Inawezekana Wamarekani ni wajinga ajabu? Wamemchagua mwanaume na kumtosa Mwanamke. 2025 Watanzania tuchague mwanamke kuonesha tuna akili zaidi yao?

Inawezekana Wamarekani ni wajinga ajabu? Wamemchagua mwanaume na kumtosa Mwanamke. 2025 Watanzania tuchague mwanamke kuonesha tuna akili zaidi yao?

Kwa Marekani Sawa maana dunia ilikuwa imeshachafuka sana

Trump kachaguliwa kutokana na sera zake

Ukilinganisha na huyo Mwingine


Kwa tanzania Rais hachaguliwi kisa sera! Bali Maguvu! Kulinganisha hivi vitu viwili si sahihi


Britanicca
 
Siamini kama pamoja wasomi wote makazini na mitaani, kuwa kimawazo akili yetu imefikia hapa. Nilifikiri kuwa hoja zingekuwa nini kimefanyika/hakikufanyika katika kipindi alichokuwepo madarakani. Lakini kwa bahati mbaya hoja imekuwa ni Me au Ni Ke, Aisee! siamini.

Ila nasikitika sana kwa ma -Great Thinkers- Tumefika pabaya. Siwezi kumshauri ndugu, Rafiki au jirani kutembelea JF baada ya maandiko haya.

Vizuri niachie hapo, kwa maana nikiendelea nitatapika yasiyohitajika. Niweke akiba!
 
Wanabodi,

Hapo nilipo bado nimepigwa bumbuwazi na matokeo ya uchaguzi wa Marekani, na kujiuliza
Inawezekana hawa Wamarekani ni majitu majinga ajabu! Wamemchagua rais mwanaume, na kumtosa Mwanamke kwasababu tuu ni mwanamke?

Mnaonaje kama 2025, sisi Watanzania tuchague mwanamke ili kuonyeshea kuwa tuna akili zaidi yao hao majinga ya Marekani?

Na kufuatia matokeo haya, sisi akina Tomaso, sio watu wa kujikalia tuu na kujiuliza, ngoja tufanye michakato ya kusogelea maeneo ya karibu na golini kujua ni nini haswa kimetokea, maana...

Duh!

Paskali

"Kafulila: Hii ndio dhana halisi ya Rais Samia kufungua nchi, Leo biashara ya nje imekua kutoka Trilioni 47 Mwaka 2021 mpaka Trilioni 87 mwaka 2024"​

Nilifikiri Tutajadili haya maendeleo. Hivi tumepotea katika akili zetu.
 
Mataifa mengine yote yanaweza kuongozwa na mwanamke isipokuwa kwa mataifa yenye nguvu hasa United states. So ku-Compare USA na Tanzania unakosea sana mkuu. #myonlyview
 
Uislamu hata ukristo vinazuia mwanamke kutawala wala kuongoza wanaume. Kwani, mwanamke ni kiwiliwili na mrume ninl kichwa. Sasa inakuwaje sasa mwili unaongoza kichwa badala ya kichwa kuuongoza?
 
Back
Top Bottom