Habari wana JF,
Naomba msaada wa mawazo kutoka kwa wenye uzoefu. Nina biashara ndogo ambayo kwa wiki inaweza kuniingizia kati ya
50,000 hadi 100,000, ingawa
sio kila siku kuna biashara.
Kinachonitatiza ni kwamba, licha ya kuwepo kwa kipato,
matumizi yanabaki kuwa makubwa kuliko pesa inayoingia.
Mfano halisi: wiki ikaingia
59,000, lakini matumizi yakafika
38,000. Matumizi hayo yanahusisha
chakula,
bili za umeme na maji, pamoja na
baadhi ya vifaa. Ikabaki
21000, nadhani hapo naelekeka sasa namaanisha nini..
Baada ya kuondoa matumizi,
faida inayobaki ni ndogo sana, kiasi cha kunifanya nishindwe kuelewa kama biashara hii inanipa faida ya maana au inanizungusha tu.. income>Expenses, lakini faida ya biashara inaonekana ndogo
Kwa uzoefu wenu:
- Je, hali kama hii ni ya kawaida kwenye biashara ndogo?
- Ni vipi naweza kupumguza expenses bila kuua biashara?
- Au kuna mbinu za kuongeza faisa hata kama mauzo si ya kila siku?
View attachment 3540163
Cha ajabu kwenye records monthly expenses zinashuka na faida kuonekana ipo, lakini sio kipato nilicholenga kulingana na biashara inavyoenda! Wajuzi mnisaidie naona navurugika kila nikifanya recordings, huwa nina kawaida ya kurecord kila ninachofanya, sasa naona siridhizishwi na haya matokeo ya mwisho!
NB, wale wanaotaka kujua aina ya biashara ni urembo in general..