Income ipo, expenses za ofisi zipo chini yake lakini profit haiendani na juhudi

Ni mauzo mkuu sasa kwa ushamba wa biashara sikuwaza yote hayo mradi kila siku naondoka na kitita 🀣🀣🀣
Na mzigo nilikua nachukua mali kauli sana, mwisho unajikuta kila supplier anakudai na inabidi unnue mzigo maana dukani umekata aloooh sikia kwa jirani tu 😭
 
150 mpaka 200 kila siku kama faida na mtaji haukui🀣🀣 bora ushike jembe tukalime mama
 
500k profit? That's roughly 15m per month.
Hiyo sio biashara ndogo, hata mtaji wake sio mdogo, soko lake ni kubwa pia. Tunaongelea mtu mwenye 100m+ kama mtaji
Ni sawa nilikuwa naongezea tu hapo, fatilia watu wenye saluni kubwa za kucha na nywele! Wanapata pesa sikufichi..
 
Biashara kama tatu zote niliziua kwa kuchanganya na matumizi yangu ya kila siku , yani hakuna kitakacho ongezeka, utakua una maintain tu biashara either isife ili uishi ila kukua sahau.
Ndiomaana biashara inaweza maliza mwaka unaishia kulipa madeni na kodi tuπŸ€¦πŸ½β€β™€οΈ
 
Fungua kabiashara kingine ka ziada unakuwa na more than one option hiyo ziada unaweka mtu unayemuamini kusimamia huku wewe ukiendelea na hiyo at the end of the day unakuwa na double source of income
 
Nimecheka sana mkuu, una kibunda cha 200k unajua hapa nina mzigo wa kutosha kumbe ya kwako haifiki 15kπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Hii biashara inaingiza faida kubwa mno, margin ni zaidi ya asilimia 50 so kitaalamu biashara yako ina Afya nzuri tu.

Kinachokukwamisha wewe sio expenses wala faida Bali mzunguko mdogo wa biashara yako.

Je kuna uwezekano wa kuipanua? Kuongeza watu ama branches?
 
500k per day ni mauzo au faida mkuu?
Mi naona ni faida, mfano wewe una saluni ya kike, Ni naturalist, lets say unasuka at least watu 40 each weekend na atleast 20 weekdays each 30,000 daily una shingapi kwa kwa siku?
Unatengezea kucha 50,000 kwa siku una watu 20+ unashingapi hapo?
Mind u sio za pembeni hizi ni zile zipo town..
 
Ukigawa hiyo 59k kwa kila siku ni kama 8k hivi. Nahisi kama faida ni ndogo bado haiwezi kabisa kusustain biashara, japo mleta mada kasema ina vary, huenda kuna wiki inapanda zaidi.
 
Umenitia moyo sana! Mzunguko sio mkubwa maana sio mjini, pia nimewaza kufanya hivyo ni either nianzishe nyingine au niipanue hiyo kwa kuhamishia eneo jingine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…