Intelijensia ya Rwanda sio ya mchezo mchezo, kinara wa Hotel Rwanda anashangaa kujikuta Kigali Airport

Kweli kabisa mkuu. Wanyarwanda wenyewe japo nchi yao kijiografia ni ndogo wanaiita "great country" labda kutokana na operations kama hizi
Mmh basi kama hayo wayasemayo itakuwa ni kweli mana mtu anapanda ndege anajua alaelekea position X mwisho wa siku anafika anakuta yupo position Y ni hatar sana intelijensia yao sio ya kitoto kabisa
 

Kuna hakika gani PK hana support ya hao hao wazungu?
 
Mkuu, ripoti rasmi tunazozisoma na kuzisikia ni kwamba Paul Kagame na RPF yake ndio walisimamisha genocide baada ya siku 100 za kuogofya sana ambapo Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuliwa na Interahamwe
"Reports, reports, reports...there will always be reports, but who writes those reports???" Benjamin Wiliam Mkapa on BBC Hardtalk 2001
 
Mwenyewe nimebaki nashangaa
Kagame mwenyewe aliulizwa je,walimteka huyo jamaa?

Akakataa akasema alikamatwa in a 'flawless Operation' na akaendelea kusema:

“He got here on the basis of what he believed and wanted to do,It’s like if you fed somebody with a false story that fits well in his narrative of what he wants to be and he follows it and then finds himself in a place like that.And he will say it, when the time comes, he will tell the people what happened."

So Mpk hapo maelezo ya PK hayajatoa mwanga wa maana wa kitu gani kilitokea nadhani mpk huyo jamaa mwenyewe aliyekamatwa aseme alikamatwaje.

Ningependa kusikia maelezo ya huyo jamaa pia.
 
Kuna hakika gani PK hana support ya hao hao wazungu?
Huyo jamaa wa hotel Rwanda ni raia wa Belgium na Permanent resident wa US, so watu walitegemea hizo nchi zitapiga kelele balaa baada ya kukamatwa kwake lkn cha ajabu Belgium iko zake kimya tu huku US ikisema huyo jamaa awe treated kibinadamu huko mahakamani/police,wahakikishe anapata haki zake na bla bla bla nyingine.

Yaani hakuna kelele za maana sana/za kushtua sana zilizopigwa na wazungu zaidi ni ngo's,HRW na baadhi ya watu binafsi ndio wanapiga kelele kimtindo.
 
Kagame amesema hawakumteka, ni kama unapopiga simu halafu unakuta umekosea namba, ndio hivyo alivyokamatwa hapo Rwanda
Sasa mkuu hio sentensi ya kupiga wrong number maana yake ni nini?
 
Hii Serikali ya Rwanda ni tata sana. Jamaa yangu mmoja (Mnyarwanda) anaiponda sana, lakini ukichat naye WhatsApp au fb utashangaa anavyoitetea. Kama utataka muongee akiwa huru inabidi utumie mitandao mingine ya kijamii kama WeChat (ambayo ni less popular).
 

We have to love our continent and her progress. Hatuwezi kuendelea kupigana nyundo na kutafuta maendeleo. Stability ya DRC, Rwanda, Burundi ni muhimu kwa ustawi wa eneo letu. Hizi approach za kizamani hazina nia njema kabisa na eneo letu
 
Kwanini intelligence ya Rwanda ilishindwa kuzuia mauaji yasitokee?
 
We have to love our continent and her progress. Hatuwezi kuendelea kupigana nyundo na kutafuta maendeleo. Stability ya DRC, Rwanda, Burundi ni muhimu kwa ustawi wa eneo letu. Hizi approach za kizamani hazina nia njema kabisa na eneo letu
Upo sahihi sana mkuu. Nyumba ya jirani haiwezi ikawaka moto kisha ukafikiri kwako patakuwa salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…