Benjamini Netanyahu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2014
- 95,871
- 116,627
Thinks tank wa Tz ni akina Kibajaji, Mwigulu, Ndugai, Sabaya, Makonda, Mnyeti, Ally Hapi, Mrisho Gambo, Bashiru, Makamba, Jery Muro, n.k unategemea nini?Hakuna neno lingine zaidi ya haya ni maajabu?
Kenya ina watu milion 53 huku Tanzania ikiwa na watu takribani milion 60.
Ukubwa wa Tanzania ni kilomita za mraba laki 9++ huku kenya wakiwa na eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba laki 5++.
Nchi ya Tanzania iko mbele mara elf moja dhidi ya kenya ktk mambo yote yenye kuleta faida kubwa kiuchumi kwa kuanzia maliasili, malighafi, madini, utalii, rasilimali watu, jografia nzuri na siasa safi.
Umoja uliopo Tanzania ni mkubwa mara elfu dhidi ya ule wa Kenya ambao wako kimakundi makundi tokana na ukabila.
Sasa inawezekanaje nchi kama Kenya ikawa na bajeti ya Tshs Trillion 66 huku Tanzania ikiwa ni Tshs Trillion 38?
Mambo haya yanawezekanaje jamani? Kwa bajeti hio ya kenya ni wazi kwamba wenzetu hawa kila kitu wako mbele yetu mara mbili zaidi!
ni nchi ya ajabu hii jamani daah.