Bila ramani hauwezi kujua matofali kiasi gani yataenda kwenye msingi na kuta. Picha haionyeshi mgawanyiko wa vyumba, sebule, vyoo na jiko. Hizo taarifa na vipimo vinasaidia sana kwenye makadirio.
Pia ubora wa mbao na bati unatofautiana. Kuna zile bati za kawaida nyeupe au za rangi lakini mwezi zimeshabadilika rangi. Pia kwenye mbao napo zinatofautiana bei.
Tufanye fundi akuezekee kwa 1M, ajenge kwa 2M, hapo ni ufundi tu. Njoo manunuzi ya bati, mbao na misumari.
Turejee kwenye nondo za mkanda wa chini kwenye msingi na lintel. Hapa inategemea unaweka nondo mbili, tatu au nne. Bei ya nondo sasa hivi imechangamka, tukadirie atatumia za 800,000/- weka gharama za mchanga, kokoto, mbao za kukodi, ringi, wire, kuchimba msingi na maji.
Turudi kwenye cement na tofali. Ikitumia tofali za 3 M ikijumuisha za msingi na kuta. Cement ya kujengea na plasta ( hapo kwenye ufundi hatukupigia hesabu plasta).
Kuna vitu vidogo vidogo sijui mirunda, mbao za kukodi hua vinaibuka kati kati na haukupigia hesabu.
Hadi hapo itoshe tu kusema akitaka inaweza kutosha hiyo 14M ila ya ubora gani?
Fundi mwanzoni anaweza kukupa makadirio ya chini ili muanze kazi, anajua ukishaingia lazima uimalize kazi. Anajua hata vitu vikiisha hauwezi kusimamisha ujenzi.
Ushauri wangu.
Ainisha gharama za kuchimba msingi, tofali za msingi, ujenzi, nondo, mchanga na kokoto hadi kwenye mkanda.
Njoo kwenye boma. Pata idadi ya tofali, lintel (kokoto, nondo, mchanga, ringi, nyaya na ufundi bila kusahau maji)
Kisha pata gharama ya mbao, misumari, bati na gharama za ufundi.
Malizia kwa kupata makadirio ya plaster ila kumbuka ni vizuri kupiga plasta ukiwa umeshaweka bomba za umeme, maji na blandering.
Jumlisha hizo gharama zote ukiona hazijavuka 13 M (Hakikisha unabakiwa na hata 1 M ya dharura), anza ujenzi kwa makubaliano ya kuandikishana kabisa kwamba fundi acheze na kufanya mbwembwe zote ndani ya bajeti.
Tena ukiweza, pata hayo makadirio kwa mafundi hata watatu, itakusaidia kupata uhalisia.
Kila la kheri mkuu.