India yapoteza ndege 5 za kivita katika siku ya mwanzo ya vita

India yapoteza ndege 5 za kivita katika siku ya mwanzo ya vita

Nawakumbusha tena mana tumeumbwa kusahau , hivi mnakumbuka ule mgogoro wa mwaka juzi India na Pakistan? India hawa hawa hawakomi na ndege zao
Yule rubani wa India aliyetunguliwa na Pakistan si mnakumbuka?
Asalaleeeee Pakistan walitakiwa kuwa Yemen wale unaambiwa muhindi wa watu hata hajafika chini na parachuti
.
Wanakijiji wa Kipakistan washachuma fimbo , mwenye rungu, mwenye kata kucha hadi mchi wa kutwangia kisamvu wanamsubiri ashuke wampe dozi nene,

Yule rubani wa India pona pona yake ni askari jeshi la undava undava ugaidi ugaidi Pakistan kumuwahi, sijui mnakumbuka lakini🤣🤣
 
Ndege na meli za kivita vinazidi kudhihiri kuwa si silaha tena za kujidai katika uwanja wa vita.
Pakistan hana sababu ya kurusha ndege kuingia India kwa sasa labda huko mbeleni.
Kwa sasa ni kuwasha data za mitambo ya kutungulia ndege na makombora tu.Halafu irushe ballistic ndani ya India.
Meli ya kivita kubwaa limeshaumizwa na Houth pekee ndani ya red sea na iko njiani irudi kwao kabla hali yake haijaathirika zaidi na kuzidondondosa ndege zote ilizobeba.
Pakistan ina ndegevita na inaendelea kuunda na inaendelea kununua. Inajua kwanini inafanya hivyo na haiendani na unachokidai hapa.
 
Porojo zitaendelea hivihivi ghafla utashangaa majeshi ya India yapo ndani ya Pakistan na majenerali wa Pakistan wametoroka na familia zao kwenda Uingereza.

Tupo hapa. India ikipigwa na Pakistan nafuta account.
Mkuu unapenda kuongopa siku hizi!
Hizo nguvu za India kuingia ndani ya Pakistani kirahisi zitoke wapi!?
Ingekua hivyo Pakistan asingeshinda vita nyingi za mpakani dhidi ya India.
 
Nawakumbusha tena mana tumeumbwa kusahau , hivi mnakumbuka ule mgogoro wa mwaka juzi India na Pakistan? India hawa hawa hawakomi na ndege zao
Yule rubani wa India aliyetunguliwa na Pakistan si mnakumbuka?
Asalaleeeee Pakistan walitakiwa kuwa Yemen wale unaambiwa muhindi wa watu hata hajafika chini na parachuti
.
Wanakijiji wa Kipakistan washachuma fimbo , mwenye rungu, mwenye kata kucha hadi mchi wa kutwangia kisamvu wanamsubiri ashuke wampe dozi nene,

Yule rubani wa India pona pona yake ni askari jeshi la undava undava ugaidi ugaidi Pakistan kumuwahi, sijui mnakumbuka lakini🤣🤣
Nakumbuka.Na niliiona Pakistan kama taifa lenye huruma sana kwani baadae walimrejesha kwao.
 
Back
Top Bottom