Inawezekana kujenga nyumba hii kwa millioni 14

Kwahiyo inatosha au haitoshi kwa mtazamo wako?
 
Haitoshi ilo bati na mbao kununua ni 4m bado gharama ya fundi
 
Hkama ilivyo? Hadi ripu hiyo
Haitoshi
Labda kama tofali unatengeneza mwenyewe
Inatosha, abadilishe tuu hilo paa maana ni zaidi ya kula bati 100 na mbao nyingii halina faida yoyote.
 
Sio matofali kwanza
Mabati na mbao vipo kibao na bei nzuri tuu.... Nunua tofali 1500 kwanza, mchanga tripu 4, simenti mifuko 50, kokoto tripu mbili, vuta bomba la maji hapo site, zungusha fensi ya nguzo za miti na waya na geti la mabati used then anza kazi fasta mwanangu...
 
Kwa jinsi ujenzi na gharama ya vifaa vilivyopanda bei nakushauri anza kujengea kwenye karatasi kwa uhalisia wa gharama za material bila hvyo hiyo ramani kama inazidi vyumba viwili jiandae kuishia njiani
 
Wazi zuri
 
Kwa jinsi ujenzi na gharama ya vifaa vilivyopanda bei nakushauri anza kujengea kwenye karatasi kwa uhalisia wa gharama za material bila hvyo hiyo ramani kama inazidi vyumba viwili jiandae kuishia njiani
Vyumba viwili na sebule
 
Kwa hiyo ramani inavyoonekana bati si chini ya 100 hapo tayari 4m imeenda Mbao 1.5m tofali 2.5-3m cemen 900k kokoto inategemeana ila si chini ya 150k nondo 7-800k fundi wa kujenga 1m fundi kupaua 800k weka na mchanga madirisha na milango 1.5m weka vitu vidgo vidgo ukiona umebakiza 3M pembeni nje ya hiyo hesabu kajenge mwanangu wa faida [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji1666]
 
Bati za kawaida 100 haifiki million mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…