Injinia Soma hiyoo: Simba yasajili striker kutoka Brazil

hahaha Mimi nasevu comment zako
Jana si umeona nlikuwa na furaha tele, hadi nilimuweka whatsup status, ila huyu simweki status,

Huwezi amini nime download vitu vya Msudani lakini huyu hata siangaiki,,

Mkuu nadhani tutaendelea kukutana ktk vilinge vyetu hivi hivi, tutakuwa tunasema hapa

Vitu vya msudani hadi watani wangu walikubali wakasema kabisa hongereni msimbazi hakika mmetupa kazi kubwa ya kusaka namba 6.
 
Mi nawasi wasi na ukuta wetu tu
 
Huwa nikiona mbrazil anakuja bongo hata siwaamini sana,,

Watani wetu si mliwaona akija jaja, cotinno,, hamna kitu
Huyu hafikii uwezo wa okwi hata robo,, tutakuja kumlaum kocha bure kuwa hampangi,,

Huyu hata ktk Taifa stars ya misri angeachwa tu,
Tangu 2012/13 hajafunga Tena goli zaidi ya 4 Hadi Leo 2019
Hapa sio kupigwa Bali Ni kupasuka kabisa
Mkuu labda ungefatilia commentz zangu za jana kuhusu ELDIN yule Msudan, pale tulilenga ila kwa huyu hapana,, kwenye ukweli tuongee tu na kwenye mashaka tuongee kweli,,
Haya ndio ukisikia maoni ya watu wa mpira ndio haya , nimependa maoni na uchambuzi wenu wadau

Km wengi wetu humu tungechangia hivi ,nadhani ule ushabiki maandazi ungepungua km sio kuisha Kabisa
 
Kocha anataka miili jumba kama yeye mwenyewe alivyo
 
Haya ndio ukisikia maoni ya watu wa mpira ndio haya , nimependa maoni na uchambuzi wenu wadau

Km wengi wetu humu tungechangia hivi ,nadhani ule ushabiki maandazi ungepungua km sio kuisha Kabisa
Mkuu nafurai kuona unaujua kuufatilia mpira pengine kuliko hata mm!! Mm nimesusa kufatilia usajili Man utd ni vituko kule,, tutapata shida mwakani Epl,,

Ila kwa Simba bado mapungufu ya namba 5,4,3,6
 
hivi inakuwaje mchezaji anatoka brazil anakuja tanzania? ni dalili ya kukata tamaa kabisa au amekosa timu ya kuchezea huko kabisa. ni sawa na mwanafunzi wa form six arudi chekechea
Ligi yetu inazidi kukua
relax Mkuuuu
Jumatatu usisahau weka bando tu
 
Toka mwaka 2015 amefunga magoli manne tu
Cheki hapo kwenye redView attachment 1133431
Mkuu hapa tulivaa miwani, hadi nna wasiwasi nani kampitisha?

Mi nadhani katika watu wanao husika na usajili kwa huyu nahisi kuna hali ya kutoelewana kabisa,,

Nahisi kuna mtu katumia vibaya cheo alichopewa, huenda wapo waliopinga ila kwa yeye ana nguvu na yuko karibu na Moe,

Hapa hamna kitu jamani uwezo wake kama wa salamba tu. Kwa namna moja watani wetu wanatucheka kabisa yaaani yale ya akina cotino
 
Mkuu nafurai kuona unaujua kuufatilia mpira pengine kuliko hata mm!! Mm nimesusa kufatilia usajili Man utd ni vituko kule,, tutapata shida mwakani Epl,,

Ila kwa Simba bado mapungufu ya namba 5,4,3,6
Mkuu mie mpira naufuatilia vzr mno hasa huu wa Africa na Tanzania, Nina historia nao mpira sana tu ,si uwanjani wala nje ya uwanja ndio maana MTU akiongea facts juu ya mpira nampa pongezi ,akienda tofauti nitampa nachojua muhimu tufike mahali tu sawa

Ingawa kupishana mawazo ni kawaida kwa binadamu
 
Kabisa mkuu,, tufike mahala tuongee ukweli tuache ushabiki wa simba na yanga,,

Mpira wa africa ni mpira mgumu kiukwel, mpira unahitaji nguvu na skillz,,

Tp Mazembe si umeona vijana wao
 
Hofu yangu ni kwamba akikaa bench mechi tatu tu atasusa,maana ataona kadharaulika katoka Brazil aje kukaa bench Tanzania?

Ndugu muangalie msije tengeneza mpasuko ktk timu ,sidhani km hawa wabrazili watataka wakae bench
 
Kwa kuangalia tu youtube hakuna mchezaji hapo. Kwa sababu youtube ni vipande vya clip pale mchezaji alipofanya vizuri. Sasa kwa mbrazili huyu nahisi tumeingizwa chaka. Kiukweli simba ilihitaji sana mshambuliaji sawa na Kagere au zaidi ya Kagere sio huyu wa kuja kumjaribu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…