Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Ukweli lazima usemwe ili mtu akifa msilete janja janja kutafuta huruma kwa watanzania wote kumbe ni nafasi kwa watu binafsi.Ni ajabu sana nyuzi kama hii kuonekana hapa jukwaani!
Je! Kama lisingalitokea tukio lile la kigaidi la HAMAS lililoiingiza Israeli vitani uzi kama huu ungepanda hapa jukwaani na hoja zake hafifu!?
Je! Vifo vya vijana hawa wa Kitanzania vilitokea katika mazingira gani na vilisababishwa na nani!?
Ukisoma katikati ya mistari, utabaini kuwa hoja zake zimetamalaki chuki za kidini, kikabila ama kikanda, na pia ndizo hasa ambazo zimempelekea mpandisha uzi kuja kihivyo. Yeye pamoja na kujaribu kuzunguka kwake kote lakini kashindwa kuficha hisia zake kuhusu "u-Kaskazini" na "u-Mangi"
Watu wenye nia njema na uzalendo kwa nchi yetu ni lazima waungwe mkono. Zinapotokea fursa na vijana wetu wakaenda nchi za ughaibuni, hiyo inakuwa ni faida kwa nchi yetu. Lakini endapo katika nchi hizo kunatokea "political & social instabilities" ambazo zinapelekea madhila fulani kuwatokea vijani wetu, watu kama hawa hawapaswi kualaumiwa na tena kupitia hisia za udini, ukabila ama ukanda wao.
Kamsikilize yule mzee wa joshua utaelewa.