Inawezekana vipi mtu kuweka roho yake kwenye mti?

Kwani unataka tuanze kukuelezea namna wazungu walivyoua mila desturi na tamaduni zetu, na kisha kuweka mifumo ambayo itatulemaza milele?!
Mzee wako kaweka roho msituni hafi ila mwili unaoza. Mzungu anakuzuiaje kutoa hiyo taarifa? Mbona ukirikodi tu video na kuelezea kinachoendelea waandishi wa habari watajazana hapo. Ikitokea mara nyingi hiyo elimu itakuwa wazi.

Kuna shida mahali.
 
Sahihi kabisa, kumbe humu wazee wezangu mpo wengi sana. Kujitafuta kuna mengi sana, enzi zetu lazima uage nyumbani na hayo ndo mazindiko yenyewe tuliofanyiwa kabla hatujaondoka.
 
Ni kweli, kijijini kwetu kuna bibi mmoja yeye mtoto mchanga hata augue vipi ukimpelekea anamwangalia anakwambia njoo kesho na kiasi flani cha pesa uchukue dawa yako, na asilimia 90 ya watoto wanaponea kwake na dawa za mitishamba za majani na mizizi
Bibi kwanini msimfate akaweka wazi hiyo elimu ya matibabu? Au wazungu wamewazuia?
 
Ni wilaya ya Mlele barna Madame B nakujua kwenu kule! Nishawahi kusikia sana story kama hizi
 
Mzee wako kaweka roho msituni hafi ila mwili unaoza.

Kuna shida mahali.
Kutokufa na kuoza kwenye scenario kama hii ni exception case, na hakuna kitu kina advantage kikose disadvantage hiyo ni nature, ndio maana pia dawa za mzungu tunameza ila zinaharibu figo, hapa tunaangalia advantage mtu aliyopata kuanzia kuwekewa imemkinga na hatari ngapi mpaka kufikia huo umri wa tamati
 
Hiyo elimu ipo na watu wanaitumia, ni wewe hapo huijui kutokana na mifumo iliyowekwa inayopanga wewe ulishwe nini na ufichwe nini,
Wajanja wachache ndo wanajua
Ipo wapi? Kwanini haipo kwa uwazi? Mbona elimu nyingine za asili zipo kwa uwazi? Dawa za asili zipo kibao kwa uwazi, ukihitaji mafunzo yapo tena mjini kabisa wazee wanakufundisha aina za miti na namna ya kuitumia. Kwanini hiyo ifichwe fichwe? Ina ubaya gani?
 
Shida ninayosema ni elimu kubwa kama hiyo iwe ya kufichwa fichwa, ipo kwenye hadithi na hakuna hata mmoja anayeweza toka hadharani akasema huyu mzee hafi huyu hapa. Hafi sababu roho ipo kwenye miti.
 
Shida ninayosema ni elimu kubwa kama hiyo iwe ya kufichwa fichwa, ipo kwenye hadithi na hakuna hata mmoja anayeweza toka hadharani akasema huyu mzee hafi huyu hapa. Hafi sababu roho ipo kwenye miti.
Mkuu kuna mambo yapo ila hayasemwi, binafsi hii kesi ya mdau nimeshuhudia sana ila kwa kule kwetu sijawahi shuhudia mtu akioza huwa wazee wanamuwahi wakiona hapa hamna kitu, Na wapo wazee mpaka dakika hii wana umri mrefu hawaumwi ila familia zao zinasema huyu naye ana kizizi. Na dawa za kuwaondoa zinatofautiana pia
 
Ndo maana nakwambia kuna shida mahali. Either hiyo elimu ina gharama kubwa sana ambayo jamii haiwezi kuikubali au ni elimu ya mdomoni ukiingia kujifunza unakuta si kweli. Otherwise, jambo kama hilo lingeshakuwa rasmi.
 
Mzee hana presha wala kisukari?
 
Sasa kwa ujenzi wa kisasa wa mapaa ya gipsum utatoboaje?
 
Wai aisee usidharua tamaduni za Africa na ndio msingi wetu sss
 
Na mm nakubaliana na wewe mnk wazee wwetu ndio ilikuwa tamaduni zao na zilifanya Kaz vzr tu leo tuvijna wanaona utamaduni Kama uchawi wakt mungu yupo na tamaduni zipo palepale
 
Ni wilaya ya Mlele barna Madame B nakujua kwenu kule! Nishawahi kusikia sana story kama hizi
Ndio hukohuko.
Origin yangu ni Tanganyika, sema si unajua tunapokuwa wakubwa huwa tunapakwepa kwetu kwa sifa za uchawi..😕
Ila kwetu wamezidi asiee.
Huwa kunakuwaga na mashindano ya uchawi mchana kweupe.
Na unaitoa roho yako sadaka, ukifa mchezoni hakuna wa kulaumiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…