Mr Why
JF-Expert Member
- Nov 27, 2019
- 2,992
- 5,665
Inawezekana Wanawake wana nidhamu ya pesa kuliko sisi Wanaume, nilishuhudia kwa macho yangu Kikoba cha Wanawake Mpesa chenye zaidi ya milioni 100 katika makundi 10
Wanawake wananitisha sana kwenye maswala ya management ya pesa kwasababu nikama wana uwezo mkubwa sana wa kutunza fedha kwa muda mrefu kuliko sisi Wanaume ila sina uhakika
Kuna kundi la Wanawake wa mtaa mmoja lilinishangaza sana, hawa akina mama waliniomba niwasaidie kuunga Mpesa kupitia App ili waweze kufuatilia Kikoba chao, walikua na Vikoba 10 kila kimoja kina ml 10, nikawaonesha namna ya kufunua salio jambo lililonishangaza walikua na zaidi ya ml 100 katika vikundi vyao 10
Nikawauliza je huwa hamdhulumiani wakanambia tangu wameanza vikundi hivyo hawajawahi kukosana na maisha yanaendelea kama kawaida na walishafikia hadi ml200, 100 wakagawiana ili wainuane kwenye kazi zao
Wakanambia hata wakiachika wanauwezo wa kujijengea nyumba kila mmoja wao, hawakuishia hapo wakanambia wameamua kuungana ili watakaponyanyasika kwenye ndoa wawe na uwezo wa kumiliki mali zao wenyewe