Inauma sana na haivumiliki

Ebu pitia hapa huenda ukaponya moyo wako

 
Haya matukio watanyaji wengi ni wanawake mwanaume akitetereka kiuchumi.
Kwà wanaume kumwacha asiyeomba hela ni ngumu sana. Wanaume tunatafuta hela ili msituache ila siyo tuwaache.
 
Kwa nini unataka kulazimisha mapenzi?

Kwa nini unataka kumdhuru mtu kwa sababu kaamua hakupendi tena?

Wewe ni mbaya hivyo kwamba huwezi kupata mwingine?

Yani huyo peke yake ndiye alikuwa mwokozi wako dunia nzima?
Tunaweza kuona ni rahisi sana lakini hii inachoma kama pasi,imagine huyo dada amemvumilia mwenzio mpaka wamejenga familia,may be na watoto wamepata,ndugu wanamjua huyo mwanaume kuwa ndo ameoa Binti Yao,then gafla anamuacha anaoa mwingine,,like seriously? Inauma aisee,omba yasikukute. Na hizi mada za single mother wanavyopondwa then umevumilia mtu mwisho wa siku anakuacha ,inaumiza sana
 
Pole Sana mkuu,Muombe Mungu akupatie wa kufanana naye[emoji120]
 
Ni mentality na utamaduni wa kijinga sana kumpa mtu mwingine control ya maisha yako.

Unaandika habari ya kumvumilia mpaka wamepata watoto. Hutakiwi kuvumilia ujinga. Unatakiwa ukiona ujinga usioutaka unamkata mtu mapema msije kupata watoto mkaleta complications zaidi.

Yani maisha yako wewe unayaacha yawe defined na matendo ya mtu mwingine. Kwa nini?

Unamkubali mtu ambaye hujamchunguza vizuri, akikuacha hapo kosa ni lako, si lake. Kila mtu ana haki ya kuacha. Ukilalamika kuachwa, wewe ndiye mwenye makosa. Unalazimisha mtu asiyekupenda akupende. Mapenzi hayalazimishwi.

Mbona sisi wengine tumekutana na wanawake ambao tumewaona hawa ni majanga, tukawakata mapema sana, na hilo limetusaidia?

Mbona sisi wengine tumekataliwa na wanawake ambao hawajatukubaki, na hilo tumelielewa na tumelikubali, bila kisasi?

Kwa nini utake kumdhuru mtu kwa sababu kakuacha? Umeshindwa kutafuta mwingine? Mabilioni yote haya ya watu, umeshindwa kutafuta mwingine?

Hapo ndipo unakutana na ujinga wa "ndugu wanamjua". Maana yake mtu anaishi maisha ya ku act anaogopa ataonekanaje kwa ndugu.

Kwa nini watu wanataka kujifanya wao wako special sana, hawataki kukataliwa, wakikataliwa wanataka kuleta vurugu na visasi?

Kumuacha mtu ni haki ya kibinadamu. Hata kama mmekaa naye miaka mia na kupata vitukuu.

Kwa nini mtu analazinisha mapenzi na kutishia kumuumiza mtu nwingine kwa sababu kaachwa?

Huu si ugonjwa wa akili huu?

Ukiachqa, una move on tu.

Ukianza habari za kisasi, unampa point yule aliyekuacha kwamba alikuwa sawa kukuacha.

Kwamba wewe una matatizo ya akili, you are an unstable psycho ambaye hawezi kukubali kuachwa.

Na hiyo ni sababu tosha ya kukuacha.
 
Daaah, alafu kadada kenyewe kazuri, Pole na siku nyingine ukisikia methali za wahenga basi uwe una amini
 
Exactly comrade
 
Wakati unamvumilia akiwa hana kitu, wewe ulikua na nini?

Sent from my SM-A235F using JamiiForums mobile app
 
Mimi nilichomuelewa hapa mtoa mada anavyosema amepotezewa muda ni zile ahadi alizokuwa akiahidiwa,mwenzie hakumuweka wazi mapema ili aendelee na mishe zake nyingine,anachoumia ni kwamba alifanywa daraja kwa mtu mwingine
 
Tupe ushuhuda kidogo
 
Aise!

Sometimes wanawake tunakuaga na maneno ya shombo sana. Then baadae tunajitilisha huruma as if tumeonewa kumbe tumesababisha wenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…