Inaumiza sana mtu ana masters degree ila hawezi hata kujilipia kodi ya chumba kimoja. Elimu ya juu imesababisha wategemezi wengi wenye umri mkubwa

Inaumiza sana mtu ana masters degree ila hawezi hata kujilipia kodi ya chumba kimoja. Elimu ya juu imesababisha wategemezi wengi wenye umri mkubwa

As long as anaweza kutia mimba inatosha kabisa... Kulipa kodi sio kipimo kilaza weee
 
Duu kweli ni janga, wengi wameishia kwenye ulevi, kamali na kuishi kwa mashemej zao[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Elimu inayoendesha MAISHA duniani kote huwa ni ELIMU ya Kujitambua ambayo huitwa "The sense of who you are"

MTU anapojitambua maana yake atajua udhaifu wake UPO wapi na uimara wake UPO wapi.

Tukija katika hoja yako ya kuwa na masters , au degree na Maisha kuwa magumu.

Kwanza elewa kuwa elimu ya Tanzania huwa inafuta ujinga Ila haiongezi maarifa yoyote ,watu unowaona wana uelewa mpana na kujitambua wapo na vitu vitatu ,malezi waliyolelewa , kusoma Sana vitabu. na kujifunza kwa WATU .


Hivyo mpaka hapo huwezi kumlaumu msomi wa degree na ukiona MTU amekwama usianze kumcheka maana elimu haimfanyi MTU afanikiwe wala asifanikiwe.


Elimu inayofanya MTU afanikiwe huwa ni Elimu ya "Kujitambua" Watu wengi hawajitambui na ili ujitambue unabidi kuwa na nidhamu na kila kitu.

Elimu sio mafanikio Ila huwa ni stepping stones ( ni mawe ambayo huwekwa kwenye njia ili watu wavuke baada ya mvua kunyesha.
 
Anachomaanisha kama huna ajira ya kumpa mwanao ni bora ukamjengea nyumba na ukampa elimu ya ufundi kuliko kutumia mamilioni kumsomesha hadi masters halafu asiweze hata kulipa chumba cha kupanga.
Kibongo Bongo unaweza soma toka vidudu mpaka Masters usilipe hata 6M katika tuitions fees.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kosa lipo hakuna ajira,viwanda vikubwa 400 vya Raisi Mwalimu Nyerere vilivyokuwa vinaajiri maelfu kwa maelfu ya wananchi vilibinafsishwa na vikaaga dunia.
Siyo tu kuajiri lakini waajiriwa walipata mafunzo mbali mbali kupitia viwanda hivyo na kupata ujuzi katika fani mbali mbali.

Mtu anasoma diploma 3,bachelor degree 4,masters 2 na Phd,yote katika mashindano ya kutafuta ajira.Muda mwingi ameutumia vyuoni na si kazini.Na kadili siku zinasonga hizi white collar job siku zake zimehasabiwa kwa mjio wa Artificial Intelligence AI.

Kauli mbio za kujiajiri kwa mapana ni kichekesho.
Kama ile pesa inayotumika kwenye miradi isiyo ya lazima wangekopeshwa wajasili mali wapatao millioni 5,nao wakatengeneza wastani wa ajira milioni 25.
Hao watu milioni 25 wataongeza chachu ya kulipa kodi na kuhudumia family zao ndio kujenga taifa la kujitegemea.
 
Back
Top Bottom