Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Sisi tunaangushwa na viongozi wetu, kupitishatu bajeti mpaka wabunge wahongwe. Yaani Africa tumelogwa na nani?
Ni roho mbaya tu sisi kila mtu anajifikiria yeye na familia yake na wapambe wake wanaomsifu !! Wenzetu wanafikiria zaidi Nchi zao na wananchi wote kwa ujumla !!
 
Wa Danish ni watu waadilifu mnoo na wachapa kazi.

Pili wanaaminiana kuliko taifa lolote.
Nimeishi na nimefanya nao kazi zaidi ya 12yrs.
Kuna mengi ya kujifunza
Hivi DANIDA ni nini?
 
As long as watu Kama
1. Mwigulu
2. January
3. Nape
4. Mbarawa
Ndio wanasaini mikataba kwenye nchi hii, hakika Kuna siku tutapokea misaada kutoka Rwanda.
 
Kama ilivyo sisi watu wa mjini kuwasaidia watu wa vijijini
 
Tatizo letu ni misingi mibovu iliwekwa toka tulipopata uhuru.

Tulipata uhuru wa kupandisha bendera zenye rangi tulizotaka au uhuru wa kisiasa lakini uhuru wa kifikra na uhuru wa kimtazamo kwa mtu mweusi bado hajaupata jumlisha uhuru wa kiuchumi ambao ni matokeo ya uhuru wa kifikra
 
Ni kanuni ya maisha anaetoa ndie anaebarikiwa.
Wazungu uwasaidia waafrika ili wazidi kuwa masikini zaidi,wanajua pesa zinadakwa juu kwa juu then zitarudi Tena kufichwa bank za ulaya na majizi ya Africa
 
Denmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.

Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?

Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.

Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.

Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.

Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.

Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?

Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.

Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?

Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.

Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?
Wanawapatia misaada viongozi wa Tanzania ambao wapo kwenye nafasi zao kuiba na kupora
 
Sidhani ni tangu tulipopata uhuru, sema tangu tulipozaliwa.

Maana kama ni misingi mibaya baada ya uhuru, mpaka leo ni miaka mingapi? Hiyo misingi mibaya kwa nini haibadilishwi? Mbona mataifa mengine yaliyopata uhuru baadaye, kama Botswana na Namibia, wao angalao wanapiga hatua kwa kasi?
Botswana na Namibia bado Wana raia wengi wazungu.
Awakutaifisha Mali za watu baada ya Uhuru.
 
Magufuli alipotaka kuigeuza Tanzania iwe sawa na nchi za Ulaya mlimfanyaje? Mnataka maendeleo lakini hamtaki namna ya kuyafikia hayo maendeleo. Maendeleo ni malengo, nidhamu, kujitoa mhanga (self sacrifice), bidii ya kazi, uadilifu na kutambua vipaji na ubunifu na kuvitumia ipasavyo. Ulaya wameweza kuviunganisha hivyo vyote kufikia hapo walipo. Sisi hapa bado tunajitafta na akija mwenye mawazo kama hayo bado hatumwelewi. Tutachelewa sana.
Hajawahi kuwa na mwelekeo wowote wa kuipeleka nchi huko unakokusema, yule alikua ni mpiga kelele tu.
Keleke zilikua nyingi kuliko vitendo. Ukute angekuwa hai hata ile Ikulu isingekamilika, maana alishahamia CHATO.
 
Wanatoa misaada au Rushwa za kutaka upendeleo.....Hatahivyo kihistoria Misaada yao ilikuwa kama kufedhehesha Ufalme wa Uingereza ambao umekuwa ndio Dhalimu kuliko Wazungu wa aina yeyote ile Duniani.

Kabla ya Umoja wa watu wa Ulaya kulikuwa na Vita za wenyewe kwa wenyewe, kulikuwa na vita za kikabila, kulikuwa na vita za Rasilimali, kulikuwa na vita baina ya wajasiriliamali, yaani wachuuzi(machinga) na matajiri..... Kwa lugha Nyingine, Hakuna Mzungu mmoja(umoja) kama unavyotaka kuaminisha...Mzungu alipata akili pale alipoona Dini haimsaidii, alipoona laana ya ukatili wake unamsumbua yaani mizengwe baina yao iliwatafuna sana mpaka wakawa masikini wa kutupwa. Wachache walijiondokea katika nchi zao/kabila zao kutaka kupata suluhu za Kiroho, suluhisho za kisiasa, suluhisho za kijamii na suluhisho za kiuchumi....

.Denmark ni muunaganishi wa makabila au jamii zilizotoka kwenye Makabila makatili madhalimu kuwahi kutokea Ulaya. Walitaka kujitawala na kuondokana na Machungu na laana na Umasikini uliowakumba, maradhi na vita zilizowaangamiza kwa kuachana na Viongozi wao hususani wale waliofaidika na Udhalimu wa Ufalme wa Uingereza. Story Short.....kwa namna moja au nyingine hawakuweza kujikwamua, kisiasa, kiuchumi, na kijamii kutokana na vizingiti walivyowekewa na majirani zao ambao bado walikuwa na ulinzi wa hekaya za Ufalme wa Muingereza....Ila baada ya Umoja wa Mataifa kuundwa na subsequently Umoja wa Ulaya bado kulikuwa na kamshipa wa Kujikomboa na Kujitawala na ndio maana Denmark walitusaidia na sio kwamba walikuwa matajiri. Kumbuka hata Denamrk walikuwa wakilipwa na Dhalimu Mwingereza ili anyamaze.

Denmark hivi karibuni waliweza kuiga aina ya Uongozi wa Uthubutu na Uamauzi wa kujikomboa kama wa Hayati ambamo walisitisha Hafla za Kitaifa na kupeleka hela hizo kusaidia Nchi yao katika nyanja za Afya n.k. Hivyo basi Tanzania imeweza kuisaidia Denmark sio hivyo tu, Rasilimali ambazo Dernmark amelipwa aidha kwa mali au malipo mengine ya hali yamewasaidia kufika hapo walipofika.

Tusijidharau na kuwapa Wazungu tano wasizo deserve!
 
Back
Top Bottom