Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Siyo Denmark pekee. Vinchi vyote vidogo huko Ulaya, na baadhi huko Asia, ukilinganisha na Tanzania ni aibu tupu:

Denmark
Norway
Finland
Sweden
Singapore
Switzerland

Utajiri mkubwa hapa Ulimwenguni ni akili, wala siyo idadi kubwa ya fisi na pundamilia, siyo dhahabu na gas, ardhi nzuri ya kilimo, maziwa, bahari au hali nzuri ya hewa.

Hata upewe vyote, ukinyimwa akili, vyote vinakuwa havina maana. Lakini ukibahatika ukapata akili,ni mwanzo wa mafanikio yote. Kwanza utajua ni nini kilicho muhimu, utakuwa na mifumo mizuri ya kuvuna rasilimali, utakuwa na tekinolojia, utakuwa na mifumo mizuri ya utawala, na mifumo mizuri ya kusimamia uchumi kwa ujumla.

Sisi tuna vitu vingi, lakini asilimia kubwa sana ya watu wetu wamenyimwa akili, utashi na maarifa. Ndiyo maana wachache wenye akili, maarifa na utashi, ama wanakuwa frustrated na kukata tamaa au kuishia kwenda kufanya kazi mataifa ya nje kwa sababu nchini mwao ni giza nene.
🙌
 
Denmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.

Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?

Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.

Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.

Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.

Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.

Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?

Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.

Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?

Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.

Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?
Tatizo ni chama Cha Mapinduzi
 
Si ndio nachosema? Mnapenda maendeleo ila hamjui namna au watu wa kuwapa maendeleo. Ushawahi kufanya kazi kwenye nchi zilizoendelea ukaona au kujifunza namna wanavyoishi na kufanya kazi?
Tumegee kidogo uzoefu wako mkuu.
 
Inawezekana sababu wao wako kinyume na sisi katika mengi. Ila kikubwa ni kwamba wamekabidhi nchi kwa watu serious na sio kuwapa madaraka watu wa hovyo kama tufanyavyo huku kwetu.
 
Kati ya makosa ninayoamini yalifanywa na baba wa Taifa ni kukumbatia sera ya Ujamaa.

Japo inawezekana ujamaa ulisaidia kutufanya kuwa wamoja, ulichangia pakubwa kutudidimiza kiuchumi.
Ujamaa sio tatizo endapo ungeboreshwa kidogo. Shida ni kukumbatia wajinga madarakani.

Siasa imegeuzwa ajira na wananchi tumekubaliana na hilo. Sisi ndio tatizo namba 1! Siku tukijitambua tukasema hapana imetosha sasa, maendeleo ya kweli yatapatikana.
 
Jibu Ni "uongozi Bora wa kizalendo"
Uzalendo haukai pamoja na kutowajibika. Ukishaona taifa linakumbatia viongozi wazembe na wasiotaka kuwajibika jua maendeleo yatabakia kuwa historia. Umaskini ndio utabaki kuwa wimbo milele.

Utawala bora na siasa safi ndio key.
 
Ujamaa sio tatizo endapo ungeboreshwa kidogo. Shida ni kukumbatia wajinga madarakani.

Siasa imegeuzwa ajira na wananchi tumekubaliana na hilo. Sisi ndio tatizo namba 1! Siku tukijitambua tukasema hapana imetosha sasa, maendeleo ya kweli yatapatikana.
Nyakati za uchaguzi, viongozi wengi huwa wakarimu sana. Mara mgao wa khanga, fulana, sukari, sabuni, mpaka na hela.

Halafu watu hawahoji sababu za huo ukarimu wakati wa uchaguzi au karibu na uchaguzi tu.

Hata Serikali, kuna baadhi ya shughuli za kimaendeleo huzishughulikia uchaguzi unapokaribia, halafu wapiga kura kimyaa, hakuna kuhoji.
 
Denmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.

Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?

Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.

Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.

Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.

Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.

Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?

Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.

Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?

Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.

Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?
Usishangae. Kwanini ndege pamoja na udhalili wao wana viota lakini tembo, pamoja na maguvu yake hana hata kibanda.
 
Uzalendo haukai pamoja na kutowajibika. Ukishaona taifa linakumbatia viongozi wazembe na wasiotaka kuwajibika jua maendeleo yatabakia kuwa historia. Umaskini ndio utabaki kuwa wimbo milele.

Utawala bora na siasa safi ndio key.
Utawala Bora na Siasa safi
 
HIMA-DANIDA, Ni miongoni mwa project kubwa iliyokuwa chini ya Denmark na ilinufaisha wengi
 
Embu subiri kwanza, umesemaje? Kwamba wanataka kuufunga ubalozi? Wametuhusisha kutoa maoni? Itakuwaje sasa? Wakija kufanya maamuzi wawe kwanza wanatuuliza wenda kuna kibabu changu huko mtaenda kukitembelea ubalozi uendelee bana huwezi jua nikawa huko nikataka msaada wa ubalozi🤣🤣🤣
 
Ina maana hujajua tu mpaka leo

Mapungufu yanayoikabili nchi hii

Ova
 
Sisi tunaangushwa na viongozi wetu, kupitishatu bajeti mpaka wabunge wahongwe. Yaani Africa tumelogwa na nani?
Viongozi wanatokana na wanananchi. Walivyo viongozi ndo walivyo wananchi maana wanachaguliwa na wananchi, Viongozi hawashuki kutoka sehenu nyingine itoshe kusema tatizo ni wananchi wenyewe wa Afrika. Kama unabisha kwanini kama shida ni viongozi wananchi mmechukua hatua gani kuwawajibisha Viongozi??

Tatizo ni WANANCHI wa nchi husika ndo msingi maana viongozi wanatokea miongoni mwetu ata ww ukiwa kiongozi leo utapita mule mule.
 
Kumbuka kuna neno KUBWA JINGA na DOGO JANGA.

Sisi ni makubwa yasiyo na akili.
Yupo mzungu alifanya research akaibuka na matokeo kuwa waafrika ndio race yenye IQ ndogo kuliko zote akapingwa kuwa ni racist lakini mim mpaka leo nakubaliana nae.
 
Mchawi ni rangi mtu mweusi hata akizaliwa USA lazima liwe ndo lijinga jinga lenye ma tabia mabaya kwenye jamii.
Nakubaliana na wewe mkuu.
Siamini kuwa binadamu wote ni sawa.
Sio kweli kuwa watu weusi na wazungu tuko sawa.
Naamini kabisa kuwa sisi weusi tuna ubongo dhaifu kulinganisha na ule wa wazungu
 
Back
Top Bottom