India: Mwanaume ameza kifaranga cha kuku ili apate mtoto

India: Mwanaume ameza kifaranga cha kuku ili apate mtoto

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Dunia inamaajabu yake na vituko kutoka kwa binadamu!

Sasa man anataka apate mtoto kwa kumeza kifaraga baada ya kuambiwa na mganga wa kienyeji. Ila hawa waganga wa kienyeji wa hovyo na wapumbavu si Afrika pekee duniani kote akili zao zinafanana ili kuwapoteza wajinga ambao wanaamini katika imani hiyo tena bila kufikiria anachoambia je kinafaa kufanyika au hakifai!
=================

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 35 kutoka Jimbo la Chhattisgarh Nchini India, amefariki dunia baada ya kumeza kifaranga cha kuku kilicho hai katika tukio ambalo linaaminiwa kuwa ni sharti alilopewa na Mganga ili apate tiba ya matatizo yake ya uzazi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Madaktari walioufanyia mwili uchunguzi walibaini kifaranga hicho cha urefu wa sentimita 20 kikiwa hai nakuziba njia ya hewa na chakula hali iliyosababisha Marehemu Anand Yadav kufariki kwa kukosa hewa.

Inadaiwa kuwa Anand, aliyekuwa akihangaika na matatizo ya uzazi alikwenda kwa Mganga wa kienyeji ambaye huenda alimshauri kufanya kitendo hicho kwa imani kuwa ingesaidia kupata Mtoto.

Polisi wameanza uchunguzi kubaini mazingira ya tukio hilo na jinsi gani imani za kishirikina zimechangia kifo hicho ambapo tukio hili limeibua mjadala mpana kuhusu madhara ya imani potofu na haja ya elimu sahihi kuhusu afya.
 
Nafahamu madhila wayapatao wenzetu waliokosa uwezo wa kuzaa/kuzalisha.

Lakini tangu lini uwezo wa kumpa mimba Mwanamke unaletwa Kwa kumeza kifaranga cha Kuku 🙌

Tuliwahi kuambiwa, bora ukose mali upate akili
 
Back
Top Bottom