Nyerere aliwahi kuwa rais mwenye kufanya mapinduzi, mabadiliko na maendeleo kwa watanzania kwa wakati huo Tanzania ikiwa nchi changa yenye changamoto kwenye kila idara ila hakuwahi kutukuzwa kupitiliza kama rais wa sasa.
Tanzania tuna matatizo mengi kwa sasa.
1. Uzalendo umepungua kwa asilimia 90% kuanzia kwa viongozi mpaka kwa wananchi, hii inatokana na mwenendo wa uongozi uliopo, wananchi hawaoni moyo na matendo ya kizalendo kutoka kwa viongozi wao.
2. Kujitambua sisi kama nchi na kutambua muelekeo wa taifa letu imekuwa ni changamo kubwa hatutambui tunajitoaje kwenye umasikini, ujinga, uvivu, na maradhi.
3. Tumechoka na kukata tamaa, tumepoteza kitu muhimu ndani ya mioyo yetu sisi watanzania hatuna TUMAINI, kwa sababu, hatuioni nuru ya mabadiliko na maendeleo katika macho yetu, masikio ndiyo yamejaa jina la mama, masikio yanasikia promotions ya jina la mama kila kukicha ila nchi haina nuru iletayo tumaini tena.
4. Hatuna kitu cha kujivunia wala kujinadi nacho kwa nchi zingine na kutufanya watanzania kusimama kifua mbele na kujiamini kwa upana na ushupavu kuwa sisi ni watanzania tunajivunia kuwa watanzania, kila kitu kimekuwa kibaya.