Inawezekana kweli Lissu amewatangulia Wanasheria wa CCM kwa miaka mia moja mbele

Mijadala kama hii inakuzidi kimo ndugu yangu, kaa mbali nayo. Kinachoongelewa hapa ni uhaini, tendo ambalo nina hakika hata ungepewa miaka kumi huwezi kuelewa ni tendo gani!
Acha porojo.. elekeza hapa ikiwa Lissu Kaivua nguo mihimili ya serikali then what!
 
"Kuwa upande" na "kuwa sehemu" ni vitu viwili tofauti.
 
Acha porojo.. elekeza hapa ikiwa Lissu Kailua nguo minimalist then what!
Nilikuasa huu mjadala unakuzidi kimo kaa nao mbali. Ona sasa. hapo juu umeandika nini? Leo utalala njaa hata hiyo buku ya Lumumba huioni. Kwa kuanzia nakuweka kwenye ignore wewe na hizo takataka unazofuatana nazo. JF kweli imekuwa kokoro inazoa tu...kwaheri!
 
Bora ukimbie tu mana hujiwezi na huwezi kuhimili mawazo kinzani
 
Halina ubishi!
 
Je umejiuliza kwa nini Kingai alikuwa na ujasiri wa kufika ndani ya mahakama lakini akakosa uthubutu ya kuwakabili majaji?
Kwanini Lissu hakufungua shauri kumlazimisha Kingai atoe ushahidi?...
 
Kama hadi maneno aliyosema mshtakiwa hujayaelewa, mimi sina hoja ya kukwambia ukaelewa
Suala siyo kuelewa. Ukinukuhu maneno ya mtu inabidi uyatumie maneno yale yale aliyotumia yeye. Ukibadili neno au maneno yake, hiyo siyo tena nukuhu bali unakuwa unamlisha maneno kama wewe ulivyokuwa unamshutumu huyo mwenzio.

Kibaya zaidi, kuna hatari ya kubadili maana ya alichokisema kama nilivyokuonyesha.
 
Sijasoma hata uzi ila naunga mkono kwa aslimia 50%
 
Sawa
 
Endeleeni kumpamba huku mkiwa magetoni kwenu mwenzenu yupo gerezani

Lissu hahitaji kupambwa anahitaji kuungwa juhudi kwa vitendo hayo mapambo yenu hayamsaidii chochote
Gereza ni kama hospitali TU halina watu maalumu wa kuingia gerezani,kama ilivyo kwa hospitali

Unaweza kufungwa kwa kumgonga mwanafunzi akivuka Barbara wakati wewe ukienda kazini.
Amefungwa Bashir Al Asad wa aliekua RAIS wa Sudani,alifungwa Charles Taylor,alifungwa Slobodan Milosevic walieokua ma Rais wa Liberia na Serbia.
MAGEREZA na hospitali yamejengwa kwa ajili ya wanadamu.
 
Dogo, tunza haya mawazo yako. Hukumu ni tarehe 25. Akichomoka uulete tena. Ila akihukumiwa kunyongwa hadi kufa ujue wewe ni nyumbu tu.
 
Ila CHADEMA mna kelele mitandaoni!
Haya kawazidi kwa miaka 100 then what!?
Ila CCM huwa ni wajinga sana,ndio maana Wana CCM unaweza ukampa kofia na fulana imeandikwa chagua CCM ili akupigie kura na akakupigia hata kama hutamletea maendeleo.

Unachodhihaki ni kwamba Bado Lisu Yuko gerezani licha ya kuwazidi akili mawakili na CCM.
Kwa akili zako unaona ni sawa TU mmoja ya Mihimili ya Dola kuiweka mfukoni Mihimili mingine miwili.
Ukiona nchi yoyote isiyoheshimu MAHAKAMA ujue nchi hiyo imekufa,kumbuka MAHAKAMA ni Chombo kitakatifu.
Kama hakuna MAHAKAMA huru maana yake hakuna utawala Bora.
Na nchi isiyo na utawala Bora ni nchi ya hovyo na isisyo ya kistaarabu.
Ila wewe mwana CCM huwezi kuelewa umuhimu wa utawala unaofuata haki.
Kumbuka bila haki hakuna amani.
Huko tuendako Kuna dalili mbaya Kwa watawala wasiofata haki hapa nchini.
Ila wewe Kwa sababu ni kipofu endelea kujivunia mnachomfanyia Lisu.
 
Hii kesi siifatiliagi sana kwa upande wa kisheria na kikatiba maana sidhani kabisa kama iko huko. Huu nauona ni mchezo unaochezeshwa na siwezi kufurahia matokeo yoyote maana sioni kama ni uhalisia. Zaidi nalaani tu uonevu anaofanyiwa Toto
 
Dogo, tunza haya mawazo yako. Hukumu ni tarehe 25. Akichomoka uulete tena. Ila akihukumiwa kunyongwa hadi kufa ujue wewe ni nyumbu tu.
Unajua wewe kijana ni mjinga,unadhani sisi hatujui hata aina ya hukumu inayoweza kumpata Lisu?
Kwa MAHAKAMA ya Tanzania hukumu inapangwa ikulu sio mahakamani.
Tuna uzoefu na kesi za namna hii toka zama za Mtikila.
Mtikila alikua anaishinda serikali Kwa KESI zote lkn haki yake alikua hapewi.
Nyinyi mhukumuni Lisu mnavyoweza na sisi wananchi tutapima.
 
Basi naiomba Ikulu na safari hii kwa Lissu wasifanye makosa!
 
Sawa, Lissu ana akili kuliko wanaCCM wote, ndio nini sasa? What next!
 
Kwanini Lissu hakufungua shauri kumlazimisha Kingai atoe ushahidi?...
Kwa akili za kawaida angeweza kufanya hivyo, lakini kama alivyosema mtoa mada, Lissu yuko mbele kwa miaka mia tano.

Kwanza alijua wote watatu watakataa hawatajitokeza na pili, alishangazwa kidogo kwa ujasiri wa huyo moja kujitokeza.

Sasa hebu fikiria huo ujumbe aliopewa Lissu na huyo kufikisha kwa majaji wa mahakama na namna alivyouwasilisha..kudos!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…