Sababu ya kufa bongo muvi ni mabadiliko ya kiteknolojia
Baada ya vhs kupikuliwa na cd na dvd, ikawa rahisi watu kukopi filamu na pirates wakawa wanapiga pesa, ikashindikana kudhibiti piracy,
Wakati huo ni miaka ya mwanzoni mwa miaka ya 2010.
Wasanii wengi walihisi kuhujumiwa na steps msambazaji mkuu, wakamsema sana hawakujua kuwa steps mwenyewe siko lishaanza kufa.
Hadi mwishoni mwa miaka ya 2010, nyumba nyingi zikawa zimeacha kutumia cd na wanatumia flash. Siku hizi nyumba nyingi hawana hata deki za dvd wanatumia flash
Hivyo tasnia haina pesa, cd hazina soko, na watu wananunua muvi kwa mia tano mia tano kwa mapirates,