Ingekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini, dunia bila dhambi kipimo cha uovu nini?

Kwani wazee wako huko kijijini miaka si mingi, fanya 90 tu nyuma walikuwa na dini? Dini ni scam.
Ninadhani mleta mada pamoja na wachangiaji wengi hawajui hata wanachokijadili.

Miaka yote jamii karibu zote duniani zikiwemo jamii za kiafrika zimekuwa na dini.

Kabla ya kuletwa kwa imani za ukristo, uyahudi, uislamu, uhindu, ubudha, shinto nk, bado dini zilikuwepo.

Kabla ya kujadili chochote mnatakiwa mkubaliane mnaposema ''dini'' mnamaanisha nini?

Ndivyo ilivyokuwaga mijadala humu JF zamani.
 
Mkuu nimekuelewa vyema, dini kwa upande mwingine ni chanzo cha migogoro na hiyo inatokana na uelewa mdogo wa waumini katika sheria na taratibu za dini zao.
 
Mkuu nimekuelewa vyema, dini kwa upande mwingine ni chanzo cha migogoro na hiyo inatokana na uelewa mdogo wa waumini katika sheria na taratibu za dini zao.
SIYO UELEWA MDOGO, HAO WALIOANZOISHA HIZO DINI NDIO WAMEANDIKA VITABU VINAVYOBAGUA watu wasio wa dini husika.
 
Watu wanajiwekea mifumo yao tu, hata hizo dini ni mifumo iliyowekwa na watu.

Na kama ukivyosema, dini zenyewe hazifuatwi.

Kipimo cha ubaya kinaweza kuwekwa kwa mifumo isiyo ya kidini kama sheria au haki za binadamu.
Sheria za kibinadamu zina nafasi yake katika maisha, pia sheria za dini zina nafasi yake. Hata sheria za binadamu zime copy baadhi ya mambo kutoka kwa sheria za Dini
 
Huenda ni kweli hatuelewi concept ya dini, kama yapo mengine naomba utujuze mkuu.
 
SIYO UELEWA MDOGO, HAO WALIOANZOISHA HIZO DINI NDIO WAMEANDIKA VITABU VINAVYOBAGUA watu wasio wa dini husika.
Kwa mfano hizi dini mbili kubwa, wewe unadhani nani alianzisha na kwa lengo gani hasa
 
Mnazoita dhambi ni moral values ambazo mtu yeyote mwenye common sense anafuata hata kama hana dini. Usiibe, usiue, usizini, usitamani, sambaza upendo nk. Hizi ni morals za kawaida tu huhitaji dini kujua au kufuata.
 
Watu wanajiwekea mifumo yao tu, hata hizo dini ni mifumo iliyowekwa na watu.

Na kama ukivyosema, dini zenyewe hazifuatwi.

Kipimo cha ubaya kinaweza kuwekwa kwa mifumo isiyo ya kidini kama sheria au haki za binadamu.
Karibu sana mkuu, nina siku mbili nawaza kukutafuta maana siku nyingi zimepita.
 
Inamaana binadamu angeweza kujisimamia mwenyewe bila muongozo kutoka kwa aliyemuweka hapa Duniani?
Hakuna aliyemweka binadamu hapa duniani.

Binadamu ameweza kujisimamia mwenyewe kwa kujitungia sheria ambazo huzitumia kumuongoza.
 
Sheria za kibinadamu zina nafasi yake katika maisha, pia sheria za dini zina nafasi yake. Hata sheria za binadamu zime copy baadhi ya mambo kutoka kwa sheria za Dini
Hata hizo sheria unazoziita za dini ni za binadamu tu.

Kwa hiyo unavyotofautisha "sheria za binadamu" na "sheria za dini" sikuelewi.
 
Aknowledge muimbaji MWANA FALSAFA.
 
Mnazoita dhambi ni moral values ambazo mtu yeyote mwenye common sense anafuata hata kama hana dini. Usiibe, usiue, usizini, usitamani, sambaza upendo nk. Hizi ni morals za kawaida tu huhitaji dini kujua au kufuata.
Sawa mkuu, maoni mazuri hayo nimeyaelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…