Internet ya bure imeharibu betri ya simu yangu

Internet ya bure imeharibu betri ya simu yangu

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Hello wanajamii forums,

Ni wiki kama mbili sasa tokea kutumia zile apps za wire tun, Thor VPN na HA Tunnel zinazotoa huduma ya free internet kutoka servers za mbali kama vile UK, US, German e.t.c

Simu yangu iliyotoka kiwandani ikiwa na 6000 mAh, ambayo ilimaliza siku 3 pasipo kuchajiwa kwa matumizi ya kawaida pasi na kuwasha data, au masaa 40 kama nitaacha data on! Sasa imegeuka nahisi si zaidi ya 1400 mAh.

Mwanzoni wakati naanza kutumia hizo huduma, simu ilichemka kuliko kawaida, kuna wakati niliiweka kwenye friji ili ipunguze joto, maake nilihisi ingelilipuka. Nimetumia kwa muda sasa kiasi kwamba simu ilichukua masaa sita tu kuwa na chaji. Ndipo nilipoamua kufuta app hizo!

Mbali na kuchukua hatua hiyo, simu yangu inatunza chaji kwa muda wa masaa nane tu, niwashe data, nisiwashe data, niitumie, iwe screen off, niizime, nisiizime! Haya yote yamekuwa bure! Masaa nane tu ndio yaliyobaki kuniweka hewani! Vya bure vimeniponza!
 
Hii inawezekana vipi wataalamu akina CHIEF MKWAWA au unataka hiyo free internet uitumie wewe peke ndio maana unawatisha wenye viinfinix
Mkuu, jaribu kutumia hizo app effectively ndani ya wiki mbili, tena wire tun inaingia hadi YouTube (Server: German2, US4, Canada2), baada ya wiki na nusu urudi hapa tuomboleze kwa pamoja!
 
Unasimu kopo lenye betri bomu unasingizia VPN.
Mkuu, simu yangu ina miezi minne tu tokea kununuliwa, mi ndo nimeitoa bikra mkuu! Naifahamu fika.

Mkuu, VPN za kuingilia sites za warumi kama vile SecureVPN na JAX VPN nimezitumia tokea naanza kuitumia hii simu, lakini hazikuleta effect yoyote! ila hizi za free internet ndo zimeniponza!
 
Huyo hatakuwa ni mnyonyaji wa makampuni ya simu ya ROSTAM AZIZI ana tafuta kututoa kwenye net za bure mbona mimi simu yangu aichemki na natumia kwa zaidi ya miezi 8 hizo huduma za bure
Motivation Speaker! Walete Walete...

Cha ajabu muda huu umeweka bando lako la 1000 ukaamua upitie hapa jf! Ngoja waje...
 
Hello wanajamii forums,

Ni wiki kama mbili sasa tokea kutumia zile apps za wire tun, Thor VPN na HA Tunnel zinazotoa huduma ya free internet kutoka servers za mbali kama vile UK, US, German e.t.c

Simu yangu iliyotoka kiwandani ikiwa na 6000 mAh, ambayo ilimaliza siku 3 pasipo kuchajiwa kwa matumizi ya kawaida pasi na kuwasha data, au masaa 40 kama nitaacha data on! Sasa imegeuka nahisi si zaidi ya 1400 mAh. Mwanzoni wakati naanza kutumia hizo huduma, simu ilichemka kuliko kawaida, kuna wakati niliiweka kwenye friji ili ipunguze joto, maake nilihisi ingelilipuka. Nimetumia kwa muda sasa kiasi kwamba simu ilichukua masaa sita tu kuwa na chaji. Ndipo nilipoamua kufuta app hizo! Mbali na kuchukua hatua hiyo, simu yangu inatunza chaji kwa muda wa masaa nane tu, niwashe data, nisiwashe data, niitumie, iwe screen off, niizime, nisiizime! Haya yote yamekuwa bure! Masaa nane tu ndio yaliyobaki kuniweka hewani! Vya bure vimeniponza!
Wewe ulicho takiwa kutuambia ni kati ya hizo huduma ulizo tumia ni ipi inafanya vizuri zaidi hapo tungekuona una akili timamu .....pia ulitakiwa kuwajulisha wana JF kuhusu hizo huduma ili nao wazijue na kuzitumia kisha walete mrejesho wa kuchemka simu hapo ungekuwa umepata hakika ya sababu ya simu yako kuchemka na kutokukaa na chaji
 
Inawezekanaje hii kitu? Am here waiting or else simu yako imebuma tu
 
Aisee naombeni muongozo wa hizo kitonga internet mie natumia voda na zantel aka tigo
Mbona mimi ninatoa maelezo kila siku hata hapa nipo JF BILA YA BANDO ...TUMIA "THUNDER VPN" ila uwe na raini ya halotel basi utapata intanet bure utatumia ...mimi natumia JF ,TWEET, FACEBOOK, ISTAGRAMU, WHATSAPP, YOUTUBE , GOOGLE BURE SIKU ZOTE ..ILA INAKUWA SLOW KIDOGO
 
Yaani app iaribu betri ?
Danganya watoto

Watu wanafanya mining na simu , na bado ziko freshi
 
Motivation Speaker! Walete Walete...

Cha ajabu muda huu umeweka bando lako la 1000 ukaamua upitie hapa jf! Ngoja waje...
Mimi natumia bando bure natumia hizo app hapa sina bando acheni ubishi nikweli 100% mm mwenyewe nimesha acha kuweka mabando siku nyingi.
 
Back
Top Bottom