Inawezekana kweli Lissu amewatangulia Wanasheria wa CCM kwa miaka mia moja mbele

Mijadala kama hii inakuzidi kimo ndugu yangu, kaa mbali nayo. Kinachoongelewa hapa ni uhaini, tendo ambalo nina hakika hata ungepewa miaka kumi huwezi kuelewa ni tendo gani!
Acha porojo.. elekeza hapa ikiwa Lissu Kaivua nguo mihimili ya serikali then what!
 
Yeye yuko upande wa wale wanaoomba na watakaoshangilia nikipatikana na hatia”

Kwahiyo amesema hayupo tayari kuja kutoa ushahidi kwa niaba yangu.

Nimemuelewa Waheshimiwa Majaji kama hayuko tayari siwezi kumlazimisha kutoa ushahidi ambao hataki kuutoa.

Waheshimiwa Majaji Kingai ameniambia kitu kingine kuhusiana na mashahidi wengine wawili IGP Camillius Wambura na CDF Jacob Mkunda, amesema vilevile hata wao watakaporejea nchini na kupata wito wa Mahakama msimamo wao utakuwa ni huo huo kwamba na wao hawatakuwa tayari kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi kwasababu ile ile kuwa wako upande wa wale wanaoombea na watakaoshangilia nikipatikana na hatia.
"Kuwa upande" na "kuwa sehemu" ni vitu viwili tofauti.
 
Acha porojo.. elekeza hapa ikiwa Lissu Kailua nguo minimalist then what!
Nilikuasa huu mjadala unakuzidi kimo kaa nao mbali. Ona sasa. hapo juu umeandika nini? Leo utalala njaa hata hiyo buku ya Lumumba huioni. Kwa kuanzia nakuweka kwenye ignore wewe na hizo takataka unazofuatana nazo. JF kweli imekuwa kokoro inazoa tu...kwaheri!
 
Bora ukimbie tu mana hujiwezi na huwezi kuhimili mawazo kinzani
 
Lissu Yuko mbele ya Muda dhidi ya CCM na wanasheria wote wa CCM.
Kwa kifupi watu wengi hawakuelewa,hata Mimi sikumuelewa aliposema mashahidi wake ni RAIS Samia,CDF,IGP,DGTISS na Kingai.
Kwa kifupi alipowataja Hawa kua ndio mashahidi wake alikua amelenga mitego miwili kwa ajili ya kupiga TKO.
Leo ndio nimegundua baada ya kupelekea kumaliza kesi kiaina na kirahisi sana.

Mtego wa kwanza alijua hata wakija hawana ushahidi wa kweli kua alitaka kupindua nchi yeye peke yake,hivyo atawashinda.

Mtego wa pili alikua fika hawatakuja kwa kua hawana ushahidi kua lisu alipanga njama peke yake za kuangusha serikali hivyo atashinda.

Kama mtakumbuka mwanzoni alimuuliza mtu je mpango wangu wa uhaini Mkuu wa Usalama wa Taifa anajua?
Je CDF anajua ,?
Je IGP anajua ,?
Mlipeleka taarifa kwa Wakuu hao?
Majibu yakawa hapana.
Mtu akaulizwa,Sasa tukio kubwa kama hili watu Wazito kama Hawa hawakua na taarifa,mko serious kweli nyinyi?

Leo Kingai kasema siwezi kua shahidi wako na nitafurahi ukikutwa na hatia na wenzangu Wana msimamo kama wangu.

Kwamba watafurahi akikutwa ana hatia,kwa hiyo hata Kingai Hana uhakika kama Lisu ana hatia.!

Sasa kama hawana uhakika kama atakutwa na hatia walimfungulia mashitaka ya uhaini kwa ushahidi upi?

Aisee kesi imeishia hapo,labda endeleeni kupoteza nguvu na pesa TU.

Kama kweli walikua wanataka kumtia hatiani Lisu na kama kweli walikua Wana ushahidi ,Hawa Wakuu wanne ndio wangemmaliza Lisu.

Maana taarifa zote za ulinzi na usalama wa nchi za Kila siku zinapitia mezani kwao,haijalishi Lisu ana maswali magumu na ya kudhalilisha kiasi Gani,kama Wangekua na ushahidi ,wangemkaanga TU.

Wangejitia wababe kwamba waje wamkaange Lisu Kwa ushahidi wa uongo,Dunia ingeingia kwenye rekodi ya Wakuu wanne wa Vyombo vya Dola kua waongo zaidi duniani.

Jamani,kutetea uongo ni ngumu sana.

Iko hivi,kesi kama ya akina Hatty Mack Ghee(Hatibu Ghandi),Rugangira,Ngaiza,Eugin Maganga,Comando Taminu na Wenzao hata angeitwa Nyerere,Kawawa na wenzao waende Mahakamani wangeenda kwa sababu kulikua Kuna ushahidi usio na chembe ya mashaka.

Nchi inawezaje kuangushwa na mtu mmoja?
Yaani mhaini mmoja TU,aliataka kupindua nchi.
Halina ubishi!
 
Je umejiuliza kwa nini Kingai alikuwa na ujasiri wa kufika ndani ya mahakama lakini akakosa uthubutu ya kuwakabili majaji?
Kwanini Lissu hakufungua shauri kumlazimisha Kingai atoe ushahidi?...
 
Kama hadi maneno aliyosema mshtakiwa hujayaelewa, mimi sina hoja ya kukwambia ukaelewa
Suala siyo kuelewa. Ukinukuhu maneno ya mtu inabidi uyatumie maneno yale yale aliyotumia yeye. Ukibadili neno au maneno yake, hiyo siyo tena nukuhu bali unakuwa unamlisha maneno kama wewe ulivyokuwa unamshutumu huyo mwenzio.

Kibaya zaidi, kuna hatari ya kubadili maana ya alichokisema kama nilivyokuonyesha.
 
Lissu Yuko mbele ya Muda dhidi ya CCM na wanasheria wote wa CCM.
Kwa kifupi watu wengi hawakuelewa,hata Mimi sikumuelewa aliposema mashahidi wake ni RAIS Samia,CDF,IGP,DGTISS na Kingai.
Kwa kifupi alipowataja Hawa kua ndio mashahidi wake alikua amelenga mitego miwili kwa ajili ya kupiga TKO.
Leo ndio nimegundua baada ya kupelekea kumaliza kesi kiaina na kirahisi sana.

Mtego wa kwanza alijua hata wakija hawana ushahidi wa kweli kua alitaka kupindua nchi yeye peke yake,hivyo atawashinda.

Mtego wa pili alikua fika hawatakuja kwa kua hawana ushahidi kua lisu alipanga njama peke yake za kuangusha serikali hivyo atashinda.

Kama mtakumbuka mwanzoni alimuuliza mtu je mpango wangu wa uhaini Mkuu wa Usalama wa Taifa anajua?
Je CDF anajua ,?
Je IGP anajua ,?
Mlipeleka taarifa kwa Wakuu hao?
Majibu yakawa hapana.
Mtu akaulizwa,Sasa tukio kubwa kama hili watu Wazito kama Hawa hawakua na taarifa,mko serious kweli nyinyi?

Leo Kingai kasema siwezi kua shahidi wako na nitafurahi ukikutwa na hatia na wenzangu Wana msimamo kama wangu.

Kwamba watafurahi akikutwa ana hatia,kwa hiyo hata Kingai Hana uhakika kama Lisu ana hatia.!

Sasa kama hawana uhakika kama atakutwa na hatia walimfungulia mashitaka ya uhaini kwa ushahidi upi?

Aisee kesi imeishia hapo,labda endeleeni kupoteza nguvu na pesa TU.

Kama kweli walikua wanataka kumtia hatiani Lisu na kama kweli walikua Wana ushahidi ,Hawa Wakuu wanne ndio wangemmaliza Lisu.

Maana taarifa zote za ulinzi na usalama wa nchi za Kila siku zinapitia mezani kwao,haijalishi Lisu ana maswali magumu na ya kudhalilisha kiasi Gani,kama Wangekua na ushahidi ,wangemkaanga TU.

Wangejitia wababe kwamba waje wamkaange Lisu Kwa ushahidi wa uongo,Dunia ingeingia kwenye rekodi ya Wakuu wanne wa Vyombo vya Dola kua waongo zaidi duniani.

Jamani,kutetea uongo ni ngumu sana.

Iko hivi,kesi kama ya akina Hatty Mack Ghee(Hatibu Ghandi),Rugangira,Ngaiza,Eugin Maganga,Comando Taminu na Wenzao hata angeitwa Nyerere,Kawawa na wenzao waende Mahakamani wangeenda kwa sababu kulikua Kuna ushahidi usio na chembe ya mashaka.

Nchi inawezaje kuangushwa na mtu mmoja?
Yaani mhaini mmoja TU,aliataka kupindua nchi.
Sijasoma hata uzi ila naunga mkono kwa aslimia 50%
 
Suala siyo kuelewa. Ukinukuhu maneno ya mtu inabidi uyatumie maneno yale yale aliyotumia yeye. Ukibadili neno au maneno yake, hiyo siyo tena nukuhu bali unakuwa unamlisha maneno kama wewe ulivyokuwa unamshutumu huyo mwenzio.

Kibaya zaidi, kuna hatari ya kubadili maana ya alichokisema kama nilivyokuonyesha.
Sawa
 
Endeleeni kumpamba huku mkiwa magetoni kwenu mwenzenu yupo gerezani

Lissu hahitaji kupambwa anahitaji kuungwa juhudi kwa vitendo hayo mapambo yenu hayamsaidii chochote
Gereza ni kama hospitali TU halina watu maalumu wa kuingia gerezani,kama ilivyo kwa hospitali

Unaweza kufungwa kwa kumgonga mwanafunzi akivuka Barbara wakati wewe ukienda kazini.
Amefungwa Bashir Al Asad wa aliekua RAIS wa Sudani,alifungwa Charles Taylor,alifungwa Slobodan Milosevic walieokua ma Rais wa Liberia na Serbia.
MAGEREZA na hospitali yamejengwa kwa ajili ya wanadamu.
 
Lissu Yuko mbele ya Muda dhidi ya CCM na wanasheria wote wa CCM.
Kwa kifupi watu wengi hawakuelewa,hata Mimi sikumuelewa aliposema mashahidi wake ni RAIS Samia,CDF,IGP,DGTISS na Kingai.
Kwa kifupi alipowataja Hawa kua ndio mashahidi wake alikua amelenga mitego miwili kwa ajili ya kupiga TKO.
Leo ndio nimegundua baada ya kupelekea kumaliza kesi kiaina na kirahisi sana.

Mtego wa kwanza alijua hata wakija hawana ushahidi wa kweli kua alitaka kupindua nchi yeye peke yake,hivyo atawashinda.

Mtego wa pili alikua fika hawatakuja kwa kua hawana ushahidi kua lisu alipanga njama peke yake za kuangusha serikali hivyo atashinda.

Kama mtakumbuka mwanzoni alimuuliza mtu je mpango wangu wa uhaini Mkuu wa Usalama wa Taifa anajua?
Je CDF anajua ,?
Je IGP anajua ,?
Mlipeleka taarifa kwa Wakuu hao?
Majibu yakawa hapana.
Mtu akaulizwa,Sasa tukio kubwa kama hili watu Wazito kama Hawa hawakua na taarifa,mko serious kweli nyinyi?

Leo Kingai kasema siwezi kua shahidi wako na nitafurahi ukikutwa na hatia na wenzangu Wana msimamo kama wangu.

Kwamba watafurahi akikutwa ana hatia,kwa hiyo hata Kingai Hana uhakika kama Lisu ana hatia.!

Sasa kama hawana uhakika kama atakutwa na hatia walimfungulia mashitaka ya uhaini kwa ushahidi upi?

Aisee kesi imeishia hapo,labda endeleeni kupoteza nguvu na pesa TU.

Kama kweli walikua wanataka kumtia hatiani Lisu na kama kweli walikua Wana ushahidi ,Hawa Wakuu wanne ndio wangemmaliza Lisu.

Maana taarifa zote za ulinzi na usalama wa nchi za Kila siku zinapitia mezani kwao,haijalishi Lisu ana maswali magumu na ya kudhalilisha kiasi Gani,kama Wangekua na ushahidi ,wangemkaanga TU.

Wangejitia wababe kwamba waje wamkaange Lisu Kwa ushahidi wa uongo,Dunia ingeingia kwenye rekodi ya Wakuu wanne wa Vyombo vya Dola kua waongo zaidi duniani.

Jamani,kutetea uongo ni ngumu sana.

Iko hivi,kesi kama ya akina Hatty Mack Ghee(Hatibu Ghandi),Rugangira,Ngaiza,Eugin Maganga,Comando Taminu na Wenzao hata angeitwa Nyerere,Kawawa na wenzao waende Mahakamani wangeenda kwa sababu kulikua Kuna ushahidi usio na chembe ya mashaka.

Nchi inawezaje kuangushwa na mtu mmoja?
Yaani mhaini mmoja TU,aliataka kupindua nchi.
Dogo, tunza haya mawazo yako. Hukumu ni tarehe 25. Akichomoka uulete tena. Ila akihukumiwa kunyongwa hadi kufa ujue wewe ni nyumbu tu.
 
Ila CHADEMA mna kelele mitandaoni!
Haya kawazidi kwa miaka 100 then what!?
Ila CCM huwa ni wajinga sana,ndio maana Wana CCM unaweza ukampa kofia na fulana imeandikwa chagua CCM ili akupigie kura na akakupigia hata kama hutamletea maendeleo.

Unachodhihaki ni kwamba Bado Lisu Yuko gerezani licha ya kuwazidi akili mawakili na CCM.
Kwa akili zako unaona ni sawa TU mmoja ya Mihimili ya Dola kuiweka mfukoni Mihimili mingine miwili.
Ukiona nchi yoyote isiyoheshimu MAHAKAMA ujue nchi hiyo imekufa,kumbuka MAHAKAMA ni Chombo kitakatifu.
Kama hakuna MAHAKAMA huru maana yake hakuna utawala Bora.
Na nchi isiyo na utawala Bora ni nchi ya hovyo na isisyo ya kistaarabu.
Ila wewe mwana CCM huwezi kuelewa umuhimu wa utawala unaofuata haki.
Kumbuka bila haki hakuna amani.
Huko tuendako Kuna dalili mbaya Kwa watawala wasiofata haki hapa nchini.
Ila wewe Kwa sababu ni kipofu endelea kujivunia mnachomfanyia Lisu.
 
Hii kesi siifatiliagi sana kwa upande wa kisheria na kikatiba maana sidhani kabisa kama iko huko. Huu nauona ni mchezo unaochezeshwa na siwezi kufurahia matokeo yoyote maana sioni kama ni uhalisia. Zaidi nalaani tu uonevu anaofanyiwa Toto
 
Dogo, tunza haya mawazo yako. Hukumu ni tarehe 25. Akichomoka uulete tena. Ila akihukumiwa kunyongwa hadi kufa ujue wewe ni nyumbu tu.
Unajua wewe kijana ni mjinga,unadhani sisi hatujui hata aina ya hukumu inayoweza kumpata Lisu?
Kwa MAHAKAMA ya Tanzania hukumu inapangwa ikulu sio mahakamani.
Tuna uzoefu na kesi za namna hii toka zama za Mtikila.
Mtikila alikua anaishinda serikali Kwa KESI zote lkn haki yake alikua hapewi.
Nyinyi mhukumuni Lisu mnavyoweza na sisi wananchi tutapima.
 
Basi naiomba Ikulu na safari hii kwa Lissu wasifanye makosa!
 
Ila CCM huwa ni wajinga sana,ndio maana Wana CCM unaweza ukampa kofia na fulana imeandikwa chagua CCM ili akupigie kura na akakupigia hata kama hutamletea maendeleo.

Unachodhihaki ni kwamba Bado Lisu Yuko gerezani licha ya kuwazidi akili mawakili na CCM.
Kwa akili zako unaona ni sawa TU mmoja ya Mihimili ya Dola kuiweka mfukoni Mihimili mingine miwili.
Ukiona nchi yoyote isiyoheshimu MAHAKAMA ujue nchi hiyo imekufa,kumbuka MAHAKAMA ni Chombo kitakatifu.
Kama hakuna MAHAKAMA huru maana yake hakuna utawala Bora.
Na nchi isiyo na utawala Bora ni nchi ya hovyo na isisyo ya kistaarabu.
Ila wewe mwana CCM huwezi kuelewa umuhimu wa utawala unaofuata haki.
Kumbuka bila haki hakuna amani.
Huko tuendako Kuna dalili mbaya Kwa watawala wasiofata haki hapa nchini.
Ila wewe Kwa sababu ni kipofu endelea kujivunia mnachomfanyia Lisu.
Sawa, Lissu ana akili kuliko wanaCCM wote, ndio nini sasa? What next!
 
Kwanini Lissu hakufungua shauri kumlazimisha Kingai atoe ushahidi?...
Kwa akili za kawaida angeweza kufanya hivyo, lakini kama alivyosema mtoa mada, Lissu yuko mbele kwa miaka mia tano.

Kwanza alijua wote watatu watakataa hawatajitokeza na pili, alishangazwa kidogo kwa ujasiri wa huyo moja kujitokeza.

Sasa hebu fikiria huo ujumbe aliopewa Lissu na huyo kufikisha kwa majaji wa mahakama na namna alivyouwasilisha..kudos!
 
Back
Top Bottom