Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Najua lengo la swali lako.
Kwamba kwa vile mim ni mweusi nipingane na ukweli kuwa mtu mweusi ni janga na hana akili.

Natamani kupinga na kusema kwa fuahari kuwa mim mtu mweusi ni bora na mwenye akili kama binadamu wengine wote ila nafsi inanisuta sababu sio kweli na hata nikijidanganya kuwa nina akili kama wazungu haitasaidia kitu.
Nimekubali! Una akili sana mkuu!!!
Hata maelezo yako yanatanabaisha hilo. Yaelekea ulikuwa mzuri sana kwenye debate!

Unajua jinsi ya kujenga hoja kutetea kile ulichokidhamiria, hata kama sicho unachomaanisha.

Ni kweli? Usijibu hapa watu wasije wakakuona wewe ni kigeugeu, lakini imeshafahamika kuwa una akili sana bila kujali rangi ya ngozi yako.

Kongole kwako mkuu!
 
Hayo yote, na hata zaidi ya hayo, ni mazuri, lakini Tanzania haijafikia kipindi cha kufanya hayo. Tungeyafanya hayo "baadaye", tutakapokuwa tumeshatajirika!
Hatuwezi tajirika bila kuuondoa ubinafsi
 
Kama watu wanaenda zindua ndege, ynategemea maendeleo yatoke wap?
 
Hakuna sheria ya kumfunga fisadi bongo zaid ya mwizi wa kuku.
Denmark ukwepe Kodi,au ufisadi Kodi hata jua utoliona
Nchi zingine raha sana. Mtu hatafuti madaraka kwa sababu ya njaa.

Afrika sasa.... nakubaliana na mtu aliyewahi kusema chanzo cha vita vya wenyewe kwa wenyewe barani Afrika ni "njaa"
 
Nchi zingine raha sana. Mtu hatafuti madaraka kwa sababu ya njaa.

Afrika sasa.... nakubaliana na mtu aliyewahi kusema chanzo cha vita vya wenyewe kwa wenyewe barani Afrika ni "njaa"
True hata chanzo Cha vita vinavyoendelea Congo ni tumbo la mobutu na njaa ya kagame
 
Ukubwa na udogo wa nchi unaupimaje ?

Resources (natural) sio msingi wa maendeleo..., hata Japan lacks natural resources na mara nyingi resources ni curse (refer Congo)....

It all comes down to necessity being the mother of all invention..., (Tanzania naturally hatuna shida kila kitu kinapatikana hata walafi wachache wakiacha kulamba asali mpaka makombo tunaweza kuishi bila kutoa jasho).
 
Nchi kama Denmark hawana makabila 120 na zaidi. Taifa karibia lote ni kabila moja, lugha ni moja, culture and way of thinking and way of life ni moja. Pia walibebwa sana na ruzuku za USA bada ya vita vya pili vya dunia ili kuinua uchumi wao. Denmark ni sawa na kusema Mwanza iwe nchi ya taifa la Wasukuma tu, sema Wasukuma nao wana Waislamu na Wakristo. Wazawa wa Denmark hamna hilo, karibia Wazawa wote asilia WAZUNGU wanazaliwa kwenye dini moja inayoongozwa na Serikai. Kila sehemu ya maisha yao ipo highly regulated sababu ni kabila moja la watu wanaoelewana kwa kila kitu. Nchi nyingi za Ulaya zimeundwa hivyo. Ni watu wa kabila moja, dini moja, lugha moja, utamaduni mmoja. Sasa washindwe vipi kupata maendeleo?
 
Tufanyeje ili na sisi tuwe kama wao?
1. Kwanza watanzania wote wenye umri wa kulipa kodi walipe kodi yaani mtu akimaliza shule au chuo mara tu apata barua ikimkumbusha kwamba akianza kazi atakuwa "subject" na kodi. Hapa nazungumzia kodi ya maendeleo ambayo wananchi ni lazima waelimishwe ili walipe hii kodi na kuondoa misururu ya kodi au tozo zingine ambazo hazina maana.

2. Kila biashara iliyopo iwe kubwa au ndogo ilipe kodi kulingana na mapato yake. Hii na namba 1 hakuna utani kwani wenzetu ni waaminifu sana katika makusanyo ya kodi na matumizi yake.

3. Mikoa yote ijitegemee kimipango na kiuchumi ila kiasi fulani kiende serikali kuu(madaraka mikoani) na si majimbo. Ile mikoa ambayo yajiweza kiuchumi iwe ni vigumu kuishi (kwa watu wa kipato cha chini) kuwa na kodi kubwa na vyanzo vingine vikubwa vya mapato ili kusaidia mikoa mingine iinuke kiuchumi na kimaendeleo.

4. Kuanzishwe taasisi za maendeleo katika kila mkoa ambazo zitabuni na kuunda mipango ya maendeleo ya mikoa, wananchi waweze kuchagua mameya na madiwani wanowataka na si kungiza siasa, hii wenzetu waita ni "local democracy".

5. Kuwepo ufuatiliaji na usimamizi wa vyanzo vya mapato na fedha zitokanazo na vyanzo hivyo. Fedha zikusanywe na ziingizwe hazina bila kupitia mikono mingi ambayo itasababisha upotevu. Hivyo hapa TRA, Bandari, na taasisi zote ambazo zatakiwa kuipa serikali gawio zinakuwa zawajibika kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Haya ni baadhi tu ya maono yangu ila kuna mambo mengi ya kuyaweka sawa maana miaka 61 ya uhuru imepita lakini Tanzania kwenye karatasi yaonekana ni tajiri lakini kiuhalisia ni taifa lenye wananchi wasojielewa wataka nini huku uchumi wao ukiwa mikononi mwa wachache.
 
Kwa nchi kama Tanganyika na nchi zote za Afrika, ambayo mipaka yake iliamuliwa na Wazungu kwa kutumia rula kwenye mkutano wa Berlin 1884-1885, sahau kupata maendeleo ya kweli. Mataifa ya kizungu yapo kikabila zaidi, lakini kwa Afrika mataifa yamebaki na mipaka ileile ya Berlin Conference ya 1884-1885 hadi leo ambapo nchi moja ina makabila 100 na zaidi.
 
Kwa nchi kama Tanganyika na nchi zote za Afrika, ambayo mipaka yake iliamuliwa na Wazungu kwa kutumia rula kwenye mkutano wa Berlin 1884-1885, sahau kupata maendeleo ya kweli. Mataifa ya kizungu yapo kikabila zaidi, lakini kwa Afrika mataifa yamebaki na mipaka ileile ya Berliin Conference ya 1884-1885 hadi leo ambapo nchi moja ina makabila 100 na zaidi.
Lakini pamoja na mipaka ilowekwa na Berlin Conference 1884-1885 bado zipo nchi barani Afrika zina maendeleo makubwa tu Botswana, Namibia, Rwanda (baada ya vita iloisha 1994) ni mfano wa nchi zinoonyesha kuwa kukiwa na nia na malengo thabiti, basi maendeleo huja kwa kasi.

Sasa sisi hadi leo twahangaika na soko moja tu la Kariakooo lilijengwa na wajerumani na tumeshindwa kujenga masoko mengine makubwa katika kila mkoa au wilaya na wananchi wapanga bidhaa zao ardhini na pembezoni mwa barabara.
 
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
3. Mikoa yote ijitegemee kimipango na kiuchumi ila kiasi fulani kiende serikali kuu(madaraka mikoani) na si majimbo. Ile mikoa ambayo yajiweza kiuchumi iwe ni vigumu kuishi (kwa watu wa kipato cha chini) kuwa na kodi kubwa na vyanzo vingine vikubwa vya mapato ili kusaidia mikoa mingine iinuke kiuchumi na kimaendeleo.

4. Kuanzishwe taasisi za maendeleo katika kila mkoa ambazo zitabuni na kuunda mipango ya maendeleo ya mikoa, wananchi waweze kuchagua mameya na madiwani wanowataka na si kungiza siasa, hii wenzetu waita ni "local democracy".

5. Kuwepo ufuatiliaji na usimamizi wa vyanzo vya mapato na fedha zitokanazo na vyanzo hivyo. Fedha zikusanywe na ziingizwe hazina bila kupitia mikono mingi ambayo itasababisha upotevu. Hivyo hapa TRA, Bandari, na taasisi zote ambazo zatakiwa kuipa serikali gawio zinakuwa zawajibika kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.
🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏
Ingelikuwa ni maamuzi yangu, hayo mawazo yangeingia kwenye utekelezaji haraka sana.
 
Lakini pamoja na mipaka ilowekwa na Berlin Conference 1884-1885 bado zipo nchi barani Afrika zina maendeleo makubwa tu Botswana, Namibia, Rwanda (baada ya vita iloisha 1994) ni mfano wa nchi zinoonyesha kuwa kukiwa na nia na malengo thabiti, basi maendeleo huja kwa kasi.

Sasa sisi hadi leo twahangaika na soko moja tu la Kariakooo lilijengwa na wajerumani na tumeshindwa kujenga masoko mengine makubwa katika kila mkoa au wilaya na wananchi wapanga bidhaa zao ardhini na pembezoni mwa barabara.
Nini? Soko la Kariakoo lilijengwa na Mjerumani? Ni kweli mkuu?

Sikuwa nafahamu hilo. Kama ndivyo, Mjerumani alikuwa ni mkoloni mzuri japo inasemekana alikuwa mkali sana na mbabe mno.
 
Siyo Denmark pekee. Vinchi vyote vidogo huko Ulaya, na baadhi huko Asia, ukilinganisha na Tanzania ni aibu tupu:

Denmark
Norway
Finland
Sweden
Singapore
Switzerland

Utajiri mkubwa hapa Ulimwenguni ni akili, wala siyo idadi kubwa ya fisi na pundamilia, siyo dhahabu na gas, ardhi nzuri ya kilimo, maziwa, bahari au hali nzuri ya hewa.

Hata upewe vyote, ukinyimwa akili, vyote vinakuwa havina maana. Lakini ukibahatika ukapata akili,ni mwanzo wa mafanikio yote. Kwanza utajua ni nini kilicho muhimu, utakuwa na mifumo mizuri ya kuvuna rasilimali, utakuwa na tekinolojia, utakuwa na mifumo mizuri ya utawala, na mifumo mizuri ya kusimamia uchumi kwa ujumla.

Sisi tuna vitu vingi, lakini asilimia kubwa sana ya watu wetu wamenyimwa akili, utashi na maarifa. Ndiyo maana wachache wenye akili, maarifa na utashi, ama wanakuwa frustrated na kukata tamaa au kuishia kwenda kufanya kazi mataifa ya nje kwa sababu nchini mwao ni giza nene.
Tatizo la Tanzania ni wizi,ukabila,rushwa na ujinga wa watu wanaongoza nchi ndio sababu umasikini mwingi Wananchi ni wanafiki wapumbavu na hudanganyika kirahisi sana na wanauoga na hofu ya maisha yao ni kama vile wanaishi utumwani na slave master is the government it’s actually amazing to understand Tanzania in 2023 . Still in the middle age.
 
Back
Top Bottom