Hilo la Yanga kupewa ndege nalo sijalifurahia hata ingekuwa kwa Simba bado ningesema.
Kuna timu juzi ilishindwa pesa ya usafiri na ikafukuzwa hotelini ikiwa ina madeni tele.
Erasto nyoni ndio alijitolea kulipa hizo gharama.
Kwa hiyo kama tunasema Raisi anajitoa kwenye michezo tumulike katika aspects zote sio kwasababu wanufaika ni Simba na Yanga basi tuone wengine hawana haki.
Timu ambayo unaisaidia wewe kuipa ndege kwenye mchezo wa ligi kuu ni timu ambayo inauwezo wa ku afford hizo gharama bila kikwazo.