Usifanye biashara ya topup ata siku moja. Ni biashara ya kifala haujawahi tokea.
Niliyaka iPhone 11 nikaenda na 8 plain yangu. Wakasema iPhone 11 plain Mil 1 hivi nikasema nikiweka 8 je? Wakakagua wee wakasema nitaongezea 850k. Kwahiyo iPhone 8 yangu ni Laki 1 na Nusu.
Nikasema sawa ngoja nikajipange. Nikamcheki mshikaji wangu nikamwambia akasema nipe namba yao, akawapigia, akasema anaomba used iPhone 8, nyeusi, GB64 battery health kuanzia 90%. Yaani kila kitu kama ile 8 yangu. Wajamaa wakamwambia 450k. Akawaambia anakuja dukani kuicheki sahivi.
Dakika 5 hazijaisha, wananipigia simu wananiambia vipi kwahiyo deal ya top up? Yaani wananibembeleza kabisa.
Kumbe wanataka kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Mi wanipige. Na wamuuzie mtu tena iPhone 8 yangu walionunua kwa 150k waiuze 450k.
Hii biashara ya topup ni bora uuze simu separately, kisha uongeze hela ukanunue simu mwenyewe.