Tunaweza kuona ni rahisi sana lakini hii inachoma kama pasi,imagine huyo dada amemvumilia mwenzio mpaka wamejenga familia,may be na watoto wamepata,ndugu wanamjua huyo mwanaume kuwa ndo ameoa Binti Yao,then gafla anamuacha anaoa mwingine,,like seriously? Inauma aisee,omba yasikukute. Na hizi mada za single mother wanavyopondwa then umevumilia mtu mwisho wa siku anakuacha ,inaumiza sana
Ni mentality na utamaduni wa kijinga sana kumpa mtu mwingine control ya maisha yako.
Unaandika habari ya kumvumilia mpaka wamepata watoto. Hutakiwi kuvumilia ujinga. Unatakiwa ukiona ujinga usioutaka unamkata mtu mapema msije kupata watoto mkaleta complications zaidi.
Yani maisha yako wewe unayaacha yawe defined na matendo ya mtu mwingine. Kwa nini?
Unamkubali mtu ambaye hujamchunguza vizuri, akikuacha hapo kosa ni lako, si lake. Kila mtu ana haki ya kuacha. Ukilalamika kuachwa, wewe ndiye mwenye makosa. Unalazimisha mtu asiyekupenda akupende. Mapenzi hayalazimishwi.
Mbona sisi wengine tumekutana na wanawake ambao tumewaona hawa ni majanga, tukawakata mapema sana, na hilo limetusaidia?
Mbona sisi wengine tumekataliwa na wanawake ambao hawajatukubaki, na hilo tumelielewa na tumelikubali, bila kisasi?
Kwa nini utake kumdhuru mtu kwa sababu kakuacha? Umeshindwa kutafuta mwingine? Mabilioni yote haya ya watu, umeshindwa kutafuta mwingine?
Hapo ndipo unakutana na ujinga wa "ndugu wanamjua". Maana yake mtu anaishi maisha ya ku act anaogopa ataonekanaje kwa ndugu.
Kwa nini watu wanataka kujifanya wao wako special sana, hawataki kukataliwa, wakikataliwa wanataka kuleta vurugu na visasi?
Kumuacha mtu ni haki ya kibinadamu. Hata kama mmekaa naye miaka mia na kupata vitukuu.
Kwa nini mtu analazinisha mapenzi na kutishia kumuumiza mtu nwingine kwa sababu kaachwa?
Huu si ugonjwa wa akili huu?
Ukiachqa, una move on tu.
Ukianza habari za kisasi, unampa point yule aliyekuacha kwamba alikuwa sawa kukuacha.
Kwamba wewe una matatizo ya akili, you are an unstable psycho ambaye hawezi kukubali kuachwa.
Na hiyo ni sababu tosha ya kukuacha.