Kosa lipo hakuna ajira,viwanda vikubwa 400 vya Raisi Mwalimu Nyerere vilivyokuwa vinaajiri maelfu kwa maelfu ya wananchi vilibinafsishwa na vikaaga dunia.
Siyo tu kuajiri lakini waajiriwa walipata mafunzo mbali mbali kupitia viwanda hivyo na kupata ujuzi katika fani mbali mbali.
Mtu anasoma diploma 3,bachelor degree 4,masters 2 na Phd,yote katika mashindano ya kutafuta ajira.Muda mwingi ameutumia vyuoni na si kazini.Na kadili siku zinasonga hizi white collar job siku zake zimehasabiwa kwa mjio wa Artificial Intelligence AI.
Kauli mbio za kujiajiri kwa mapana ni kichekesho.
Kama ile pesa inayotumika kwenye miradi isiyo ya lazima wangekopeshwa wajasili mali wapatao millioni 5,nao wakatengeneza wastani wa ajira milioni 25.
Hao watu milioni 25 wataongeza chachu ya kulipa kodi na kuhudumia family zao ndio kujenga taifa la kujitegemea.