Inasikitisha sana mji mzuri kama huu wa Walebanoni kufanywa magofu Kama Gaza kwa kuunga mkono magaidi wa Hizbola

Inasikitisha sana mji mzuri kama huu wa Walebanoni kufanywa magofu Kama Gaza kwa kuunga mkono magaidi wa Hizbola

Afghanistan chini ya Waislamu wa Taliban wenye misimamo mikali na mahala salama ya kuishi?
Aloenda kuiharibu Afghanistan nani Afghanistan ilikua mahala salama kuishi kabla muuaji marekani hajaenda kuleta ujinga wake
 
Naomba sababu za msingi za Hizbola kushambulia Israel ikiwa kwenye nchi ya Lebanon
Huku ikijua wazi madhara yake kwa wananchi walebanon
Ukitaka kuelewa mambo rudi nyuma zaidi usiyaangalie kijuujuu. Sababu ya Hezbollah kuundwa ni kupambana na Israel, Israel alikalia kimabavu Lebanon na Hezbollah wakawa toa kinguvu hapo Lebanon,

Je Frelimo Msumbiji, Kina Jomo kenyata, Mandela na wengineo walikua ni wajinga kupambana na wakoloni?

Hilo ni Eneo lao Hezbollah wamezaliwa Hapo, Wamekua hapo, baba zao na Babu zao wametoka hapo, Eneo wanalolipiga Haifa ni lao pia ambalo linakaliwa kimabavu na wakoloni ambao baba na Babu zao walizaliwa Poland, Ujerumani na nchi nyenginezo.

Ujinga wa Mu Africa ambaye miaka 80 iliopita alikua anatawaliwa kushangaa watu kama wao ambao wanatawaliwa, wanaonyimwa haki za kimsingi za kibinadamu kushika silaha na kupigana na watesi wao.
 
Hana mpya anatumia mass killings akidhani atawadhoofisha wapiganaji wa Islamic resistance chaajabu jamaa wanazidi kuwaua IDF na silaha zao. Hezbollah na Hamas Hawaui raia na kama wangetaka kufanya hivyo wayahudi wengi wangekua marehemu saahizi
Oct 7 Hamas walifanya genocide ya watu zaidi ya 1200 ndani ya Israel, then Oct 8 2023 Hezbollah wanaanza kurusha makombora kuwaunga mkono Hamas, ulitegemea Israel wapige magoti mbele ya magaidi,?!
 
Wakati Hamas waliposhambulia Israel na kuua raia wa Israel mamia ya wanawake na vitendo viovu , hizbola ilikemea Hamas ?

Kwanini hizbola haikwenda front kule Gaza kuisaidaia Hamas badala ya uhuni wanofanya Lebononi kusabisha Lebanon kuwa Gaza nyingine ?
Kabla ya hio Oct 07, unafahamu kilichotokea August 23, juu wa waisrael kuwakanyaga na vifaru wakulima wa kipalestina?.
 
Oct 7 Hamas walifanya genocide ya watu zaidi ya 1200 ndani ya Israel, then Oct 8 2023 Hezbollah wanaanza kurusha makombora kuwaunga mkono Hamas, ulitegemea Israel wapige magoti mbele ya magaidi,?!
Na August 23,ya kabla ya Oct 7 waisrael waliwafanya nini wapalestine?.
 
Mimi nakubaliana ya kua Palestine inaonewa. Lakini swali kwa hamas na hezebola wapo na capacity ya kupigana na israel kwa sasa? Kwanini wasinge develop kwanza capacity hata kwa miaka 30 ndo waje kulipa kisasi au kuikomboa ardhi yao?

Hii ya kurusha viroketi uchara Israel na wanajua majibu ya Israel ni kuonea raia wao wenyewe.

Walichofanya Hamas October 7, walitegemea majibu yake yangekuaje, sasa gaza yote ni magofu. Wamepata nini? Na Dunia ilivyo na unafiki Israel sio tu imeachwa ifanye genocide inapewa fedha na silaha pia. Poor Palestine...
Hamas hawakukurupuka walijua haya yata tokea tu hamas waliona kungojea miaka hio uloisema ingewafanya israhell wawe karibu zaidi na mataifa vibaraka ya kiarabu yakiongozwa na Saudia na khatimae kadhia ya Palestine kupotezewa ila kwasasa kadhia ya palestina inaongelewa dunia nzima na hakuna muarabu ataanzisha uhusiano na wazayuni kwasasa kadhia ni Palestine tuuu
 
Ni ili waonewe huruma wakati ni wachokozi halafu washari ilhali kupambana hawawezi.Wanajibebesha maiti za watoto na kupanua midomo hadi inagusana na masikio huku wanajiliza hadharani.😂
 

Attachments

  • IMG_4312.jpeg
    IMG_4312.jpeg
    1.1 MB · Views: 1
Mkiambiwa hamuna akili mnasema mnatukanwa umoja wa mataifa upi uloitambua hamas na hizbullah kama makundi ya kigaidi wazayuni tokea waseme hamas wanajificha nyuma ya raia washaua raia wangapi hamas wameifuta au unadhania kubomoa majengo ndio ushindi hamas atapambana na mazayuni mpaka mwisho na watatema tu bungo kaeneo kama kismayo wanahangaika nacho mwaka wapili sasa
Mkuu; pitia Taarifa mbalimbali za UN au Google usome orodha ya makundi ya kigaidi katika maeneo/nchi mbalimbali duniani. Kumbuka azma ya Israeli (unaowaita wazayuni)sio ushindi bali ni kuyafuta kabisa au kuyatokomeza hayo makundi ya kigaidi. Kazi hiyo sio ndogo unaanza leo unamaliza kesho-Hapana; tena ujue kuna gharama kubwa mali na Uhai kuikamilisha kazi hiyo.
 
Unavhokisema ni ukweli ila sio kwenye mgogoro huu. Hezbollah wamesimama kwenye haki. Wanawatetea binadamu wenzao wanaouliwa kila kukicha kama sisimizi tena kikatili.

Hakuna binadamu mwenye akili anaweza kuuwa binadamu wenzake kama Israel. Juu ya yote, anawamyima wapalestina hata chakula, maji na dawa. Analipua hadi hospitali, kambi za wahanga wa vita, shule za watoto wa primary, yani ni unyama uliokithiri.

Hata kama ingekuwa Kenya, Tanzania tungeyatimba kama Lebanon maana hatuwezi kamwe kumuona jirani yetu anauliwa bila huruma kama Israel wanavyowafanyia wapalestina. I stand with Lebanon despite the disastrous outcome
Hezbollah wameifanya hii ni vita ya kidini hivyo wana haki ya kuingilia kati. Hali hii ndio imesababisha Israel awakaange vilivyo. Hezbollah inakaribia kukata moto.
 
Ifike mahali wakataliwe na Kila jamii na Dini zote wanasababisha miji mizuri Kama kuharibiwa

Labda MTU mwenye Sababu zenye akili za Hizbola kushambulia Israel azieleze hapa

Pia mwenye sababu za msingi za Iran kuichukia Israel na kutaka kuifuta kwenye ramani ya dunia na kumuundia vikundi vya kigaidi
Aleezea hapa

Tafauti na hapo tukubaliane na majibu ya Israel na WASHIRIKA wake ya Sasa na baadae View attachment 3139368
View attachment 3139368
Dunia nzima ipo pembeni hakuna anayejali kinachoendelea ghaza watu wanapambania uhuru kama babu zako walivyopambania uhuru wa tz
 
Hezbollah wameifanya hii ni vita ya kidini hivyo wana haki ya kuingilia kati. Hali hii ndio imesababisha Israel awakaange vilivyo. Hezbollah inakaribia kukata moto.
Israel ni mwehu tu vita vinapiganwa baina ya wanaume wawili yeye anapiga residential areas ili iweje sasa
 
Kwanza Mheshimiwa na kupa hongera sana kutumia jina la mwamba Yahya Al Sinwar huyu kiongozi Israel hawata kuja msahau, wao na mashoga zao US, UK. Germany na badhi ya mafala viongozi wa kiarabu.

Israel hawezi vita anacho weza kuvunja majumba na kufanya genocide basi.
Sinwar walimfumua kile kichwa ili kuondoa ujinga mwingi uliokua umejaa huko.
 
Israel ni mwehu tu vita vinapiganwa baina ya wanaume wawili yeye anapiga residential areas ili iweje sasa
Kuna mali za viongozi wa Hezzbollha, mahandaki ya silaha na vitu vingine. Analenga baadhi ya maeneo sio kila mahali.
 
Mkuu; pitia Taarifa mbalimbali za UN au Google usome orodha ya makundi ya kigaidi katika maeneo/nchi mbalimbali duniani. Kumbuka azma ya Israeli (unaowaita wazayuni)sio ushindi bali ni kuyafuta kabisa au kuyatokomeza hayo makundi ya kigaidi. Kazi hiyo sio ndogo unaanza leo unamaliza kesho-Hapana; tena ujue kuna gharama kubwa mali na Uhai kuikamilisha kazi hiyo.
Mkiambiwa hamjitambui mtaona kama mnatukanwa leta sehemu ambayo UN wameiorodhesha hizbullah na Hamas kama makundi ya kigaidi pia kama nchi unavyosema basi hata mandela alikua anaitwa gaidi mwisho suala linajulikana kama wanataka waikalie Ghaza ila hilo wasahau dunia iliishavuka huko tuupe muda nafasi yake utaamua tuuuu
 
Back
Top Bottom