Inasikitisha na kuumiza kweli: Hapa ndo tulipofika Tanzania, Taifa na Wajinga na Ujinga

Kama ni Rais ndo wavae t-shirt zenye sura yake? Ndo wavae t-shirt zenye jina lake?

Kwa hiyo ni Tanzania tu ndo tuna Rais au Kiongozi nchi zingine hawana? Mbona kwenye mataifa mengine ya watu wenye akili hawafanyi huo upuuzi wenu?
Tumefika nchi ngapi dada?!!! Ipi na ipi?!!!!!
 
Hao wa kulaumiwa nao si wanawekwa na huyo huyo?
 
Ndio pesa za mikopo vinavyotumika hovyo ,tafrija ,misafara na anasa .

Ukitajiwa pesa iliyotumika kusafirisha wapambe na machawa , PR team kuprint hizo fulana, kofia na vitu vingine , malazi,posho na viburudisho vingine kila siku baada ya ziara hakika unaweza kuzimia, kwa kujiuliza ni nchi hiyo hiyo ndio inaongozwa kwa kutembeza bakuli la misaada kwa wahisani ilhali hata bajeti ya mwaka bado inafadhiliwa kwa 40% ya mikopo ya wahisani bado kuna utapanyaji mkubwa wa fedha kwa shughuli na mambo yasiyo na tija.

Inashangaza na kusikitisha ila inajidhihirisha jinsi nchi inavyoongozwa na watu waliopoteza dira hivyo nchi inaelekea mahali ambapo hapafai.
 
nacheza sarakasi balaa gentleman, na siachi,
na hata majuzi kakitambi kalitaka kuniletea ugumu lakini nimekadhibiti vizuri nasasa nasonga mbele vizur sana,

hayo mengine staki kueleza sana kwasababu bado niko kazini na ninsonga mbele vizuri sana, na wengi wanaopitia mikononi mwangu sio rahisi kabisa kutapeliwa na vibaka wa siasa kama ilivyo kwa baadhi ya vijana waliopitia mikononi mwa wengine kitaaluma.

napenda kilimo, napenda ufugaji, biashara na hata kuhubiri na kusaidia kuwapeleka watu wacha Mungu mbinguni,

nitaendelea kua nanyi humu jukwaani mara zote ninapopata nafasi, ili kusudi kwa pamoja tuendeleze umoja, amani na utangamano kama Taifa la watu wastaarabu duniani licha ya utofauti wa mirengo na imani tofauti za kidini na kisiasa pia
 
Haya sawa mchungaji tufanyie maombi hii nchi ilipofikia ni kama jehanamu. 😂🙏🏾
 
Watendaji wa Serikali kumsikiliza kiongozi ndo wavae kofia zenye jina lake? Ndo wavae T shirt zenye picha yake?

Kwa nini mapenzi kwa kiongozi badala Taifa? Tumekuwa nchi ya namna gani sisi?
Watendaji wa Serikali kumsikiliza kiongozi ndo wavae kofia zenye jina lake? Ndo wavae T shirt zenye picha yake?

Kwa nini mapenzi kwa kiongozi badala Taifa? Tumekuwa nchi ya namna gani sisi?
Kazi unayo Mwaka huu na ndio kwanza mwezi wa Tatu hata ukifika wa kumi nakuhakikishia unaenda kuwa Chizi makopo yanakuhusu mate.
 
Uchawa tumshukuru muasisi wa uchawa asa the kwa kuupenda uchawa oyeee,eeee
 
Sikufurahishwa na anguko la taifa lile lakini ilibidi nitazame anguko la taifa lile
 
Mkuu wewe save hizi picha ni swala la muda tuu, chuma huliwa na kitu, mtu huzali na kufa vile vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…