Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
nadhani kinachokuumiza zaidi ni gubu na makasiriko right?Watu wanawaza kuwalamba miguu Viongozi na kuwa machawa wao ili waendelee kula. Hawawazi maslahi mapana na Tanzania na kesho njema ya Taifa letu.
Viongozi badala ya kuelekeza fedha zikawahudumie Wananchi ikiwemo kununua madawa, kuweka miondombinu bora ya elimu kwa watoto wetu inayohudumiwa na kutunzwa vizuri muda wote, wao wanazielekeza kwenye ku print kofia, t shirt na kanga za kumuabudu Kiongozi ili aendelee kuwateua na waendelee kula.
Hakuna anayeumiza kichwa kuwaza Dunia ilipo na changamoto zake Tanzania tuweje na tufanye nini ili tuwe nchi imara inayojitegemea na kutegemewa na wengine kiuchumi na kila kitu.
Kwa sasa ni kama wote hatuwazi, hatufikirii, tumepigwa upofu na wala hatuiangalii Tanzania ya kesho na Watoto wake inapaswa kuwaje.
Naionea huruma Tanzania. Naumia kuishi nyakati ambazo Tanzania inakufa huku naiona.
View attachment 3254495View attachment 3254496View attachment 3254497View attachment 3254498View attachment 3254499View attachment 3254500View attachment 3254501View attachment 3254502View attachment 3254503View attachment 3254504View attachment 3254505
hua inaangamiza watu vibaya hiyo kitu, ni vizur ukaanza kupunguza gentleman kwasabb mapenzi ya wananchi kwa Dr Samia Suluhu Hassan ni ya kiwango cha juu mno kwa waTanzania.
kuna kikundi cha vibaka na matapeli wa kisiasa wanawatapeli wananchi pesa kidigitali,
Je, hao pia wanakuumiza sana gentleman?
Unaumia sehemu gani zaidi kwa mfano?🐒