Innocent Bashungwa amejiwekea rekodi ya kupita na kufanya kazi Wizara nyingi sana.Unafikiri sababu ni nini?

Yule ni kipenyo full stop wala usihangaike kumfuatilia
 
Anaandaliwa 2030, ajipange tu kukwepa vipande vya waganga wa kienyeji na ajali za kutengenezwa
 
Kijana anajitahidi sana kuwa na ile hofu ya Mungu (hata kwa muonekano wake tu) ukimlinganisha na binadamu wengine. Na kwa huo uteuzi wake, naamini vitendo vya kuteka watu hovyo vitafikia kikomo.
Vitafikia kikomo tu pale kama wanaoteka ni Polisi, kitu ambacho sio kweli
 
Magufuli alikuwa wa wawapi?
Msukuma wa Chato mkoani Geita.
Hata hivyo kumpa msukuma pia ilikuwa kosa la kiufundi ambalo halitajirudia japo kwa upande wangu Magufuli nilikuwa namkubali sana na itachukua miaka mingi sana kupata rais bora aliyefikia viwango vya utendaji kazi wa Magufuli.
 
Acha ukabila wa kipumbavu, mbona jiwe na mother wanafanya mengi ya upendeleo lakini husemi. Utendaji wa mtu hauhusiani na kabila lake we bwege
 
Uwaziri Tanzania ni sawa na siti ya daladala. Anakalia yeyote!
 
Ebu tuseme kwa pamoja huyu Innocent Bashungwa ana upekee wa aina gani hadi awe yeye tu ndio Kinyara kwenye teuzi, amekuwq waziri katika wizara 7 ndani ya miaka 5.

Ana Maajabu gani hasa, je, ni mamluki kuna nguvu ina msogeza sehemu nyeti kwa dhamira ya kimkakati au ni nini hasa kuhusu Bashungwa?

Karibuni nyote

Pang Fung Mi
 
Labda ni kushindwa. Anahamishwa kutafutiwa anakofaa.
 
Nyota yake iling'ara ghafla kwa kitendo cha muda mfupi alichokifanya yeye bila kujua kwa kukataa burungutu la mamillioni ya dollar kipindi cha utawala wa Magufuli.

Fedha hizo za mtego zilitumwa na Magufuli kumpima uaminifu wake.

Baada ya kukiruka kihunzi hicho, aliepewa hadhi ya Waziri muadilifu wa taifa, hivyo wizara zote ni zake.

Piga, ua, garagaza ashakuwa ni mtoto pendwa, hawezi kuwekwa benchi hata siku moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…