INSYUKA ni movie bora sana kuwahi kuigizwa na wasanii wa Tanzania haina mpinzani

Hi movie ilitakiwa ipewe heshima yake katika ulimwengu wa sanaa kwa namna bora ya uigizaji na namna ilivyoweza kuleta muamko mkubwa ndani na nje ya tasnia ya bongo movies. Nadhani hio ndio ilikuwa turning point ya bongo movies. Sidhani kama itakuja kuwa na mpinzani labda kwa baadae sana. Kudos kwa waigizaji woteView attachment 2403346View attachment 2403352
Kwangu saladini ndio movie bora hakika bongo movie ilikua zamani
 
Hongera kwa Musa Banzi kwa kutengeneza kazi hii nzuri na nyingine nyingi kama vile Tabana,Game of love,Sakafu wa Moyo,Zogo,Kihongwe,Kiss me,Shenaiza n.k.......Bongo movie ilikuwa na uelekeo mzuri sana mpaka ilipokuwa na uelekeo mbaya
Girlfriend
Saradini
 
Kanumba na wenzie walipoanza kuwaiga Wa Nigeria ndio walipo poteana na hawa wa sasa wanawaiga Wahindi,
Lol [emoji23]
 
Chite ukae pia ilikuwa movie kali sana ila sijui ilikuwaje hawakuweza kumalizia part two
 
Hi movie ilitakiwa ipewe heshima yake katika ulimwengu wa sanaa kwa namna bora ya uigizaji na namna ilivyoweza kuleta muamko mkubwa ndani na nje ya tasnia ya bongo movies. Nadhani hio ndio ilikuwa turning point ya bongo movies. Sidhani kama itakuja kuwa na mpinzani labda kwa baadae sana. Kudos kwa waigizaji woteView attachment 2403346View attachment 2403352
Of course, hii ndio ilikuwa turning point ya golden era of bongo movie, 2003- 2012

Watu wengi wanaicredit filamu ya girlfriend, ila kiukweli hii ndio ilileta mapinduzi

Kwanza ndio ilikuwa filamu ya kwanza kuwa na matangazo kwenye tv kuwa ipo madukani, na postas kibao zilibandikwa na kanda yake kuuzwa sambamba kwenye wauza mikanda kipindi ambacho mikanda mingi ilikuwa ya kinigeria, ama kichina ama kimarekani

Baada ya hii kufanya hivyo ndio muvi zikaanza kurusha ads kwenye tv kama utitiri, zikiwemi muvi kama safari, kaburi la safia, Johari njia panda etc etc
 
Hongera kwa Musa Banzi kwa kutengeneza kazi hii nzuri na nyingine nyingi kama vile Tabana,Game of love,Sakafu wa Moyo,Zogo,Kihongwe,Kiss me,Shenaiza n.k.......Bongo movie ilikuwa na uelekeo mzuri sana mpaka ilipokuwa na uelekeo mbaya
Sababu ya kufa bongo muvi ni mabadiliko ya kiteknolojia

Baada ya vhs kupikuliwa na cd na dvd, ikawa rahisi watu kukopi filamu na pirates wakawa wanapiga pesa, ikashindikana kudhibiti piracy,

Wakati huo ni miaka ya mwanzoni mwa miaka ya 2010.
Wasanii wengi walihisi kuhujumiwa na steps msambazaji mkuu, wakamsema sana hawakujua kuwa steps mwenyewe soko lishaanza kufa.

Hadi mwishoni mwa miaka ya 2010, nyumba nyingi zikawa zimeacha kutumia cd na wanatumia flash. Siku hizi nyumba nyingi hawana hata deki za dvd wanatumia flash

Hivyo tasnia haina pesa, cd hazina soko, na watu wananunua muvi kwa mia tano mia tano kwa mapirates,
 
Sababu ya kufa bongo muvi ni mabadiliko ya kiteknolojia

Baada ya vhs kupikuliwa na cd na dvd, ikawa rahisi watu kukopi filamu na pirates wakawa wanapiga pesa, ikashindikana kudhibiti piracy,

Wakati huo ni miaka ya mwanzoni mwa miaka ya 2010.
Wasanii wengi walihisi kuhujumiwa na steps msambazaji mkuu, wakamsema sana hawakujua kuwa steps mwenyewe siko lishaanza kufa.

Hadi mwishoni mwa miaka ya 2010, nyumba nyingi zikawa zimeacha kutumia cd na wanatumia flash. Siku hizi nyumba nyingi hawana hata deki za dvd wanatumia flash

Hivyo tasnia haina pesa, cd hazina soko, na watu wananunua muvi kwa mia tano mia tano kwa mapirates,
Baada ya watu kuzoea kuona muvi kwa flashi, soko la uhakika la muvi limekuwa gumu kuingia na kupata faida,

Hii imefanya watu wenye fedha kuacha kuinvest kutengeneza muvi, hii inafanya wasanii wazuri, madirector wazuri na hata maproducer kuacha kufanya kazi kwasababu ya ukali wa maisha na kufanya ishu ingine hii ikafanya bongo movie kuwa low quality kuliko za enzi zile za kanumba kipindi watu wako tayari kununua m8kanda na deki walikuwa nazo

Sasa siku hizi kuna platform kama showmax na netflix, shida ya hizi hazifikiki kirahisi na maproducer wa kawaida wa kibongo wasio na pesa ni kama platform za kimagharibi mno na hazilengi maproducer wa Kiafrika na soko letu kwa ujumla, huku platform zetu kama swahiliflix zina changamoto kibao
 
Sasa kama mmenotisi tamthilia ni kali kuliko muvi, jiulizeni kwanini leo bongo muvi ipo chini ila tamthilia kama jua kali, kombolela, nk ni nzuri na zina ubora

Jibu ni kwenye tamthilia ndio kuna pesa

Sasa maproducer wazuri madirector wazuri na waigizaji wazuri na watu wenye hela wanainvest kwenye tamthilia zaidi maana tv stesheni za azam ama dstv na startimes zinawalipa pesa nzuri ndefu tena per episode, maana watanzania washanogewa wananunua ving'amuzi na kulipia vifurushi kila mwezi hivyo pesa ipo huko

Kwahiyo future ya tasnia ya uigizaji tanzania ni tamthilia na hizi paltform za online kama swahiliflix, netflix, showmax etc huko ndio kutaanza kuwa na kazi bora zaidi na zaidi

Sisi tukichelewa wezetu afrika kusini na wanijeriwa metupita mbali, kwao hata mapriducer wenye pesa kidogo wanweza kuweka kazi zao netflix, tena kama nigeria netflix wana ofisi kabisa, showamax nao wanaofisi nairobi na afrika kusini, sisi hatuna connectiin nzuri na platform hizo ndii maana watengeneza filamu na wasanii wake bado hawana pesa kihivyo, hii inafanya wasanii wazuri kukimbia filamu na kuhamia mazima kwenye tamthilia
 
Hamna, bongo movies hawana platform ya kuuzia movies zao. Hilo ndilo tatizo kubwa
Uko sahihi kabisa, hakuna pa kuuzia, hakuna pakurejesha pesa mtu anayoinvest, inafanya wenye pesa kufanyia pesa zao biashara ingine, inafanya wasanii wakose pesa na wale wanaojua hasa kuigiza kuachana na kazi za sanaa, ama wale wenye majin makubwa kuacha kucheza filamu na kufanya kazi za tamthilia peke yake
 
Ubora na viwango pia upo chini huwezi amini insyuka au shumileta ni za zamani lakini bado zikikuwa bora kuliko hizi za sasa.
 
Uko sahihi kabisa, hakuna pa kuuzia, hakuna pakurejesha pesa mtu anayoinvest, inafanya wenye pesa kufanyia pesa zao biashara ingine, inafanya wasanii wakose pesa na wale wanaojua hasa kuigiza kuachana na kazi za sanaa, ama wale wenye majin makubwa kuacha kucheza filamu na kufanya kazi za tamthilia peke yake
Kazi mbovu watu hawanunui mbona kuna movie za kibongo zipo Netflix?
 
Kanumba na wenzie walipoanza kuwaiga Wa Nigeria ndio walipo poteana na hawa wa sasa wanawaiga Wahindi,
Lol [emoji23]
Ubunifu hakuna kabisa huo ndio ukweli.
 
Back
Top Bottom