Inasikitisha sana. Kwanini Azam Media inaendekeza udini namna hii?

Inasikitisha sana. Kwanini Azam Media inaendekeza udini namna hii?

Desprospero

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
1,015
Reaction score
2,493
Kwa mara ya kwanza nilipoomba kazi ndani ya Azam Media (Tv na Radio) watu wengi waliniambia si rahisi kupata kazi katika makampuni ya Bakhresa kama wewe si Muislamu. Walioomba kazi hiyo tulikuwa Wakristo 8 na Waislamu 4. Lakini nafasi zilikuwa 13. Cha ajabu kwa Wakristo alichukuliwa mtu mmoja tu lakini Waislamu wote walichukuliwa hata ambao hawakuwa na sifa stahiki.

Hatua hii ilinisukuma na wenzangu kufanya uchunguzi wa kitaaluma. Loh! Yani asilimia 79.4 ya wafanyakazi katika chombo hiki cha habari ni Waislamu. Ni asilimia 19.6 tu ndio wa dini na madhehebu mengine.

My take: Hata kama wewe ni wa dini fulani lakini kama umewekeza katika jamii mchanganyiko si busara kuwabagua wafanyakazi wako kwa udini, ukabila, jinsia nakadhalika maana unaowauzia bidhaa zako si wa Imani yako pekee. Bakhresa lichunguze hili isije ikawa hata wewe hujui ila ni maamuzi ya wakubwa uliowaweka humu ndani.
 
Ukiona mwajiri anambagua mtu kutokana na dini yake basi elimu haijamsaidia ,Biashara nyingi zinashindwa kuendelea kwa haraka kutokana na kuendekeza undugu , ukabila na udini hii inachangia wafanyakazi kufika kazini kwa kutimiza ratiba tu na kusubiria mshahara mwisho wa mwezi , no creativity , very poor competence kabisa hili ni tatizo ambalo lipo sana Afrika sio Tz tu.
 
Back
Top Bottom