Inawezekana vibwengo ni viumbe wageni kutoka sayari nyingine(aliens) wanaozuru duniani

Inawezekana vibwengo ni viumbe wageni kutoka sayari nyingine(aliens) wanaozuru duniani

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kuna stori nyingi hasa za wanafunzi wa shule za sekondari kuona au kukutana na viumbe wa ajabu ajabu wasioeleweka ambao wamepewa jina maarufu la vibwengo.

Stori nyingi huwa zinawahusisha hawa viumbe wanaodaiwa kuonekana na uchawi, tatizo kubwa Waafrika mambo mengi yasiyoeleweka huwa yanahusishwa na uchawi, majini au ushirikina.

Ukiwasikiliza watu wa West wanapoongelea viumbe kutoka sayari nyingine nje ya dunia wenye teknolojia ya juu sana kuliko binadamu unaweza kufikiri vibwengo ni aina fulani ya aliens, labda huwa wanakuja duniani wanajaribu kufanya mawasiliano na binadamu ila kunatokea mgongano wa mawasiliano wanaishiwa kufikiriwa ni viumbe vya uchawi.
 
Vibwengo na Aliens ni viti viwili tofauti. Mimi ni mmoja wa watunwanaofatilia ancient alien theories, vibwengo ni aina ya majini tu
 
Vibwengo ni zygote zilizotokana na mimba zilizokusudiwa kuharibiwa na binadamu lakini kiroho hazikuharibika au zilihuishwa na mashetani zikafanikiwa kuwa viumbe mifano ya wanadamu wenye umbo dogo usawa wa kuku Mtetea au Paka mkubwa na akiwa mrefu sana ni usawa wa Jogoo

Ni kiumbe kisumbufu, chenye hulka ya kutishia Binadamu lakini zaidi kumtesa sana aliyekusudia kutoa mimba iliyombeba yeye

Vibwengo hawatahiriwi kamwe na hawamwagi damu zao asilani

Vibwengo hawanyoi nywele zao

Kibwengo ana uwezo wa kukuua Wewe Mtu mzima mwenye kilo 120

Vibwengo hufa lakini baada ya miaka mingi tofauti na Bin-Adam
 
Swala la uwepo wa Aliens ni Assumptions tu hakuna hao viumbe, watu wanasema kwamba ni viumbe wenye akili sana ni kipi walichofanya kuthibitisha hilo?
 
Kuna stori nyingi hasa za wanafunzi wa shule za sekondari kuona au kukutana na viumbe wa ajabu ajabu wasioeleweka ambao wamepewa jina maarufu la vibwengo.

Stori nyingi huwa zinawahusisha hawa viumbe wanaodaiwa kuonekana na uchawi, tatizo kubwa Waafrika mambo mengi yasiyoeleweka huwa yanahusishwa na uchawi, majini au ushirikina.

Ukiwasikiliza watu wa West wanapoongelea viumbe kutoka sayari nyingine nje ya dunia wenye teknolojia ya juu sana kuliko binadamu unaweza kufikiri vibwengo ni aina fulani ya aliens, labda huwa wanakuja duniani wanajaribu kufanya mawasiliano na binadamu ila kunatokea mgongano wa mawasiliano wanaishiwa kufikiriwa ni viumbe vya uchawi.
Umetoa taarifa ama Uzi??
 
Swala la uwepo wa Aliens ni Assumptions tu hakuna hao viumbe, watu wanasema kwamba ni viumbe wenye akili sana ni kipi walichofanya kuthibitisha hilo?
Ukifika kwenye sayari zao ndio utajua kama wana akili au hawana akili
 
Kwanini walipotea? Je katika viumbe wote waliopotea ni wao tu? If yes why?
Kuna viumbe wengi wamepotea duniani kwa sababu mbalimbali, kupotea kwa dinasours kunahusishwa na janga la asteroids, mabadiliko makubwa ya hali hewa au mlipuko wa volcano.
 
Back
Top Bottom