Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Unaposema France unamaanisha nini?
Kwamba France kale ka sehemu ya Ulaya tu ambapo empire yake kule west Africa, Visiwa vya Carebean , Guyana, Mayote viko chini yake au France mtaa uliopo kule Sumbawanga?

Mwingine kaitaja Denmark hajui kuwa Greenland ni sehemu ya Denmark?
 
Kati ya makosa ninayoamini yalifanywa na baba wa Taifa ni kukumbatia sera ya Ujamaa.

Japo inawezekana ujamaa ulisaidia kutufanya kuwa wamoja, ulichangia pakubwa kutudidimiza kiuchumi.
Hakukuwa na makosa yoyote maana nchi haikuwa tayari kuingia kwenye Ubepari
 
Mentality Waafrika tunamentality ya kimasikini.
 
Mabadiliko makubwa ya kimfumo na kimtazamo yanahitajika
 
Inawezekana sio kitu cha ajabu, wametuzidi kwenye mengi na pia ukilinganisha wale ni developed country kwahyo mpunga wanao
 
1. Denmark ina uchumi mkubwa na ulojitosheleza na ni ule uitwao Mixed Economy.

2. Denmark wana kiwango kikubwa cha wasomi yaani wananchi wengi wana shahada MUHIMU za chuo kikuu.

3. Denmark ni moja ya nchi zinoongoza kwa sayansi na teknolojia duniani.

4. mfumo wa kodi wa Denmark ni mgumu sana, uko juu na wabana kila senti uipatayo VAT pekee ni asilimia 25. Kodi kwa mashirika yaani corporate ni asilimia 22 na wageni wote wa kitaalam hutakiwa kujiandikisha ili waweze kulipa kodi.

5. Denmark wana kiwango cha juu cha maisha kwa wananchi wake.

Hayo ni baadhi tu ila kikubwa ni kwamba Denmark kama zilivyo nchi zingine za Ulaya watumia akili zao kwa manufaa ya nchi zao.

Na mfano wake ni pale ambapo wazitenga kabisa fedha zao za misaada kwa mataifa yenye kuongozwa na viongozi ambao akili wameweka mifukoni.

Afrika mtu akiwa na nafasi au madaraka akili zetu huamua kuziweka mfukoni na kuiba fedha za kodi na kuwanyonya wananchi wenzake.

Akitokea mwafrika mwenye kutaka kutumia akili kuleta manufaa kwa nchi yake wale waafrika wenzie waloweka akili zao mifukoni, kuamua kuzihamisha kwa muda akili zao na kufanya mambo ya kihuni na kikatili.
 
Kila siku huwa naelezea kuwa Mungu alifanya upendeleo wakati anawaumba wazungu navyohisi alipokuwa anawaumba wazungu akawawekea ubongo ila alipokuwa anawaumba weusi akawawekea Ugali kichwani badala ya ubongo.

Plan ya Mungu kumuumba binadamu sidhani kama alikuwa anamanisha binadamu weusi. Tatizo la Afrika sio kwenye rasilimali zake lipo vichwani mwa watu wake.

Afrika tunapoelekea pamoja na neema ya bara letu itafika point tunadondoka kwa njaa kwa sababu kiakili hatujiwezi kabisa ndio maana tunashinda makanisani kutia huruma kwa Mungu. Na mbaya zaidi ma dini yenyewe yameletwa na wazungu ambao kwa sasa hawana time nayo sisi ndo tunayashobokea mpaka yanatuongezea umasikini wajinga sisi.
 
Huyo Magufuli nae ni mwehu mwingine wala sio wa kumention humu. Bora hata ungemtaja JK NYERERE ila huyo mwehu anatawala badala ya kuongoza ni kielelezo cha mfalme juha ambae alishawahi pita hapa nchini.
 
Wazungu hawatoweza kuongoza matahira kutazua taharuki sana. Hivi unajua kuwa watu wenye akili ndogo huwa ni vinara wa kulalamika
 
Viongozi huwekwa na watu na watu wenyewe ndio sisi so why tusiwabadilishe?
 
Msilinganishe mataifa ya Ulaya na Nchi za Afrika...

Mataifa ya Ulaya yapo miaka 1000 kabla ya nchi yoyote ya Afrika kuanza kuwa nchi, Denmark ndio nchi ambayo bendera yake haijabadilika zaidi ya miaka 500
 
Kama ni model za uzalishaji tuliaga za China but why chines wakafanikiwa kuliko sisi, sote tulikuwa hatuna technology na maarifa?
 
Ukubwa wa taifa siyo Kilomita za mraba za eneo la nchi bali ukubwa wa maarifa na ujuzi wa watu wa taifa husika.
Akili ni mali Mkuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…