Wanaojua masuala ya uongozi wa nchi zetu Zanzibar na Tanganyika wanisaidie juu ya haya Mawasiliano baina ya Marais wetu Dk. Hussein Mwinyi na Dk. Magufuli (Tanzania).
Nijuavyo ni kwamba Muungano wetu ni wa nchi moja ndani ya Serikali mbili. Uamuzi wa Rais Magufuli unaathiri maeneo yote ya nchi kwa maana ya Zanzibar na Bara kwa ujumla.
Swali langu, Rais Magufuli anaamini hakuna Covid-19 isipokuwa kuna "changamoto ya upumuaji" na ndio maana hapendekezi uvaaji wa barakoa kupambana na janga hilo.
Rais Mwinyi ameweka hadharani kuwa Zanzibar kuna Covid, inaua watu na inaua uchumi wa Zanzibar na kutaka wananchi kuchukua tahadhari. Je, Magufuli hawezi kumuadhibu Mwinyi kwa nini atangaze uwepo wa Corona ndani ya nchi ya Tanzania na si changamoto ya upumuaji?
Msemaji wa Serikali ya Tanzania, Dk. Abbas anasema, "hatujasema Tanzania hakuna korona'! Watanzania tushike lipi na la nani? Kwa nini kabla ya kuzungumza masuala ya Kitaifa pakawepo Mawasiliano na uamuzi wa pamoja?
Nawasilisha!