Intelijensia ya Rwanda sio ya mchezo mchezo, kinara wa Hotel Rwanda anashangaa kujikuta Kigali Airport

Intelijensia ya Rwanda sio ya mchezo mchezo, kinara wa Hotel Rwanda anashangaa kujikuta Kigali Airport

kutokana na mienendo ya pk kwa wapinzani wake ni vigumu kuamini kwamba alishiriki kutekeleza genocide, wafikirie akina ingabire na wengine wengi, Rusesabagina alianza kumpinga PK waziwazi then he is paying the price, thax god he is alive
 
kwahakika ni kijana wake wa kiume,yuko mafunzoni ya kijeshi US au km karudi atakua yuko kitengo nyeti Kigali
But mmoja wa his son aameshindwa shule huko USA mara mbili na alikamatwa kwa plagiarism na kisha akasusa shule
 
Paul Rusesabina aliyekua Manager wa Hotel Rwanda akiwaokoa Watutsi wasivamiwe na kuchinjwa na Interahamwe hatimaye amefikishwa mbele ya sheria kwa makosa ya kuhusika na njama za mauji hayo hayo.

Baada ya filamu ya Hotel Rwanda kueleza kisa cha Rusesabina, wakati wote dunia ilimuona kama shujaa aliyesaidia kuokoa maisha ya makumi ya Watutsi wasio na hatia waliokimbilia Hotel Rwanda hadi pale uchunguzi ulipofanyika na kugundua naye alikua mmoja wa walioshiriki kutekeleza genocide ile. Suala kama ana hatia au la mahakama itaamua lakini kilichoacha watu midomo wazi ni namna alivyofikishwa Rwanda, maana alikua akiishi Ubelgiji na alishachukua urai wa huko.

Inasemekana alikua Dubai na alidanganywa kupanda ndege ambayo labda aliamini inaenda sehemu nyingine. Kuja kutahamaki anajikuta anashuka Kigali Airport na pingu zikimsubiri!. Kabda ya hapo kuna jamaa wa Kinyarwanda aliandika makala akisema alijipa jukumu la kufuatilia nyendo za Rusesabagina duniani kote na alifanya hivyo kwa miaka 15 na kwa kukamatwa kwa Paul Rusesabagina basi ametimiza kazi yake akiwa kama Mzalendo wa nchi yake! Maofisa wa Rwanda wanasema jamaa amerudi mwenyewe kwa hiyari yake jambo ambalo ndugu wanalikanusha wakidai kua ametekwa, na sababu ni kwamba alianza harakati za kumuondoa madarakani Rais Kagame kwa kuongoza kundi la FNL ambalo Kigali inasema ni lakigaidi.

Serikali ya rais PK kama alivyo yeye mwenyewe ina mkono mrefu na wanamsemo wao kua "There is a price to pay in betraying Rwanda" na kwamba hicho ndio kilichomkuta Paul Rusesabagina.
Umenikumbusha kilichompata Umaru Dikko, alopata kuwa waziri wa Uchukuzi wa Nigeria 1979-1983 enzi za Rais Shehu Shagari, jinsi alivyo rudishwa nyumbani "Kimafia"

Kwa hakika Intelijensia ya Rwanda iko vzr na hasa mlengwa akiwa against PK....
 
shujaa kumbe naye ailikuwa "mdhamini" wa mauaji na msaliti wa nchi yake! (Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa huyu jamaa hasa pale unapoona kiongozi anapewa support kubwa na mataifa ya magharibi na Marekani
Kila jambo lina mwisho wake. Eeh Mwenyeenzi nipe fursa ya kushuhudia anguko la unafiki na ufedhuri huu
 
Umenikumbusha kilichompata Umaru Dikko, alopata kuwa waziri wa Uchukuzi wa Nigeria 1979-1983 enzi za Rais Shehu Shagari, jinsi alivyo rudishwa nyumbani "Kimafia"

Kwa hakika Intelijensia ya Rwanda iko vzr na hasa mlengwa akiwa against PK....
Ni kweli Mkuu, intelijensia yao lazima ipewe heko.

Ile mission ya kumteka Umar Dikko ili fail dakika za mwisho uwanja wa ndege nadhani ni Heathrow pale Uingereza kufuatia maofisa wa England kushtukia dili na kuamuru kifurushi alichokua amefungwa Dikko baada ya kupewa madawa makali ya usingizi kifunguliwe

Nakumbuka kadhia hiyo iliteteresha mahusiano ya kibalozi baina ya UK Nigeria wakati ule
 
Lak
Mbele ya kagame ni kosa kwakuwa unafifilisha slogan ya mauaji ya kimbali amayo kwa PAKA ni mtaji wa kidiplomasia
Lakini wote ni Wanyarwanda na walipitia the same tragedy, kwanini iwe hivyo?!
 
Wazungu wakampa uraia, akapewa tuzo nyingi kama shujaa kumbe naye ailikuwa "mdhamini" wa mauaji na msaliti wa nchi yake! (Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa huyu jamaa hasa pale unapoona kiongozi anapewa support kubwa na mataifa ya magharibi na Marekani) Ingekuwa Tanzania Paul Rusesabagina angekuwa kiongozi wa chama cha siasa au NGO ya kutetea Haki za raia, na hata urais angegombea tu, ila kwa Rwanda ukiisaliti nchi na kuwatumikia "mabeberu" lazima wakuwinde tu!
View attachment 1568411
thibitisha kuwa PR alihusika
 
Rwanda ni uonevu tu, mahakama ya Arusha ina kazi gani?
Kuna wakati Kigali iliilaumu mahakama hiyo kwa kuchukua muda mrefu kusikiliza kesi ambazo wao walikua wanaamini ushahidi wqke uko wazi kabisa
 
Back
Top Bottom