Interview Rais Samia na Azam TV, azungumzia safari, Urais, Mikopo ya Miradi ya Magufuli, Ripoti ya CAG

amezungumzia miradi mikubwa ambayo ilikuwa ikitekelezwa wakati wa utawala wa Hayati John Magufuli kwa kueleza kuwa alikuwa akiijua lakini changamoto ni kwa kuwa ilikuwa ikiendeshwa kwa fedha za mikopo.
Si tulikuwa tunaambiwa tunajenga kwa fedha za ndani?
 
Nasikia marekani mafuta ni 6,000/= kwa kilo,
Eeh kwa lita
Eti kilo,
Tunawaza unga tuu
Haya twende kazi
 
mbele kwa mbele kijani
 
Jambo hili kulilinganisha na Marekani ni uchache wa Busara kwasababu kuilinganisha kiuchumi Tanzania na Marekani ni upuuzi.
Kulinganisha kipato cha raia wa Tanzania na Marekani ni upumbavu.
Katika hili kilichoongelewa ni PUMBA TUPU
 
Watanzania bwana! Akili zetu kiduchu! Yaani mnakubaliana kabisa na maneno ya huyu mama! Eti sisi tuko bora kuliko marekani! Hivi unaweza kulinganisha nchi hii na mareakni kwa ishu yoyote ile? Na watu mpo mnasifia!
Afu eti sisi tuko bora kuliko Kenya, Rwanda, Uganda, na bado mtapiga makofi? Wenzetu wamepewa subsidy kusudi bei zisipande, sisi tukaambiwa kuwa bei zitapanda tuuu, na kweli zinapanda, na bado mko hapa mnaimba mapambio! Ama kweli wajinga ndiyo waliwao!
 

Mama! Usikute hayo mafuta unalinganisha galoni na lita. Hivi ni vipimo tofauti.

Hallelujah
 
nimesikitishwa na kauli iliyotolewa baada kufananishwa na USA.kila nikipekenyua kujua tunalingana nao vipi japo kidogo .
wajuaji mnaweza kutupa maelezo
 
Yeye yuko wazi tunatekeleza kwa mikopo full stop.. Sio tulidanganywa tutembee kifua mbele eti tunajenga kwa pesa zetu z a ndani kumbe ni mikopo.. Je umeelewa sasa?
Kuna kitu hujaelewa, wakati Mirada inaanza Nchi Wahisani walitaka kutupa mikopo yenye masharti, ndipo kama nchi ikaamua kuanza Mirada hiyo kwa fedha za ndani, hata kama kuna Mikopo si kama anayokopa huyu Mama. Yeye anasema tulijenga kwa pesa zetu lakini tulikopeshwa bila kutoa ufafanuzi kuwa tulikopeshwa na nani? Hata lile daraja pale Kigamboni limejengwa kwa fedha zetu lakini tulikopeshwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii.

Hii nchi ina Rasilimali za kutosha, kama zingesimamiwa vizuri, hii Miradi midogo midogo hii kama ya ujenzi wa madarasa tungeweza kutumia fedha za tozo tu na si kuchukua fedha za COVID.
 
Huyu Mama sijui kama ana Washauri wazuri wa masuala ya kiuchumi, hata kwa akili ndogo huwezi kulinganisha Marekani na Nchi zetu hizi za Afrika, Kule kuna allowance za kutosha, na kipato chao kipo juu hivyo hata kama vitu vikiwa bei juu wana uwezo wa kumudu.

Si kwamba Watanzania akili zao ni kiduchu, isipokuwa imefika mahali Watu wanapenda kuleta ushabiki usio na tija, yaani wanaleta utimu kwenye mambo ya msingi.
 
Sometimes ukijifanya unajua on the other side hujui kama hujui ni kitu kibaya san! Tuliambiwa miradi inayoendelea inaendeshwa kwa pesa za ndani!! Hapo ni Kiswahili lkn bado unahitaj tafsir ili uelewa ama unakaza tu fuvu hapa!!
Kwani kila pesa ya mkopo ni pesa ya nje, kama tulikopeshwa na Makampuni ya ndani je? Kwani lile daraja pale Kigamboni si limetumia pesa za ndani ambazo ni mkopo kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii? Huenda wewe ndiye unayekaza fuvu kuliko huyo unayemshutumu.
 
Kwamba miradi hiyo ilikuwa ikitendeshwa kwa fedha za mikopo. Awali tuliambiwa kuwa fedha iliyotumika ni toka hapa ndani ya nchi. Sasa tunaambiwa vinginevyo. Ama kweli wanasiasa si hasa.
Inawezekana ni fedha za mkopo kutoka ndani ya Nchi, sijaona mahali aliposema vinginevyo, yeye kasema tulijenga kwa fedha zetu lakini za mkopo, kwani lazima kila mkopo uwe wa fedha za nje?
 
hivi kweli mijianaume na midevu yetu tumekaa mwanamke ndiye anaenda kututafutia ?

vya kutafuta ni vingi na mama hajaweka wazi anaenda kutafuta nini sisi tukae tukenue meno tu ataleta
Kwa hiyo unataka tufanyaje? Yeye si ndiye Rais wa Nchi na ameona njia sahihi kwake ni hiyo?
 
Yeye yuko wazi tunatekeleza kwa mikopo full stop.. Sio tulidanganywa tutembee kifua mbele eti tunajenga kwa pesa zetu z a ndani kumbe ni mikopo.. Je umeelewa sasa?
Kwahiyo Kodi zilizokusanywa na magufuli alizikwa nazo!!?
 
Wabongo wengi mna upumbavu mobu , sasa wewe shida yako kama mwananchi ni nini? ni masharti au unataka miradi ifanyike? Hayo masharti umewahi wekewa hadharani tangu awamu ya kwanza ya fisiemu ?
Wewe unaangalia tu kwamba Miradi ifanyike bila kujali inafanyikaje? Unajua kuwa hii Mikopo si misaada? Unajua nani anatakiwa kulipa? Leo hii tumekewa tozo kwenye Miamala ya Simu na tozo ya Jengo kupitia LUKU, ina maana hiyo inamgusa hadi Mwananchi wa hali ya chini, hayo yote yanatokana na huo mzigo wa madeni, ambapo fedha zinazokusanywa zinatumika kulipa madeni badala ya kufanya shughuli za maendeleo.

Sijui kama unafahamu kuwa Mikopo hiyo inalipwa hata sasa? Unafahamu kuwa uwanja wa Ndege wa Entebe pale Uganda ulichukuliwa na Wachina kwa kushindwa kuwalipa madeni? Kuna faida gani hiyo Miradi ikaisha alafu ikachukuliwa na Nchi Wahisani kwa kushindwa kuwalipa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…