Ipi ‘style’ ya kushangilia goli inayokuvutia kwenye soka?

Kuna yule jamaa wa boca juniors alishinda goli halafu akakimbia akaruka yale mabango ya matangazo akapanda jukwaani akakaa kwenye kiti akaanza kujipigia makofi kana kwamba na yeye ni mshangiliaji,aliporudi uwanjani akala red akatoka🤣

Lakini mi naikubali ile shangilia ya bafetimbi gomis yule mtu mweusi kipindi kile anachezea swansea,jamaa anashangilia kama sokwe hivi..
Hata ile ya mademu kwenye women world cup,kuna demu yule wa paraguay akishinda wanakimbilia kwenye kibendera wanakata viuno kwa kuzunguka huku mikono wameinyosha juu na kwa maringo saaana,aaaah mpira raha sana
 
Staili bora kwangu ni ile ya Selestine Babayaro. Ilikuwa kwenye kombe la Dunia, sikumbuki ni mwaka gani.
Aliruka sarakasi kisha akawa anayumbayumba kama Piere liquid akiwa amelewa.
 
Luis Nani.
Aisee alikuwa na sarakasi hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…