Inawezekana kipindi cha Mkapa ndio ujambazi mkubwa ulitamalaki

Tek sio tatizo.marekani wana tek ya hali ya juu lakn ujambazi na mauaji vinafanyika tu

Vinafanyika ila sio wakishamba kama huu wa kwetu .Alafu huwa wanashikwa mbona hata kama itachukua muda gani.
Kule wauwaji huwa ni wale washajitosa kiwa nao watauliwa au kukamatwa sio anafanya kosa kama hilo akiamini kuwa hatoshikwa kama huku kwetu
 
hata kipindi cha suleman kova ujambazi ulikuwepo sana tena ndo kipindi makundi mengi ya panyarod yalifanya uhalifu mwingi. Magufuli alitokomeza kabisa ule mtandao. Ukaja kuibuka tena alivoingia samia lakini naona kuko kimya sina hakika kama wamedhibitiwa au wametulia kwa muda uchaguzi upite kwanza kisha matukio yaendelee.
 
Banjoo Vs Saba Sita
Haswaaaa! Saba Sita!

Ndio maana Mimi binafsi niliposikia kwamba Askari Polisi Saba Sita ameamua kuchimba kaburi lake yeye mwenyewe angali akiwa bado yuko hai na kujiandalia maandalizi yote kabisa juu ya kifo chake wala hata sikushituka. Yuko sahihi kabisa kufanya hivyo kwa sababu anayajua mambo aliyofanya wakati akiwa Askari Polisi.
 
Kuna boda inaweza kufukuza defender, discover, Vogue au land cruiser yoyote, sema advantage yao miaka hiyo magari hayakuwa mengi hivyo jam ingekua sio kikwazo kwao tofauti na miaka hii foleni kuanzia asubuhi hadi jioni
Ndio maana nikasema mazingira yamebadilika ni kuhusu mafoleni barabarani.
Sio speed na uwezo wa gari
 
Kwa tukio la NMB Ubungo Mataa inasemekana kuna silaha ya kivita iliazimwa kutoka kambi moja wapo ya Jeshi.

Source: Kijiwe cha gahawa..
Hapana sio kijiwen ni kweli walikua wajeda kambi moja pale kurasin kuna jamaa alitoka kawa mlokole alikua anahadithia ila alikua anakanusha kuhusika lkn ukimsikiliza vizur unapata picha
 
Kikwete ndiye ambaye alianzisha Operation kali Sana ya kuwadhibiti Majambazi hapa Tanzania. Mara tu alipoingia madarakani Majambazi-papa wote kabisa walikamatwa na Jeshi la Polisi na kuhojiwa. Wengi wao walipewa onyo kali la mwisho la kutakiwa kuacha kabisa shughuli za ujambazi na kufanya kazi zao halali. Wale Majambazi-papa waliokaidi onyo hilo walikuwa eliminated kimya kimya.
But all in all, IGP Omar Mahita alikuwa miongoni mwa Watu vinara waliosaidia kustawisha Ujambazi hapa Tanzania hali iliyosababisha hata Bunge kumwita na kumhoji kuhusiana na utendaji kazi wake. Majambazi waliiteka nchi.
 
But all in all, IGP Omar Mahita alikuwa miongoni mwa Watu vinara waliosaidia kustawisha Ujambazi hapa Tanzania hali iliyosababisha hata Bunge kumwita na kumhoji kuhusiana na utendaji kazi wake. Majambazi waliiteka nchi.
 
Watu wa zamani mmeishi kwa shida sana aisee. Poleni sana.
Mnaishi kama swala porini, muda wowote mnaliwa.
 
Aise Mshana jr hii mada umeitoa wapi..umenikumbusha miaka hyo ujambazi ulishamiri sana, Tz ilikuwa kama shamba la bibi huko Kigoma-Tabora kulikuwa hakufai..Kigoma maeneo ya Kazuramimba,Msitu wa kuitafuta Kibondo ukija Kigoma mjini,kutoka Kigoma vijijin kwenda Kasulu kuna kasehem kanaitwa makonani yaani ni kama walikuwa wameshaanzisha familia hapo..ukija maeneo ya kaliwa hatari..kuna sehem nyingine Mkoa wa Songwe ukitokea Mbozi unapita njia ya kuelekea kamsamba katikati kuna msitu mkumbwa ukiwa unaingia kajiji fulani kanaitwa Ntugwa yaani walivokuwa washenzi hako kasehemu walikatunga najina kabisa eti "Bank kuu" hapo walikuwa hawakosi...ila hawa majambazi walikuwa hawafai miaka hyo.. tukio sinto kuja kulisahau nikiwa darasa la nne walimuuwa classmate wangu walienda kuvamia kwao yeye akawa wakwanza kufungua mlango wakamlima shaba ya kichwa kesho yake tunatangaziwa shuleni Rehema amefariki kwa kupigwa risasi na majambazi iliniuma saaaaana halafu alikuwa rafiki yangu.Majambazi hawafai.
 
Ujambazi ulikuwepo ila mnaposema mpaka ilifikia hatua ya vituo vya Polisi kufungwa usiku sababu yao hapo mmeongeza chumvi.
Unapoaambiwq vituo sio maana ya vituo vikubwa mkuu ni hiv vituo vidogo vidogo vya kata sio central
 
Wanaposema technology imekua ni kwamba sasa hiv mambo ya simu tu yamezuia sana uharifu yaan ukipanga tu mipango inanaswa ndo mana leo tunaona watu wanafatwq tu maofisin mwao na kuchukuliwa na kupotezwa izo ni kazi ya simu hiz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…