Inasikitisha na kuumiza kweli: Hapa ndo tulipofika Tanzania, Taifa na Wajinga na Ujinga

Inasikitisha na kuumiza kweli: Hapa ndo tulipofika Tanzania, Taifa na Wajinga na Ujinga

Usalama wanapigaje marufuku uchawa ? Na ni lini umewahi kusikia wamepiga marufuku kitu au jambo ?
Sio lazima watoke kusema mzee, wana weza Waka Wapa maelekezo hao viongozi wa juu

Kwani mkuu wa usalama nnae si mshauri wa serikali?, au una dhani kazi yake kubwa ni kulinda watu tu?

Kuna usalama wa uchumi, afya, na hata sekta nyingine.
 
Na akili za namna hii ndo zimejaa huko CCM na zinaliangamiza Taifa letu. Wanaendekeza fikra na akili za kijinga kiasi ambacho hawatumii tena akili na maarifa kulisadia Taifa na Wananchi wake kuondokana na shida walizonazo na umaskini huu wa kutisha.
Ninapo jibishana na mtu JF, hasa kwenye maswala ya nchi na maslahi ya wananchi wake huwa sipotezi kumbukumbu ya majibishano na mtu kama huyo.
Sasa ninajiuliza, hii lugha unayotumia katika hizi siku za hivi karibuni imetoka wapi?

Hapana, usidhani natafuta kukusuta; nasherehekea tu haya mawazo yako mapya yanayotia moyo sana.
 
Watu wanawaza kuwalamba miguu Viongozi na kuwa machawa wao ili waendelee kula. Hawawazi maslahi mapana na Tanzania na kesho njema ya Taifa letu.

Viongozi badala ya kuelekeza fedha zikawahudumie Wananchi ikiwemo kununua madawa, kuweka miondombinu bora ya elimu kwa watoto wetu inayohudumiwa na kutunzwa vizuri muda wote, wao wanazielekeza kwenye ku print kofia, t shirt na kanga za kumuabudu Kiongozi ili aendelee kuwateua na waendelee kula.

Hakuna anayeumiza kichwa kuwaza Dunia ilipo na changamoto zake Tanzania tuweje na tufanye nini ili tuwe nchi imara inayojitegemea na kutegemewa na wengine kiuchumi na kila kitu.

Kwa sasa ni kama wote hatuwazi, hatufikirii, tumepigwa upofu na wala hatuiangalii Tanzania ya kesho na Watoto wake inapaswa kuwaje.

Naionea huruma Tanzania. Naumia kuishi nyakati ambazo Tanzania inakufa huku naiona.

Tumekuwa Taifa la Wajinga na Ujinga
View attachment 3254495View attachment 3254496View attachment 3254497View attachment 3254498View attachment 3254499View attachment 3254500View attachment 3254501View attachment 3254502View attachment 3254503View attachment 3254504View attachment 3254505
Ujinga ni mtaji!! Jitajidi sanaa kufuta ujinga kwa vizazi vyako maana watakuwa mtaji kwa watu werevu. Ujinga hauna umri. Tuombe sanaa Mungu atusaidie Taifa letu lisiangamie! Tunaanza kuona makucha ya Wazungu kupitia Trump....
 
Sijaona mfano halisi wa mtu, muadilifu ambaye ana mtukuza Binadamu mwenzie awe muarabu, muhindi, mtu mweupe au mchini. Anayefanya hivyo ni mapungufu yake ya kuijua dunia inavyo kwenda
Uoni waislamu wa matumbi wanavyo mtukuza muarabu wa gaza ..Palestina na kutokuongelea chochote kuhusu wabantu wenzao wanao chinjagwa africa yote hata Sudan nk upishawa kumsikia muarabu akimuulimia mtu mweusi kwa vita au akimtakia amani hata kwenye mauaji ya kimbari ya rwanda uliwai kusikia washenzi wa kiarabu wakisema kitu chochote au kutoa msahada wowote wa maana
 
Mbona kama ni hivyo madai ya waisiharamu kwa uongozi wa nyerere ni hivyo hivyo ...kama unacho sema ni kweli basi madai ya waislamu wakimlaani nyerere yanatokaga wapi tumia akili wacha upumbavu.
Hauko sawa, sijatetea mtu wala kiongozi kulingana na dini yake na madhaifu yake, ninachojaribu kukifanya ni kukuelewesha wewe na wengine wenye mitizamo ya kulinganisha viongozi, uongozi, na udini au ukabila wao kuwa hicho kitu si sawa na hakifai kukishikilia, kama raisi fulani amefanya makosa basi tumtizame yeye kwa upande wake na wala sio kwa udini au ukabila wake hapo umenielewa.

Kwenye nchi kama hii ukiweka mambo kama hayo utaleta mpasuko ndani ya nchi na ni ishara za ubaguzi.

Kwenye hii nchi kuna watu wenye imani za kidini tofauti tofauti, inapaswa wote wawe kitu kimoja na wote watawaliwe kama wananchi bila kuwagawa kwa makundi makundi.
Mkuu, hii ni nchi sio sehemu ya ibada au sehem ya kutafuta waumini mzee.
 
Sio lazima watoke kusema mzee, wana weza Waka Wapa maelekezo hao viongozi wa juu

Kwani mkuu wa usalama nnae si mshauri wa serikali?, au una dhani kazi yake kubwa ni kulinda watu tu?

Kuna usalama wa uchumi, afya, na hata sekta nyingine.
Sasa kama allshauri wakapuuza ?
 
Hutokuja kunielewa ,kwanza mimi sijawahi kupiga kura wala sina kitambulisho cha kura ..Nina uhakika CCM watashinda tu japo sina chama.

CCM imesheheni watoto wa mjini ,wana mbinu zote za ushindi ,wana vyanzo vingi vya mapato kila mkoa ,chama cha muda mrefu sana kinajua kila aina ya uchafu..

Wewe usijidanganye bora upiganie familia yako kimpango wako ,si kwa kizazi hiki kuwatoa sahau ...Halafu kama hapo hamna tatizo maana hizo kofia wamenunua CCM..

Sasa unaweka picha za watu kwa kuwaona kama hawana akili ,hao wengi ni watumishi wameenda kuhudhuria mualiko wa bosi wao (Rais).

KIUFUPI: Unaumiza kichwa kwa kitu ambacho hakiwezekani kabisa.​
Laah!
Sasa na wewe unataka mjadala na mimi, kweli?
Tutaanzia wapi wakati nikisoma mabandiko yako yote humu yanavyo eleza upungufu mkubwa sana siyo kielimu tu, bali hata katika maarifa ya aina yoyote?
Maana ya kutokujibu mwenyewe moja kwa moja ni kuepuka kufukuzana na mtu asiyekuwa na sifa za kufukuzana naye.
Kikawaida huwa muda wa kupoteza na mtu nisiyeweza kufaidika na chochote kimawazo kwake huwa sina.
Natumaini utakuwa umenielewa vizuri.
 
Hauko sawa, sijatetea mtu wala kiongozi kulingana na dini yake na madhaifu yake, ninachojaribu kukifanya ni kukuelewesha wewe na wengine wenye mitizamo ya kulinganisha viongozi, uongozi, na udini au ukabila wao kuwa hicho kitu si sawa na hakifai kukishikilia, kama raisi fulani amefanya makosa basi tumtizame yeye kwa upande wake na wala sio kwa udini au ukabila wake hapo umenielewa.

Kwenye nchi kama hii ukiweka mambo kama hayo utaleta mpasuko ndani ya nchi na ni ishara za ubaguzi.

Kwenye hii nchi kuna watu wenye imani za kidini tofauti tofauti, inapaswa wote wawe kitu kimoja na wote watawaliwe kama wananchi bila kuwagawa kwa makundi makundi.
Mkuu, hii ni nchi sio sehemu ya ibada au sehem ya kutafuta waumini mzee.
Ni waislamu ndiyo wanao leta mipasuko ndiyo maana tuna usema huu ukweli....
 
Ujinga ni mtaji!! Jitajidi sanaa kufuta ujinga kwa vizazi vyako maana watakuwa mtaji kwa watu werevu. Ujinga hauna umri. Tuombe sanaa Mungu atusaidie Taifa letu lisiangamie! Tunaanza kuona makucha ya Wazungu kupitia Trump....
Mkuu umesema vyema sana, sasa wakuu wa kimataifa watoaji wa misaada wanaanza kujitoa kwenye kuzisaidia nchi zinazoendelea, badala ya kuanza kufikiria namna ya kujitegemea tusitokomee kwenye depression watu wanaanza kutizama udini, hili bara la Afrika sijui lina matatizo gani, yani watu hawajali kuhusu maisha na kujiboresha wao na vizazi vyao wanawaza uchama na udini duh.
Is so Tragedy to be born in Africa especially in Tanzania.
 
Sasa kama allshauri wakapuuza ?
Mkubwa samahani huwa una utaratibu wa kusoma au kufatilia makala za wenzetu?.

Wenzetu uki enda nje ya maelekezo yenye kujenga, una andaliwa option 2.

aidha uondolewe kwa kupewa ushahidi wa maamuzi yako mabovu yaliyo leta hasara, au upumzishwe kwa kupewa ugonjwa.
 
Ni waislamu ndiyo wanao leta mipasuko ndiyo maana tuna usema huu ukweli....
Sawa uko sawa ila simama katika upande wa kuelimisha kujenga na kutatua changamoto katika jamii yako, si kila mwenye smartphone na anayetype humu amesoma mzee, usiwe sehemu ya waharibifu wa jamii na nchi kwa ujumla.

Kemea ujinga kwa lengo kujenga taifa.
 
Watendaji wa Serikali kumsikiliza kiongozi ndo wavae kofia zenye jina lake? Ndo wavae T shirt zenye picha yake?

Kwa nini mapenzi kwa kiongozi badala Taifa? Tumekuwa nchi ya namna gani sisi?
Una umiza kichwa chako mzee tafuta chimbo lako ulambe asali hata hao waliovaa hivo wametafuta Chimbo lao wanalamba asali tuu
 
Mkubwa samahani huwa una utaratibu wa kusoma au kufatilia makala za wenzetu?.

Wenzetu uki enda nje ya maelekezo yenye kujenga, una andaliwa option 2.

aidha uondolewe kwa kupewa ushahidi wa maamuzi yako mabovu yaliyo leta hasara, au upumzishwe kwa kupewa ugonjwa.
Makala za wenzetu wa wapi ?
 
Una umiza kichwa chako mzee tafuta chimbo lako ulambe asali hata hao waliovaa hivo wametafuta Chimbo lao wanalamba asali tuu
Kama tumefikia kuwa na akili za namna hii basi tukubaliane tu Taifa letu limeshajifia. Lizikwe tu!
 
Sikubaliani na msemo huo.
Huo ndio ujinga wenyewe.
Kwa maana hiyo, tusherehekee "zama" za kiujima kama hizi tulizomo sasa?
Huwezi pingana na kanuni za kiulimwengu.

Asiyebadilika ni Mungu tu ila mambo yetu sisi wanadamu yana mabadiliko.

Hata kitabu cha biblia, kina Agano la kale na Jipya.
 
Una umiza kichwa chako mzee tafuta chimbo lako ulambe asali hata hao waliovaa hivo wametafuta Chimbo lao wanalamba asali tuu
Njaa haiishi kwa kuwa na uhakika wa kula siku moja, tumbo halijawahi kujaa, kusupport makosa kwaajili ya kujipatia kipato cha kutatua shida za msimu na kubaki na majanga ya muda mrefu huo ni ukichaa, be rational, tusihimizane kufanya upumbavu unaoangamiza nchi, hatuma misimamo wala mitazamo ndiyo maana wanasiasa wanatuchezea akili wanavuna wanatuacha masikini.

Njaa ya siku moja isikufanye mtumwa wa milele mkuu inawezekana kuwa na hiyo asali unayoizungumzia wewe kila siku kama tu utaamua na kuwa na mosimamo ya kutotumika kusupport upumbavu.

Unapewa t shirt, kofia na kaka af kila kikao elf hamsini, then kampeni zinaisha october ndani ya miaka mitano baada ya uchaguzi wa october utaishi katika mazingira gani?
 
Tuwalee watoto wetu vyema uenda wakaja kufanya jambo uko mbeleni.

Kizazi cha 60 kurudi nyuma ndio hao wazee wameshikilia kila kitu sasa huwa wanapanga mikakati ya kurithisha nasi za uongozi kwa watoto wao.

Kizazi cha 70-80 wamekua machawa waandamizi

Kizazi cha 90 ni kama vile wapo bize zaidi na maisha yao. Hawatilii mkazo sana habari za siasa.

Kizazi cha 2000[GenZ). Hiki ndio kizazi mfu kabisa. sio wa kuwategemea kwa chochote.

Tuwakuze vyema watoto wetu wa kuanzia 2020, uenda wakaja kufanya jambo uko mbeleni
 
Back
Top Bottom