangaza na kusikitisha ila inajidhihirisha jinsi nchi inavyoongozwa na watu waliopoteza dira hivyo nchi inaelekea mahali ambapo hapafai.
 
Uko sawa ila kwa namna unavyotafsiri mambo na kutasimamia, napata mashaka kwa wanafunzi unaowafunza, napata mashaka na diplomasia yako, nahisi we ni mwanasarakasi wa kimataifa kama ulivyojitambulisha.

Na kuhusu uadhiri huenda unafundisha tuition ya chuo kikuu labda.

Ila unareflect taswira ya wasomi wa Tanzania ndiyo maana nchi iko hivi kwaajili yenu ninyi, yani me na elimu yangu hii ya bachelor degree siwezi kubaliana na mwwnendo huu ila wewe mhadhiri unapongeza ety?
nacheza sarakasi balaa gentleman, na siachi,
na hata majuzi kakitambi kalitaka kuniletea ugumu lakini nimekadhibiti vizuri nasasa nasonga mbele vizur sana,

hayo mengine staki kueleza sana kwasababu bado niko kazini na ninsonga mbele vizuri sana, na wengi wanaopitia mikononi mwangu sio rahisi kabisa kutapeliwa na vibaka wa siasa kama ilivyo kwa baadhi ya vijana waliopitia mikononi mwa wengine kitaaluma.

napenda kilimo, napenda ufugaji, biashara na hata kuhubiri na kusaidia kuwapeleka watu wacha Mungu mbinguni,

nitaendelea kua nanyi humu jukwaani mara zote ninapopata nafasi, ili kusudi kwa pamoja tuendeleze umoja, amani na utangamano kama Taifa la watu wastaarabu duniani licha ya utofauti wa mirengo na imani tofauti za kidini na kisiasa pia :NoGodNo:
 
Haya sawa mchungaji tufanyie maombi hii nchi ilipofikia ni kama jehanamu. 😂🙏🏾
 
Watendaji wa Serikali kumsikiliza kiongozi ndo wavae kofia zenye jina lake? Ndo wavae T shirt zenye picha yake?

Kwa nini mapenzi kwa kiongozi badala Taifa? Tumekuwa nchi ya namna gani sisi?
Watendaji wa Serikali kumsikiliza kiongozi ndo wavae kofia zenye jina lake? Ndo wavae T shirt zenye picha yake?

Kwa nini mapenzi kwa kiongozi badala Taifa? Tumekuwa nchi ya namna gani sisi?
Kazi unayo Mwaka huu na ndio kwanza mwezi wa Tatu hata ukifika wa kumi nakuhakikishia unaenda kuwa Chizi makopo yanakuhusu mate.
 
Uchawa tumshukuru muasisi wa uchawa asa the kwa kuupenda uchawa oyeee,eeee
 
Sikufurahishwa na anguko la taifa lile lakini ilibidi nitazame anguko la taifa lile
 
Watu wanawaza kuwalamba miguu Viongozi na kuwa machawa wao ili waendelee kula. Hawawazi maslahi mapana na Tanzania na kesho njema ya Taifa letu.

Viongozi badala ya kuelekeza fedha zikawahudumie Wananchi ikiwemo kununua madawa, kuweka miondombinu bora ya elimu kwa watoto wetu inayohudumiwa na kutunzwa vizuri muda wote, wao wanazielekeza kwenye ku print kofia, t shirt na kanga za kumuabudu Kiongozi ili aendelee kuwateua na waendelee kula.

Hakuna anayeumiza kichwa kuwaza Dunia ilipo na changamoto zake Tanzania tuweje na tufanye nini ili tuwe nchi imara inayojitegemea na kutegemewa na wengine kiuchumi na kila kitu.

Kwa sasa ni kama wote hatuwazi, hatufikirii, tumepigwa upofu na wala hatuiangalii Tanzania ya kesho na Watoto wake inapaswa kuwaje.

Naionea huruma Tanzania. Naumia kuishi nyakati ambazo Tanzania inakufa huku naiona.

Tumekuwa Taifa la Wajinga na Ujinga
View attachment 3254495View attachment 3254496View attachment 3254497View attachment 3254498View attachment 3254499View attachment 3254500View attachment 3254501View attachment 3254502View attachment 3254503View attachment 3254504View attachment 3254505
Mkuu wewe save hizi picha ni swala la muda tuu, chuma huliwa na kitu, mtu huzali na kufa vile vile.
 
Back
Top Bottom