Inawezekana vipi mtu aliyekuja Dar es Salaam mwaka 1992 kukosa kiwanja?

Pesa ilikuwaa ngumu kwa kipindi hiko kama ambavyo ni ngumu kununua kiwanja mil 6 kwa Sasa hivi. Ndo ilikuwa ni aghali ku unua kiwanja kwa laki 1 kipindi hiko. So usiwatukane watu.
Sidhanii mkuu, labda ungesema kipindi kile watu walikuwa waungwana hivyo bei ya viwanja haikuwa ikipanda kwa kasi sana hivyo watu walikuwa wame relax na pindi kipato kikianza kupanda kiasi cha kuweza kujenga ananunua kiwanja na kuanza kujenga tofauti na sasa unaanza na kiwanja hata kama hujui lini utaanza kujenga maana ukizubaa bei inakuwa mara 2 ya mwaka jana.
 
Mbona tupo born here here na hatuna hata kipande cha ardhi cha futi 6 kwa 6!
 
Hayo maeneo sio kuwa hayakuwa na watu bali yalikuwa mashamba ya watu hivyo viwanja havikupatikana kwa kuvamia tu na kufyeka pori...
 
Kwani analala nje? Dunia tunapita, hivi vyote tutaviacha.
 
Jambo ambalo binadamu wanatofautiana ni kwenye matumizi ya akili..........ndo maana unaweza kuona tofauti kubwa ya kimaendeleo iliyopo kati ya mzungu na ngozi nyeusi, ni hilo tu..........
 
Mali tunazozimiliki sio kwa akili zetu ni kwa neema ya aliyepo juu. Unaweza kuta mtu yupo ofisini mshahara mzuri na hana kiwanja wala nyumba lakini ukamkuta muuza utumbo,fundi cherehani,muuza mihogo,konda wa daladala anamiliki kiwanja na kijumba cha room 2. Haya mambo ni kuweka dua ili Mungu akupe kibali kwanza na kufanya kazi. Ora et labora that goes the Latin maxim.
 
Mambo gani yasiyohusisha ardhi[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Mambo yote lazima uwe na ardhi. Makazi, kilimo, ufugaji, teknolojia n.k

Au hata uzeeni utakuwa unatafuta kodi kuwalipa wenye ardhi wakajenga?
Tatizo liko wap? Mkinunua nyie inatosha [emoji3][emoji3]
 
Tatizo liko wap? Mkinunua nyie inatosha [emoji3][emoji3]
Tatizo litakuwepo kama hutakuwa na makazi katika uzee wako, kama biashara/ajira yako itashindwa kukutunza katika uzee wako.

Ule umri wa 80's 70's au dharura ya disability (MUNGU akuepushe nayo) ukashindwa kufanya kazi ukajiingizia kipato ukaweza kulipa kodi ya eneo la biashara na makazi.
 
Ila ukifikiria ni kweli aisee.. ngoja nitafute eneo hata kama ni nje ya mji.
 
Ila ukifikiria ni kweli aisee.. ngoja nitafute eneo hata kama ni nje ya mji.
Kabisa mkuu. Hata 20 kwa 20 nje kabisa ya mji huko ukaweka kanyumba ka vyumba viwili msururu ka m5 incase of emmergency kisha ukaendelea na mapambano.
 
Inategemea mkuu,jumamosi juzi Kuna jamaa nyumba yake ilikuwa inapigwa mnada baada ya kuachana na mkewe.Ikiuzwa atagawiwa vijipesa kidogo afu awe hana nyumba Tena.Ukikutana naye baadaye hana hata kiwanja.Mambo yanabadilika kwa kasi Sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…