Inawezekanaje bajeti ya Kenya ikawa kubwa mara mbili ya ile ya Tanzania?

Uzalishaji hafifu wa Tanzania, tunge jikita katika kuzalisha na kuuza zaidi bidhaa nje ya nchi kuongeza kipato na income ya mtu mmoja mmoja, viongozi wetu wanafanya vitu basic mno hadi aibu, tuna sera nzuri sana Tanzania mdomoni na kwenye Karatasi, lakini utekelezaji ni zero, hatuwezi kamwe na haitakuja tokea hata siku moja tukaendelea kwa kutegemea misaada, sasa hii misaada ndio sera halisi iliyo tufikisha hapa, kila Rais anataka afanye juu chini kuwafurahisha wakubwa apate misaada, wana sahahu kuwa duniani kote sekta za uzalishaji kama vile kilimo, viwanda ndio zinaweza kututoa katika umasikini, yanayobaki yote ni upotezaji wa muda.
 
Uchumi wa kenya ni mkubwa sana ukilinganisha na huu uchumi wenu wa tozo....
 
Kwa hiyo wao hawalioni hilo tatizo, isipokuwa ww mtanzania ndiye unayeona matatizo Yao hayo. Tukubaliane tu kuwa wao walianza mapema kugawana shughuli za kufanya. Serikali kazi yake ikawa kukusanya kodi, na si kufanya biashara,, kuweka mazingara ya kupatikana ruksa za kuwekeza . Kwetu kila kitu ilikuwa ni kufanya na serikali, matokeo ni uzembe na uporaji wa mitaji ya serikali, baada ya hapo, aliyepora anaondolewa kigoma anapelekwa Dodoma. UNATEGEMEA KITU GANI KITATOKEA?. HADI LEO HAKUNA KUWAJIBIKA WALA KUWAJIBISHANA KI SHERIA.
 

Makosa ya kisiasa yalitugharimu sanaaaa
Nauchukia ujamaa ulitulea vibaya
 
Correction ni vita kuu ya kwanza ya Dunia. Kifupi ilitakiwa tuwe huru mapema pamoja na Egypt (1922), South Africa (1934) na Sudan (1947).

Lkn umasikini wetu ni matokeo ya ujeruman kushindwa vita. Inamaana ujerumani ingeendelea kututawala washindani wetu wangekuwa South Africa au tungewapita.

Waingereza ndio waliotufanya tuwe masikini maana muda wote walitulea kama mtoto wa kambo.

Lkn mi Tanzania tulivyo wajinga tunaiona uingereza ndio Kila kitu kuliko German.
 
Thinks tank wa Tz ni akina Kibajaji, Mwigulu, Ndugai, Sabaya, Makonda, Mnyeti, Ally Hapi, Mrisho Gambo, Bashiru, Makamba, Jery Muro, n.k unategemea nini?
Vituko, na leo tuna kikao Cha ccm kinaendelea bungeni unategemea Nini?

Kenya wako mbali sana, wajinga ni wachache mno.

Kwa utawala wa magu 2015-2021 kule Kenya vita ingetokea live. Lkn huku watanzania hawajitambui Kwa Kila kitu.
 
Bro uclinganishe bajet ya tajir na masikin hata siku moja. Bajeti ya Mo dewji kwa cku ni sawa na watu wote wa tandale kwa cku. Tatizo tunapenda kubishana lakin hatusemi ukweli. Wakenya wako mbali mno.
 
Sababu ni nyingi ila chache ndo zimeirudisha Tz nyuma sana:
1. Mfumo tulioachiwa na Wakoloni.. Wakoloni waliacha Kenya na maendele sana tofauti na sie yakuwemo mashule,Hospitals na mtandao wa Barbara.
2. Idd Amin Dada kwa %kubwa sana aluturudisha nyuma sana kutokana na Vita ya Kagera kwani kipindi hicho shilling ya Tz Na Kenya zilikua sawa ila vita isikie tu imeturudisha nyuma sana maana zana nyingi za kivita tulikopa hivo kuanza kulipa miaka na miaka...
3. Hatukua na wataalamu wengi yani wasomi ambao wangeweza kuendeleza nchi
4. Sera yetu ya ujamaa iliturudisha nyuma sana kwani haikuchochea ushindani wakimaendeleo zaidi ulitudumaza kwa maana ya wote tuwe sawa ata ukipambana uwe na Mali basi aidha Mali zako zilitaifishwa au kupewa kesi ya uhujumu uchumi

Hizo ni chache kati ya nyingi kwanini Kenya wanatuzidi...
5. Kenya ina viwanda vingi sana hivo import/export kwao inakua kubwa...
 
Samahani mkuu nikuulize swali nje ya mada kidogo.Umewahi kuona mtu anakichwa kikubwa lakini hakiendani na uwezo wa akili?
 
Umeelezea vema. Zaidi ya hapo kihistoria, pia Waarabu wa Ghuba hususan Oman, wameathiri TZ kifikra na mtizamo kuhusu maendeleo. Hii inahitaji elimu ya kina ya historia.
 
Vituko, na leo tuna kikao Cha ccm kinaendelea bungeni unategemea Nini?

Kenya wako mbali sana, wajinga ni wachache mno.

Kwa utawala wa magu 2015-2021 kule Kenya vita ingetokea live. Lkn huku watanzania hawajitambui Kwa Kila kitu.
CCM inataka kuwa na watu wajinga wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…