Kashishi yetu
JF-Expert Member
- Mar 22, 2014
- 3,509
- 3,741
Kwahiyo inatosha au haitoshi kwa mtazamo wako?
Mm ni Mhandisi by professional ngoja nijaribu kukupa roughly estimate ( ningeona ramani na plot yako ningekupa most accurate estimate)
Tofauli kwa kozi 14, msingi na septic 2500-3000
Gharama fundi mzuri yoyote 1.8 - 2M (boma tu)
Saruji mpaka plaster 100-150 bags
Nondo mm 10 pc 25 na mm 12 pc 30 (ukifunga tatu tatu)
Kokoto trip 2 (nzuri ni ile nyeusi chukua za size 20-25mm) Dar trip moja 300k mpka 400k
Mchanga trip 7-10
Kupaua ( fundi+mbao+bati gauge 30) 4-6 M itategemea aina ya bati unazohitaji so inaweza kuzidi or kupungua
Kuna gharama za maji, kuchimba shimo la choo, usafiri, rings, kukodi mbao, majukwaa, na mapipa ( itategemea na mahali ulipo)
Pia kuna gharama za milango, madirisha, plumbing,electrical installation, finishing ya floor, ceiling, na rangi hizo zitategemea na mahitaji yako mkuu. Na vitu vingne kama misumari, binding wire, mbao za 2x2 kwa ajili ya msingi wakt wa setting, plywood kma unahitaji arch wakat wa renta fundi atakuongoza idadi yake. All the best