Msaada jamani kwa mwenye uzoefu ama ufahamu wa kutosha naomba nisaidie kujibu hili swali.
Je nitamjuaje nabii wa uongo?
Natanguliza shukrani.
Akianza kuuza mafuta na maji na vinginevyo,akianza kuambatanisha maombi na sadaka kwa maandiko ya agano la kale yale ya zamani ku justify utoaji wa sasa!
Akianza kukuambia toa sadaka KWA kuvunja agano tena anasema kabisa roho wa Mungu kasema utoe sh. Kadhaa kwa AJILI ya HILI na lile huyo ni mchungaji,nabii,mtume,shemasi vyovyote vile wa uongo!!!
Hata kama ni huyu mwalimu mashuhuri akisema ambatanisha maombi na sadaka huo ni wizi!
Yesu hakuponya KWA kuambatanisha na sadaka bali walitoa baada ya kuponywa ndio wakaleta shukrani na sio KABLA ya uponyaji kufanyika!!
Paulo anaandika hivi"NIFUATENI MIMI KAMA JINSI NINAVOMFUATA KRISTO!
YESU HAKUWAAMBIA SADAKA KABLA YA KUTATUA MATATIZO YAO WALA HAKUWAAMBIA ETI WAAMBATANISHE SADAKA KATIKA MAOMBI BALI KILA MTU ATOE KWA SHUKRANI KAMA ALIVOBARIKIWA TENA KAMA DESTURI YA WANA WA MUNGU!!!!
HAKUNA KUAMBATANISHA MAOMBI NA SADAKA BALI SHUKRANI KWA JINSI ULIVOGUSWA!!!
KATIKA ULIMWENGU WA AGANO JIPYA NA UKRISTO HAKUNA SADAKA ZA KUAMBATANISHA ILI MUNGU AKUJIBU BALI NI HAPO KALE!
MAHUBIRI YA KUAMBATANISHA SADAKA NI WIZI ULIOHALALISHWA KWA MAANDIKO YA GANO LA KALE ILI KUFUMBA MACHO WAJIBU WA AGANO JIPYA!!!
HIVYO TU YAANI!!!