Sijalewa maana bado ni asubuhi sana. Tanzania haijwahikuwa na Katiba. Ila Zanzibar na tanganyika ndo zilizkuwa na katiba zao. Baada ya kuiungana mwaka 1964 hakujawahi kutengenezwa katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanganyika na Zanzibar. Isipokuwa ilikubaliwa kuwa iliyokuwa katiba ya Tanganyika ndiyo itakuwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Wakati huo Zanzibar ilikubaliwa kubaki na Katiba yake na Serikali yao. Serikali ya Tanganyika ndo ikapata ubatizo na kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tangayika na Zanzibar.
Hivyo, popote paliposomeka Tanganyika katika Katiba ya Tanganyika iliboreshwa na kusomeka Tanganyika na Zanziba. Baada ya jina kubadilika kuwa Tanzania miaka kadhaa baada ya muungano, paliposomeka Tanganyika na Zanzibar katika katiba paliboreshwa na kusomeka Tanzania.
Kwa mujibu ya Katiba yetu, Mamlaka ya Waziri Mkuu Mkuu yanaishia pale ilipokuwa mamlaka ya Tanganyika. Mwisho malili 1 kiutoka ufukwe wa Fery.
Ndo maana huwezi kumuuona waziri Mkuu akielekeza nini kifanyike huko Zanzibar. zanzibar ina waziri Mkuu wake a.k.a Wziri Kiongozi. HII NCHI NGUMU SANA.