Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Denmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.

Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?

Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.

Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.

Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.

Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.

Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?

Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.

Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?

Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.

Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?
Mtu mweusi ni hatari kwa afya ya dunia.
 
Tatizo viongozi na wananchi wa Tanzania wana attitude kama changudoa.. kuogopa kuvuja jasho.. maneno kibao, action zero..

Yaani full kujilegeza..
Vinginevyo hakuna sababu ya nchi yoyote kuisaidia Tanzania..
Nafikiri mfumo wa kikoloni wa kucharaza bakola watu wazembe ulikuwa mzuri.. tungekuwa mbali sana..
Natumai sauti inatosha
 
Huyo Magufuli nae ni mwehu mwingine wala sio wa kumention humu. Bora hata ungemtaja JK NYERERE ila huyo mwehu anatawala badala ya kuongoza ni kielelezo cha mfalme juha ambae alishawahi pita hapa nchini.
Upumbavu na ujinga huu, ndio haswaa sababu ya tulipo na tutaendelea kuzidi kuwa chini!

Shida yako wewe ni Magufuli kuwa mtawala na siyo kiongozi tu basi?

Ila ukasahau kabisa misingi mhimu aliyokuwa akiiweka?

Usimamizi bora, nidhamu serikalini (maofisini) zikikosekana hizo, ndio chanzo cha kila umasikini wa nchi na wananchi

Hata wazazi wako na hata wewe ukikosa vigezo hivyo, hutatoboa
 
Unaposema France unamaanisha nini?
Kwamba France kale ka sehemu ya Ulaya tu ambapo empire yake kule west Africa, Visiwa vya Carebean , Guyana, Mayote viko chini yake au France mtaa uliopo kule Sumbawanga?

Mwingine kaitaja Denmark hajui kuwa Greenland ni sehemu ya Denmark?
Hata visiwa vya Unguja na Pemba viko chini ya Tanganyika.
 
Hizo ni fikra tu. Hatuna uhakika kama mambo yatabakia vile vile au yatabadilika, kwa sababu hatujawahi kubadili uongozi na mifumo yake hata mara moja. Ila tu tumejazwa na imani kuwa hali itakuwa vile vile.
Sijui ni mwaka gani aina ya uongozi tulio nao utabadilika.

Sent from my Pixel 3 using JamiiForums mobile app
 
Just imagine... Unanunua tiketi kwa ajili ya watu ambao wangeweza kujinunulia tiketi... What a wastage of resourses any way yani Muumba aje tu atutwae wote[emoji34][emoji34][emoji34]
Ila kwa kweli hii nchi yani ukifikiria vzr Ina mambo ya hovyo kuliko alafu watu wanafurahi kabisa mambo ya hovyo yanafanyika watu Wana matatizo lukuki huku mtaani maji hakuna umeme hakuna kila.kona matatizo alafu pesa zinaenda kwenye mipira yani ujingaujinga tu
 
Tumegee kidogo uzoefu wako mkuu.
Yeah mtu wa kawaida anaweza kufanya kazi zaidi ya tatu tofauti ili mkono uende kinywani. Waajiri hawana simile au uvumulivu wa uzembe au ubadhirifu wa aina yoyoye ile. Matokeo ya kazi yanapaswa kuonekana sasa hivi ili kujihakikishia kibarua chako ukifanya kazi taasisi ya aina yoyote ile. Huo ni baadhi ya uzoefu wangu tu. Magufuli alileta ile model ya tumbua tumbua na kuonyesha hulka ya kutovumilia uzembe wa aina yoyote ile matokeo yake kale kafala kakaanza kumuita dikteta uchwara. Leo hii eti mnajiuliza Denmark inawezaje?
 
Hajawahi kuwa na mwelekeo wowote wa kuipeleka nchi huko unakokusema, yule alikua ni mpiga kelele tu.
Keleke zilikua nyingi kuliko vitendo. Ukute angekuwa hai hata ile Ikulu isingekamilika, maana alishahamia CHATO.
Sawa
 
Nayo pia ni kanchi kadoogo, inaingia Tanzania zaidi ya mara mbili, na kana population ya watu milioni tano tu, lakini inaipa Tanzania misaada.

Ila Wazungu nao!!! Kama vile hawawaamini watu weusi.

Mwaka 2009, niliingia ibadani kwenye Kanisa moja mkoani Kilimanjaro. Mchungaji wa hilo Kanisa alikuwa amerejea kutoka Finland alikoenda kuomba msaada. Katika taarifa aliyoitoa Kanisani ya safari yake, alisema Wafinish wamekubali kuufadhili mradi husika ila hawatatuma pesa, watakuja kuusimamia wenyewe. Walikuwa na mashaka kuwa kama wangewapatia pesa taslimu, huenda zingetumika isivyostahiki.

Yaani hawawaamini hata Wachungajui?
Wenzetu Wana akili sio sisi tunaswagwa kama kuku kila siku.kuimba nabii flani sijui nini ujingaujinga tu
 
Ukubwa wa pua si wingi wa kamasi.Jiulize ki nchi kama Belgium kutawala linchi likubwa kama Congo -Belge.
Halafu kumbe Kabelgiji nako ni kadoogo, hakafikii hata mkoa wa Arusha, kana ukubwa wa kilomita za mraba 30,688 huku Arusha ikiwa na kilomita za mraba 37,576.

Ingawa kana population ya watu milioni kumi na moja, lakini ni tajiri mara nyingi kuizidi nchi kuubwa, Tanzania na jirani yake Congo D.R.C.

Eti kanchi kadoogo vile, Belgium, kanashika nafasi ya sita kwa utajiri barani Ulaya.

Au ni wachawi sanaa?
 
Kati ya makosa ninayoamini yalifanywa na baba wa Taifa ni kukumbatia sera ya Ujamaa.

Japo inawezekana ujamaa ulisaidia kutufanya kuwa wamoja, ulichangia pakubwa kutudidimiza kiuchumi.
Kuna mwingine pia alisema hata kupigana vita ya Kagera kuliigharimu uchumi wa nchi , sijui kama Kuna ukweli wa hili.
 
Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.
Tanzania imewazidi Denmark kuwa na wasomi wengi wenye PHD ambao majina yao yananza na Dr. Siku hizi wameongezeka na wengine nimeona wanaanza na CPA so and so. Matunda ya wasomi hawa hayaonekani. Badala ya kujikita kuendeleza nchi yetu kupitia fani walizosomea wanakimbilia kwenye siasa ambako hela zipo njenje. Kama tunataka kuendelea mishahara ya wabunge ipunguzwe iwe milioni moja na watumie public transport tuone kama wataendelea kutoana macho kuutaka ubunge. Bunge lenyewe ukiangalia wabunge wanaokuwemo mjengoni wakati mijadala muhimu inaendelea zaidi ya robo tatu hawamo. Kuna haja gani kuwalipa mahela yote wanayopata halafu tutegemee nchi yetu kupata maendeleo!!
 
Back
Top Bottom